Waajiri wajitafakari kwenye suala la matumizi ya mtandao

Mwalupale

JF-Expert Member
Apr 29, 2012
1,049
672
Habari wana JF

Nimekaa nimetafakari hili suala nimeona niwashirikishe ili tutafakari kwa pamoja. Ni kuhusu namna hawa waajiri wetu wanavyong'ang'ania mtindo wa kizamani (analojia) katika kufanya recruitment ya watu kwajiri ya kuwaajiri kwenye nafasi mbalimbali kwenye makampuni yao. Kwakweli hii njia ya sanduku la posta inakera sana (P. O. BOX).
Just imagine.. Uko zako sehemu ambayo ofisi za posta ziko mbali alafu mtu kakurushia kimeo kupitia whatsapp ili ujaribu ku-apply ujaribu bahati yako kwasbabu ameona kimeo kimeendana na academic qualification zako unafungua ile kazi unakuta kipengele cha "how to apply" wanakutaka utumie njia ya posta. Kwakweli inakera sana.

Ifike mahala waajiri (hasa ofisi za kibongo) mjiangalie katika hili jambo. Watu sikuizi wanatafuta ajira kwa nguvu sana na mara nyingi wana access kubwa ya mtandao inayoweza kuwawezesha kuomba kazi electronically, sasa nyie mmekazania sanduku la posta ili iweje? Yaani uchome nauli kwenda kutuma barua ya kuomba kazi alafu hauna uhakika kama utaipata hiyo kazi kutokana na nepotism ilivyoshamiri si upuuzi huo.! Hebu waajiri wekeni utaratibu wa kuomba kazi kwa njia ya electronic ili irahisishe mambo. Kama ni kuwachuja mje kuwachuja kwenye interview sio kuwapa watu gharama zisizo na ulazima. Ukiomba kazi tano kwa wiki utasafiri au utakodi bodaboda kwenda post offices mara tano. Sitaki kusema utamlipa bodaboda sh ngapi. Hiyo hainihusu cause sijui umbali wa kila muomba kazi.

Human resource officers wa kibongo njooni tuitumie fursa ya mtandao kuongeza "human capital" kwenye institutions zetu.

Nawasilisha.
 
yan ni kweli kabisa wakati mwingine mtu umefulia ile mbaya ku print cv na kutoa copies of certificates, bado nauli ya kupanda gar kwenda ku post unaweza ata ka 10000 kaka isha kwa maombi mawili tu. saa nyingine had unapotezea
 
human resource officer wengi wa kibongo computer hawajui ndiyo mana unaweza omba kazi kwenye mtandao kwa kupitia e mail zao na usiitwe ila ukatuma kwa kutumia posta ukaitwa na upata,, hata maofisini huwa hawafungui e mail kwa sababu hawajui kutumia mtandao
 
Mtu hauna kazi alafu bado unawapangia watu jinsi ya kufanya kazi.Kila ofisi na utaratibu wake,shirika la posta ni moja ya mashirika machache ya umma yaliyobaki,hivi unafikiri litajiendeshaje hili shirika.
 
Kama kuna HR Officer asiyeweza kutumia mitandao, huyo hastahili kuitwa HR Officer huyo ni personnel officer.

Tiba
 
Mtu hauna kazi alafu bado unawapangia watu jinsi ya kufanya kazi.Kila ofisi na utaratibu wake,shirika la posta ni moja ya mashirika machache ya umma yaliyobaki,hivi unafikiri litajiendeshaje hili shirika.

Mkuu unajivunia shirika la posta? Wameua viwanda na mashirika reputable wanaacha shirika ambalo ni exploitative kwa watanzania wenye hali ya chini. What a shame.! Narudia tena HR wa kibongo wajikite kwenye teknolojia ya mtandao sio kung'ang'ania analogia. Otherwise wataendelea kukosa human capital wazuri na kuajiri liabilities.
 
