Waalimu watishia kuing'oa CCM; Wasema hakuna maisha bora chini ya CCM

Watanzania ni lazima tuwe wakweli. Hivi kweli mtu anadai nyongeza ya mshahara 100% na malupulupu mengine?. Na hao ni waalimu tu bado madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta nyingine mbalimbali. Serikali itapata wapi pesa za kuwalipa mishahara mnayojipangia?.

Ninakubaliana na majibu ya Mh Raisi, kwamba serikali haina uwezo wa kulipa mishahara hiyo. Anayeona hawezi kukubaliana na mshahara uliopo ni vyema aachie ngazi mara moja.

Na bila ubishi kuna mkono wa mtu (Vyama vya upinzani) kwenye migomo yote inayotokea sasa hapa nchini.
 
Hao si walimu ni watu tu kama wewe ndo wenye mawzo hao, suala la hali ya uchumi wa nchi si la chama bali ni mabadiliko ya kiuchumi duniani kote.

Kwa mtu mwenye mawazo finyu kama wewe anaweza kuamini kuwa matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi nyingi ..../SIZE]


we ndo buda kabisa.. hii kauli irresponsible ya kusema eti matatizo ya kiuchumi ni na dunia nzima hutolewa na mijitu ya ccm, na hii inadhirika kuwa ccm mnafikiri kwa kutumia m.sa.b.ri.
 
Hao si walimu ni watu tu kama wewe ndo wenye mawzo hao, suala la hali ya uchumi wa nchi si la chama bali ni mabadiliko ya kiuchumi duniani kote.

Kwa mtu mwenye mawazo finyu kama wewe anaweza kuamini kuwa matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi nyingi duniani kote yanasababishwa na vyama tawala vya nchi hizo, wakati hata nchi nyingine hazina mfumo wa nyama vya siasa.

"Even a fool is thought wise if he keeps silent, and discening if he holds his tongue" Proverbs 17:28
 
Laiti wangalijua haya 2010 na waliambiwa na dr slaa hawakumelewa kuwa ccm ni bomu
 
Mimi bado nasubiri ahadi za JK toka alipoingia madarakani nilihusisha na muda alioubakiza na muda wake ndiyo huo unatokomea. Na huyo mrithi wake wa kampeni "ahadi hewa" sijui ataanzia wapi kupata supporters.
 
Hao si walimu ni watu tu kama wewe ndo wenye mawzo hao, suala la hali ya uchumi wa nchi si la chama bali ni mabadiliko ya kiuchumi duniani kote.

Kwa mtu mwenye mawazo finyu kama wewe anaweza kuamini kuwa matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi nyingi duniani kote yanasababishwa na vyama tawala vya nchi hizo, wakati hata nchi nyingine hazina mfumo wa nyama vya siasa.

Wewe kweli zuzu!! Yaani unataka kusema kuwa matatizo ya sasa ya nchi hii yamesababishwa ba matatizo ya kiuchumi ya dunia?? Kwa hiyo befeore that walimu mambo yao yalikuwa mswano?? Kama mpaka sasa hujui kuwa matatizo ya nchi yetu yamesababishwa nani basi hustahili kuchangia hoja kama hizi.
 
Mimi kwa 100% siziamini hizi trade unions zetu, RAAWU, TUCTA,CWT, CHODAWU, etc, maana naziona ni kama UVCCM, au UWT, wapo kwa maslahi ya nani. Vyama vyote hivi vinawawakilisha wafanyakazi japokuwa wapo kwa sekta zao, ila kilichonivunja nguvu na kunipa wasiwasi na hivi vyama ni kwamba - sijaona tamko lolote la chama chochote kuunga au kutounga mkono harakati za mwenzake! kwa mfano: Madaktari walipoanza harakati zao nilitegemea hivi vyama vingine navyo viwaunge/visiwaunge mkono even hata kwa tamko - vikawa kimya hadi madaktari wakawa jinsi walivyo sasa. Madaktari wakamaliza, wamefuata CWT na walimu ambao nao wamekuja kivyao bila support ya wenzao hadi waliponyamazishwa, sasa wapo jamaa wa Madini - na issue ya miaka 55, hii issue naiona inagusa kila mfanyakazi mmoja na jumuiya yake, lakini sijaona TUCTA, wala yeyote kutoa tamko au kutoa strategy...Sasa hapa naona hawa walimu wakuu wapewa demotion kwa maslahi ya wengi, lakini hadi sasa hakuna any statement kuhusiana na hilo jambo - labda linafanyika kimya kimya:

