Wa Mozambiki hawajui kuwa wao ni wa Msumbiji

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,326
6,841
Hivi mnjua kuwa nchi nyingi tunazitambua kwa majina yao halisi, kama Kenya ni Kenya tu
Zambia ni Zambia tu
Angola ni Angola tu

Lakini Mozambiki inakuwa Msumbiji imekaaje hii jamani?? Kwani hata ukikutana na watu wa Mozambiki ukiwatajia Msumbiji wanashangaa tu..

Nini kimetufanya wa TZ tuwaite wenzetu jina lisilo lao?, na tumelitoa wapi? linamaana gani?
 
msumbiji ndio jina halisi la hiyo nchi, lakini hilo la mozambique (mozambiki), ni la kireno na kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa chini ya ureno kwa muda mrefu, wengi walilijua hilo tu la kireno na si ajabu kwa young generation awalijuhi kabisa hilo la msumbiji
 
Lugha zina namna tofauti ya kutaja majina ya nchi, waingereza wanaiiita Swidi Sweden, waswahili wanaiita Swidi, Waswidi wenyewe wanaiita nchi yao Sveridge.

Waingereza wanaiita Fini Finland, waswahili wanaiita Fini, wafini wenyewe wanaiita Suomi.

Waingereza wanaiita Marekani (US) America, waswahili wanaiita Marekani, wamarekani wenyewe wanaiita America.

Kusema watu wa Msumbiji hawalijui jina hilo ni sawa na kusema wamarekani hawalijui jina la "Marekani".

Msumbiji ni jina la Kiswahili la Mozambique, unless mtu anajua Kiswahili au kawasikia wanaoongea Kiswahili wakiitaja hii nchi kwa jina hili, anaweza asilijue.

Kama vile Marekani lilivyo jina la Kiswahili na Mmarekani asiyejua kiswahili na kutopata nafasi ya kuwasikia wanaoongea kiswahili wakisema nchi yake kwa jina hili, hatajua, rightly so.
 
Back
Top Bottom