Waafrika ndivyo tulivyo?

Swali, je sisi Waafrika/ watu wenye asili ya Kiafrika ikija kwenye mambo ya michezo na burudani kama vile muziki, tumewazidi wazungu na watu wa asili zingine kama Waasia?
 
Swali, je sisi Waafrika/ watu wenye asili ya Kiafrika ikija kwenye mambo ya michezo na burudani kama vile muziki, tumewazidi wazungu na watu wa asili zingine kama Waasia?

N.Ngabu,
Kuna jamaa wa DRC aliniambia wao wakati wa Mobutu- yeye aliwaambia Wazairwa- nchi yao ni tajiri kwa madini kama gold, almasi -natural forests e.t.c. Kwa hiyo wao washangilie. Ndo miziki ya Bakongo ikaja juu sana kama Ndombolo ya Solo n.k kushangilia kuu utajiri- na Mobutu alipromote sana mziki!
Sasa wakabaki huko2 wanashangilia- wengine wakawa wanaiba madini!
Sijui kama hadi sasa wanshangilia au wameshtuka na kuacha!
 
Swali, je sisi Waafrika/ watu wenye asili ya Kiafrika ikija kwenye mambo ya michezo na burudani kama vile muziki, tumewazidi wazungu na watu wa asili zingine kama Waasia?

...ila angalau huko tunaonyesha upinzani kidogo,hatuko nyuma!

...unajua,wakati mwingine mazingira humfanya mtoto wa kiafrika asiweze kuwa mtu wa maana baadae.

...hebu chukulia wototo weusi waliokuzwa na wazungu,wengi wao hufanikiwa maishani. kwani hujengewa msingi mzuri wa kujitafutia maisha. wawezasema hata connection hupewa labda!

...sasa,utakuta sisi tuna-lack mafunzo na makuzi mazuri ili kuweza ku-compete na wenzetu.

...hebu ona watoto wa shule za awali uropa na amerika wanavyocheza na pc au mac. sasa niambie,watoto wanaofukuzana na matairi yalotumika ya magari watakuwa ligi moja na hawa?
 
Unaona hapo...umesema "wototo weusi waliokuzwa na wazungu,wengi wao hufanikiwa maishani. kwani hujengewa msingi mzuri wa kujitafutia maisha". Why is that?
 
Mliyosema yote ni sawa kabisa, lakini nafikiri factor ya uongozi mmeisahau. Waafrika tumeangushwa sana na viongozi tuliowachagua kwa mbinu za ujanjaujanja na ugizaugiza. Tatizo la pili ni kwamba sisi tumewaachia madaraka makubwa mno viongozi wetu, yaani tunafikiri viongozi wetu wanajua kila kitu na bahati mbaya nao wanafikiri hivyohivyo. Hata kufungua zoezi la kupima virusi vya ukimwi inabidi tumuite Rais badala ya daktari bingwa wa mambo ya virusi vya ukimwi!

Viongozi wetu wanaingia madarakani kwa kuwadanganya wananchi kuwa wanaweza kufanya kila kitu, matokeo yake hawafanyi chochote.

Bottomline: leadership leadership leadership. Tazama pale ambapo wamebahatisha kuchagua viongozi wazuri, tofauti imeonekana, Botswana, Kenya, n.k.
 
Wazee naomba kuuliza swali, hawa kina Balali na mkewe walikuwa kwenye mashirika ya pesa ya kimataifa na waka-perfom perfectly na hatujkusikia negativity, sasa wakishaingia tu serikalini bongo basi tunaanza kusikia noma, je nayo ni low IQ au elimu ndogo?

Just curious?

Mzee ES: ili kupata jibu la swali hili itabidi kusoma kitabu cha Phillip Zimbardo: Lucifer effect: how good people turn evil. Kwa kifupi mwandishi katika kitabu hiki kwa kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali alizofanya anabainisha jinsi ambavyo mazingira ya kishetani yanaweza kumbadilisha hata malaika kuwa shetani. Ametumia mifano mingi kuthibitisha hili.

Kwa maoni yangu, hapa kwetu CCM is a devil's workshop. yeyote aingie huko hawezi kukwepa kuwa shetani. ndio maana tunaona akina JK walikuja na moto wa ajabu wa ari mpya, n.k., lakini leo wamegeuka na wapo complicit na uchafu wote na sasa wanaogopa hata kutamka neno "maisha bora kwa kila mtanzania". tazama akina Mwandosya walivyokuwa clean guys pale UDSM lakini leo huwasikii tena wakikemea uchafu japo kuwa inawezekana wao hawajachafuka. Muone Mkapa alivyoingia madarakani alikuwa mtu clean akiwa na vinyumba viwili, mbuzi kadhaa na viwanja viwili ambavyo havikuendelezwa, lakini leo tazama alivyopata tamaa ya utajiri hadi anataka kumiliki hata nchi yetu yote. Kwa hiyo Balali ni victim wa mazingira ya ushetani yaliyopo katika nchi hii wakiongozwa na CCM. Ndio kusema bila kuishinda CCM itakuwa vigumu kushinda uchafu katika nchi hii; turejee ile thread ya adui yetu ni nani.
 