Ushauri wangu kwa vyama vya wafanyakazi:

1. wafahamu kabisa adui yao ni mmoja - mwajiri
2. Matatizo yao yana fanana kwa maslahi duni
3. wanatakiwa kuwa na mkakati mmoja na nguvu moja "kama wanavyoimba Solidaarity forever"
4. wawe waumini wa solidarity hio na si kwa ajili ya kuimba tu
5. wakipanga vitu kama mingomo basi wajue wawe na uwezo wa kuwalinda wanachama wao ambao kwa namna moja au ingine wataadhirika na matokeo ya mgomo - kuwalipa.
6. wasiwe watu wa kupenda media (vyombo vya habari) - maneno mengi vitendo kidogo

walimu wakuu 10 wavuliwa madaraka kwa kuhamasisha mgomo



Walimu Wakuu 10 wa shule za msingi wilayani Tarime mkoani Mara, wamevuliwa madaraka yao hayo baada ya kubainika kufunga ofisi, kushindwa kulinda mali za shule na wanafunzi na kuhamasisha mgomo kwa walimu wenzao.

Ofisa Elimu wilayani humo, Emanuel Johnson alikiri walimu hao kuvuliwa madaraka yao tangu Agosti mosi, mwaka huu na kwamba bado mchakato unaendelea wa kuwabaini walimu wengine waliohusika na mgomo huo, "Ni kweli tumewavua madaraka Walimu wakuu wa shule za msingi 10 tangu Agosti Mosi na tunaendelea na mchakato wa kuwabaini wengine waliohusika katika kushindwa kulinda mali za shule na wanafunzi na kufunga ofisi za umma na kuwezesha walimu kugoma kufundisha na kuathiri sekta ya elimu," alisema.

Alimtaja mmoja wa Walimu Wakuu waliovuliwa madaraka kuwa ni Esther Magesa wa Shule ya Msingi Mturo ambaye alikamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbili na kuachiwa baada ya kudhaminiwa.

Walimu wengine waliovuliwa madaraka wanatoka shule za msingi za Kwihanche, Reamagwe, Nkerege, Gibaso, Kitagutiti na Nyamwino. Walimu Wakuu wa shule mbili, za Nyankoni na Itiryo, walipewa onyo lakini endapo itabainika kuwa walihusika, na wao watavuliwa madaraka.

Johnson alisema Polisi wilayani humo inamsaka Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Tarime, Matinde Magabe kwa tuhuma za kuchochea mgomo wa walimu, kutoa vitisho kwa walimu waliokataa kugoma na kusababisha uvunjivu wa amani katika baadhi ya shule.



Source: wavuti - wavuti
 
Serikali hii ya ajabu sana yan police wanapewa posho 150,000/, walimu hawapewi,dawa hapa ondoen mfumo mzima utawala(ccm)
 
Walimu kwani lazima mufundishe?? Kama mnawafundisha wanakuja kuwageuka mnahangaikia nini? Toeni mazero yakutosha. Watakapokuwa wengi ndo watakaoing'oa CCM madarakani manake watakuwa wamekata tamaa!
 
Wakiamua, walimu pekee wanaweza kuing'oa CCM, pamoja na vitisho vyake na mahakama za Vodafasta!
 