Lakini ni kweli jamani yani mimi mwenyewe nikiona tangazo la kazi linataka tutume maombi wka njia ya posta huwa nakufa moyo kabisa,na mara nyingi huwa situmi hata kama tangazo lina meet qualification ambazo ninazo kwasababu najua kabisa kuwa napoteza pesa na muda halafu kazi yenyewe sipati.Posta yenyewe iko mbali hadi nipande gari
wajaribu kutumia system ya email bwana kwani huu ni wakati wa kidigital zaidi
 
Habari wana JF

Nimekaa nimetafakari hili suala nimeona niwashirikishe ili tutafakari kwa pamoja. Ni kuhusu namna hawa waajiri wetu wanavyong'ang'ania mtindo wa kizamani (analojia) katika kufanya recruitment ya watu kwajiri ya kuwaajiri kwenye nafasi mbalimbali kwenye makampuni yao. Kwakweli hii njia ya sanduku la posta inakera sana (P. O. BOX).
Just imagine.. Uko zako sehemu ambayo ofisi za posta ziko mbali alafu mtu kakurushia kimeo kupitia whatsapp ili ujaribu ku-apply ujaribu bahati yako kwasbabu ameona kimeo kimeendana na academic qualification zako unafungua ile kazi unakuta kipengele cha "how to apply" wanakutaka utumie njia ya posta. Kwakweli inakera sana.

Ifike mahala waajiri (hasa ofisi za kibongo) mjiangalie katika hili jambo. Watu sikuizi wanatafuta ajira kwa nguvu sana na mara nyingi wana access kubwa ya mtandao inayoweza kuwawezesha kuomba kazi electronically, sasa nyie mmekazania sanduku la posta ili iweje? Yaani uchome nauli kwenda kutuma barua ya kuomba kazi alafu hauna uhakika kama utaipata hiyo kazi kutokana na nepotism ilivyoshamiri si upuuzi huo.! Hebu waajiri wekeni utaratibu wa kuomba kazi kwa njia ya electronic ili irahisishe mambo. Kama ni kuwachuja mje kuwachuja kwenye interview sio kuwapa watu gharama zisizo na ulazima. Ukiomba kazi tano kwa wiki utasafiri au utakodi bodaboda kwenda post offices mara tano. Sitaki kusema utamlipa bodaboda sh ngapi. Hiyo hainihusu cause sijui umbali wa kila muomba kazi.

Human resource officers wa kibongo njooni tuitumie fursa ya mtandao kuongeza "human capital" kwenye institutions zetu.

Nawasilisha.

80% ya Watanzania wanaishi vijijini ambapo
1: 35% ndio wana pata umeme. so internet kwao ni hadithi
2: Huko vijijini cafes zipo nyingi kiasi gani kukidhi.
3: Hata katika miji na majiji yetu bado cafes zipo city centres (Dar-Posta, Mza-Posta, Tanga-posta nk nk)
4: Gharama kwa POSTA kawaida haizidi shs 2000/ affordable internet DKK 30 tshs 800/ ukiscan nondo za kutosha shs 3000/ .
5: Unataka kazi halafu unataka POSTA wapunguziwe kazi hauoni mtakuwa wengi mtaani?
6: Ni miongoni mwa Mashirika ya Umma makongwe yaliyosalia.( ATC TRC Rtc nafco bhesco nk) yamepotea.
7: Naona unapigia debe cafe yako.
 
Hata huko dunia ya kwanza ambapo technolojia iko juu,bado wanatumia posta mpaka leo.sasa sie wabongo kwa kujifanya babukubwa,ndio tunaiponda posta.
 
Marekani, China, UK, German bado posta yatumika kama kawaida. Sisi Tanzania ni Limbukeni ndo maana tumeikimbia Posta. Wao hadi simu za Posta bado zipo sisi hakuna
 
Njia zote yaani oline n posta zitumike kuajiri kama wanavyoajiri NIT ila wasiwasi wangu Hr wengi hawasomi email?
 