Mliyosema yote ni sawa kabisa, lakini nafikiri factor ya uongozi mmeisahau. Waafrika tumeangushwa sana na viongozi tuliowachagua kwa mbinu za ujanjaujanja na ugizaugiza. Tatizo la pili ni kwamba sisi tumewaachia madaraka makubwa mno viongozi wetu, yaani tunafikiri viongozi wetu wanajua kila kitu na bahati mbaya nao wanafikiri hivyohivyo. Hata kufungua zoezi la kupima virusi vya ukimwi inabidi tumuite Rais badala ya daktari bingwa wa mambo ya virusi vya ukimwi!

Viongozi wetu wanaingia madarakani kwa kuwadanganya wananchi kuwa wanaweza kufanya kila kitu, matokeo yake hawafanyi chochote.

Bottomline: leadership leadership leadership. Tazama pale ambapo wamebahatisha kuchagua viongozi wazuri, tofauti imeonekana, Botswana, Kenya, n.k.


Mara ya mwisho kuangalia nchi hizi zilikuwa bado kwenye kundi la nchi za ulimwengu wa tatu. Au kama unataka kuzungumzia uongozi bora...inakuwakuwaje uongozi/ utawala dhalimu wa makaburu Afrika Kusini uliweza kujenga uchumi unaoshindana na nchi za Ulaya Magharibi huku wananchi wake walio wengi wakibaguliwa? Je, unaweza kuuita uongozi wao uongozi bora? And, is leadership, leadership, leadership, the single panacea for our economic ills?
 
Lakini Kigezo Kimoja wapo Ili ufanikiwe kuongoza Hayo mashirika Ilipaswa uwe na Kitambi!
 
Njabu Ngabu,
Unajua umetupa mtihani safi sana hapa?...nakupa pongezi labda tunaweza kuipata sababu hasa maanake kuna ukweli ndani ya hoja yako. HALI HALISI ni ushahidi tosha kabisa kwa sisi watu weusi kuwa nyuma pamoja na kwamba tumeandika sababu kibaoo!, nadhani hasi sasa bado kabisa tumeshindwa kuipata sababu moja kubwa.

Kuna jambo moja ambalo kidogo limechomoza akilini mwangu nalo ni kwamba... Inakuwaje pia kuwa nchi za Kiafrika ambazo zimepoteza tamaduni zake (hasa nchi za kusini mwa sahara) ndizo zimekuwa maskini zaidi?, Labda tukiondoa Botswana ambao ni matajiri lakini binafsi naamini kuwa hawana maendeleo kulingana na utajiri wao. Tazama mavazi yetu unajua kwamba sidhani kama kuna mmtu anayefahamu hasa vazi la asili la Mtanganyika!...
Naposema kupoteza tamaduni utagundua kwamba ni nchi hizi za kusini mwa sahara tumekuwa tukijaribu kuiga kila kitu cha mzungu!.. tumekuwa karibu sana na culture zao kuliko wengine wote na sisi ndio tumeshuka zaidi. hata nchi za west Afrika ambazo pia zimekuwa zikikumbatia sana culture za hao wakoloni ndizo zipo chini zaidi!...
Ni hoja tu nimewakilisha inawezekana wenzangu mnao mtazamo tofauti!
 
Hata imani/ dini kuu (hususan ukristu)...tumeletewa. Hata mambo ya serikali kama zilivyo sasa tumeletewa. Ni nini ambacho hatujaiga kutoka kwa wazungu? Wenzetu hata kabla hawajaja kututawala walikuwa na katiba (US) ambayo hadi leo hii na inawezekana hata milele itakuwa relevant....
 
WAZUNGU WENYEWE HAWA? LABDA MZEE OLE ANWEZA KUFAFANUA ZAIDI HII TIOPIKI YA UCHUMI INAKAA VIPI HAPA KWENYE SIASA?
redneck.jpg
 
Blazamen,
Wee subiri kesho utaona linaanzishwa tamasha la mbizi za tope! - kufurahia masika!
 
Kizuri ni kuwa ANAYEJUA KUWA HAJUI NDIO ANAJUA, AU NDIO MWENYE FURSA NZURI YA KUWEZA KUJUA. Leo muulize kiongozi yoyote mtanzania kuhusu hili atakwambia "oo tumepata mafanikio makubwa sana toka enzi za ukoloni mpaka leo" Lakini in fact ukiangalia tumerudi nyuma sana, Angalia shule ile ya Kibaha aliyosoma Kikwete na uangalie shule aliyosoma Ridhiwani uone nani amesoma shule nzuri, angalia elimu aliyopata kikwete na Ridhiwani uone nani amepata elimu nzuri. Wazee wetu wenye rika la kina kikwete wamenufaika sana na system iliyowekwa na wazungu, sisi system tuliyowekewa na wazee wetu ni bogus and rotten. Nadhani tatizo kweli sio elimu, tatizo ni rotten and corrupt system we have, sio tatizo la individuals, angalia nchi kama China rushwa kidogo to issue, Saudia hata wezi hakuna acha wala rushwa, Tanzania wezi ndio wanatanua na kulindwa....nadhani tukubali ukweli kwanza ili tuweze kubadilika.Let us be ashemed of ourselves first........
 