Walimu sijui walifikiri nini. Kama Madaktari walishindwa, wao walidhania vipi wataweza? Kwa Serikali ya CCM labda wagome Wanajeshi.

Wanaweza, just imagine kila mwalimu akitafuta watu 1000 au hata 100 wakati wa kura 2015 huko vijijini, CCM kwisha.
 
  • Thanks
Reactions: PPM
Kumbe ile Maisha Bora kwa kila Mtanzania ilikuwa haiwahusu waalimu, bado sijabaini kundi lipi hasa ndilo lililokuwa likilengwa.
.

walilengwa mafisadi wanaoiba mamilioni ya fedha kila kukicha halafu wanajifanya kulia machozi ya mamba.

Hawa walimu binafsi nilikuwa nawashangaa, HUWEZI UKAMFUTA MTOTO TONGOTONGO, HALAFU KAKUA, KAJUA KUOGA ANAKUFANYA WE MPUMBAVU, ANAANZA KUKUAMBIA LUGHA ZA KEJELI, ETI " AKILI ZA MBAYUWAYU CHANGANYA NA ZA KWAKO" Hii dharau sana kwa walimu. Walimu lazima wahakikishe hii serikali inawapigia magoti kuwaomba msamaha. Na huo msamaha wasiukubali kwanza na waiadhibu kwa kusaidia kuweka serikali nyingine madarakani.
 
Hao si walimu ni watu tu kama wewe ndo wenye mawzo hao, suala la hali ya uchumi wa nchi si la chama bali ni mabadiliko ya kiuchumi duniani kote.

Kwa mtu mwenye mawazo finyu kama wewe anaweza kuamini kuwa matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi nyingi duniani kote yanasababishwa na vyama tawala vya nchi hizo, wakati hata nchi nyingine hazina mfumo wa nyama vya siasa.

inaonekana mdau ni hafidhina wa kiccm hata kama imekwenda upande hoja ni kuitetea tu mpka mwisho.Kimsingi serikali inatakiwa itumikie umma , bila kujali itikadi.lakini je hakuna ilani na sera za ccm katika kuendesha serikali?hoja ya mabadiliko ya uchumi duniani, ni kipengere pekee cha uchumi wa nchi kudorola na kutoa maisha bora kwa wananchi wake?swali kuendeleza rasirimali katika kuendeleza uzalishaji na kuongeza pato la nchi unahusisha vipi na mdorolo wa uchumi duniani?je hili la uongozi bora, sera nzuri za nchi unaliwekaje pia?ufisadi , uhujumu, uongogozi mbovu , inachagiwa na mdorolo wa uchumi duaniani?Ni lazima tuache visingizio , kutoa mahusisho yasiyo na mantiki kujitetea bila kunagilai uhalisia.Nchi yetu kubwa , hoja ya sera mbovu, uongozi mbovu, watendaji wabovu katika kusimamia rasirimali , ndo mambo yanayolalamikiwa, kiasi kwamba yamesababisha maisha kuwa magumu.leo tunatatizo la nishati ya umeme kuwa tatizo kwa miaka kumi sasa, nalo ni sera za uchumi duniani?mikataba mibovu isiyozingatia usitawi ma masilahi ya umma, nalo ni madiliko ya uchumi duniani?Leo inafikia mpka nchi inaanza kukumbwa na upungufu wa chakula na kusababisha mfumko wa bei, kuhimiza kilimo bora, chenye tija nalo ni mabadiliko ya uchumi duniani?tuache kuttea uzembe na ubovu sera zetu , nchi haiwezi kujengwa na blabla, zenye visingizo visivyo isha.hizo ni siasa mfu zisizo za kizalendo na kuongeza ombwe na ubovu wa uongozi.hapa ccm na sera mfu ndo tatizo, na hasa kipindi hiki ambacho chama cha ccm kinaonekana hakina wanachama , bali kikundi cha kutafuta uraisi.
 
Back
Top Bottom