80% ya Watanzania wanaishi vijijini ambapo
1: 35% ndio wana pata umeme. so internet kwao ni hadithi
2: Huko vijijini cafes zipo nyingi kiasi gani kukidhi.
3: Hata katika miji na majiji yetu bado cafes zipo city centres (Dar-Posta, Mza-Posta, Tanga-posta nk nk)
4: Gharama kwa POSTA kawaida haizidi shs 2000/ affordable internet DKK 30 tshs 800/ ukiscan nondo za kutosha shs 3000/ .
5: Unataka kazi halafu unataka POSTA wapunguziwe kazi hauoni mtakuwa wengi mtaani?
6: Ni miongoni mwa Mashirika ya Umma makongwe yaliyosalia.( ATC TRC Rtc nafco bhesco nk) yamepotea.
7: Naona unapigia debe cafe yako.

NGOJA NIKUJIBU HOJA ZAKO HAPA CHINI.

1. Kama cafe zipo vijijini basi ni sehemu nzuri kwa kufanya hizo job application.

2. Kama umescan certificates zako zipo kwenye e-mail hauna haja ya kuscan tena mara ya pili. Unachukua zilezile unatuma kwenye application mpya unayoifanya.

3. Hata kama gharama ya posta ni Tsh 2000 lakini kwa watanzania wengi mpaka wafike kwenye ofisi za posta wanaweza kutumia hata elfu 15 au 20 kama wapo vijijini kwenda mjini kupost barua zao. Hata Ofisi zilizipo kwenye miji na majiji kuzifikia lazima kuanzia elfu 5 ikutoke. Ni tofauti na kukaa nyumbani na kutuma application kwenye laptop yako au ya jirani/rafiki yako kwa gharama ya internet bundle ya elfu moja tu.

4. Sijapigia debe cafe yoyote na wala mimi sina internet cafee. Sijasema wafanyakazi wa posta wafukuzwe kwani ofisi zile zina kazi nyingi sio hii tu. Kumbuka hapa naongelea job applications na sio barua za kawaida au nakala za taarifa mbalimbali maofisini, majumbani na kwenye nyanja zingine. Hao wanaweza kuendelea kutumia huduma hizi za posta. Hata huko nje ya nchi huduma za posta zipo lakini waajiri wanarahisisha sana namna ya kufanya recruitments zao.

5. Naendelea kuwashauri waajiri wajikite kwenye ulimwengu wa dijitali. Hata kama wameshindwa basi waweke njia mbili za kuapply kwenye post zao ili watanzania wengi wapate fursa. Ni njia nzuri ya kupata intellectual assets kwenye mashirika yao coz watawafikia watu wengi na kisha watawachuja kwenye interview zao.

Nawasilisha
 
80% ya Watanzania wanaishi vijijini ambapo
1: 35% ndio wana pata umeme. so internet kwao ni hadithi
2: Huko vijijini cafes zipo nyingi kiasi gani kukidhi.
3: Hata katika miji na majiji yetu bado cafes zipo city centres (Dar-Posta, Mza-Posta, Tanga-posta nk nk)
4: Gharama kwa POSTA kawaida haizidi shs 2000/ affordable internet DKK 30 tshs 800/ ukiscan nondo za kutosha shs 3000/ .
5: Unataka kazi halafu unataka POSTA wapunguziwe kazi hauoni mtakuwa wengi mtaani?
6: Ni miongoni mwa Mashirika ya Umma makongwe yaliyosalia.( ATC TRC Rtc nafco bhesco nk) yamepotea.
7: Naona unapigia debe cafe yako.

Cha msingi ni vyema waweke option zote mbili kwenye mode of application,yan electronic(email,recruitment portal etc) na njia ya posta...let them go simultaneously!!
 
Back
Top Bottom