Waafrika weusi bwana! Nenda British schools katika nchi mbalimbali utaona watoto wa mabalozi wa kiafrika, nenda mahospitali Ulaya utaona viongozi wengi tu toka afrika, viongozi wana majumba Ulaya nk lakini wote hawakuanza siasa wakiwa na biashara zingine. Wanaiba ama kufuja mali za umma nasi bado twawaunga mkono tena wengine wanatasema sasa unataka watibiwe wapi, wafe? Lakini bado tunalalama kwa kua nyuma. Hatupo realistic na kutaka maendeleo na ni wabinafsi wa kutupwa. Waulize viongozi watakwambia Tanzania tunaendelea vizuri sana!!!! watasema elimu yetu bomba lakini hutaona watoto wao huko. Ubinafsi tu. Halafu tumewapa madaraka yote lakini hawawezi kuunda efficient systems.
 
Whatever the nature of problems that may contribute to poor levels of education in the majority of people in African countries, the fact is that Africa remains the most economically backward continent due to among other reasons, the inferior education of most Africans.

On the same level, African countries have to import virtually everything (from pins to tractors) from outside because of acute shortage of scientific expertise and technical know-how in their workforce necessary for production and industry.

Now yo don't need to be a rocket scientist to figure out that this would be the perfect recipe for socio economic underdevelopment.

Vicious Reckles Savage,

I find your comments pathetic, vicious and disrespectful.

The level of education among the ruling elite in African countries is the highest. These are the ones who are prepared for long term looting in this continent and neo-colonialism.

Majority of these elite are either Western or US educated, enough to understand that they can establish the looting links from the continent ranging from natural resources,land just to list them to different banks and reserves in western world.

You dont have to ask for anything as I believe you know that,and you have all the facts.

The real question here should be,did Africans need any outside help to develop without any European interference. When I say enterference I mean the distorting or inhibiting effect of previously learned behavior on subsequent learning-right?

We have examples of people whom Europeans and Arabs collaborated with, I mean to cooperate, usually willingly, with an enemy nation, esp. with an enemy occupying one's country, to steal African wealthy.

I find it very difficult to digest what you are saying here!
 
Labda wakati umefika inapotubidi tu re-assess/accept the theory by Dr.Bundara, na sera za U-mimi zilizotutawala
watu weusi, na labda tukubali, hata iweje, "Waafrika Ndivyo Walivyo?"(Tulivyo)
Bitter pill to swallow!
 
No, waafrika ni watu potential sana.

  • Waafrika ni wafuasi wazuri sana wa viongozi wao. Wako kama mbuzi wa shughuli ambaye atamfuta mfugaji wake hadi kwenye shughuli yenyewe na kuchinjiwa huko.
  • Kwa sasa hivi waafrika wengi wana viongozi wa shughuli tu.
  • Ili waafrika wajikwamue, wanahitaji kiongozi mwenye vision nzuri anayeona iliko promised land; wao wanamfuata tu na kumsadia hadi awafikishe huko.

 
Kichuguu umenichekesha kweli...
Kwa vile sisi ni wafuasi hodari...tukimpata huyo kiongozi mwenye vision tutamfuata hadi huko..hata kuwe kuzimu...hatutamstukia kama kachemsha..sisi fuatafuata tu
 
Kichuguu umenichekesha kweli...
Kwa vile sisi ni wafuasi hodari...tukimpata huyo kiongozi mwenye vision tutamfuata hadi huko..hata kuwe kuzimu...hatutamstukia kama kachemsha..sisi fuatafuata tu

That's correct: Ndiyo maana tunawafuata akina Kikwete, Lowasa, Nchimbi, Mkapa, Sumaye na wengineo kwa vile ni viongozi wetu.

Nakumbuka sana jinsi Mkapa alivyotumia neno "wajinga" katika hotuba zake na jinsi ukweli kuhusu jinsi alivyotufanyia wakati huo unavyodhihirisha.
 
Ni nini ambacho hatujaiga kutoka kwa wazungu?

..maneno mengi kazi kidogo!

..ahadi nyingi utekelezaji mdogo!

..kuweka mbele chakula na si jembe!

..uzembe wa kutumia teknologia zilizopo kurahisisha kazi!

..kuweka maslahi binafsi mbele badala ya taifa!

..wizi wa waziwazi wa mali ya umma!

..mdundiko,gombe sugu,chagulaga,n.k!

..vingine wengine wanafahamu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom