Vyuo vikuu UDSM, UDOM mnachelewa nini kumpa udaktari wa heshima Masoud Kipanya

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
482
969
Itoshe kusema ndugu masoud kipanya ni bonge la genius, yaani jamaa ni extraordinary mind anaejua kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia vibonzo, anaegusa mpaka madhaifu ya viongozi wakubwa wa kisiasa bila ya woga. Huyu jamaa ni Mwanaharakati ambae Watanzania tunatakiwa tujivunie sana kuwa nae kwani cartoon zake zinaenda na wakati husika juu ya jambo fulani iwe siasa au mambo ya kijamiii. Bila kupepesa macho kwa Africa hakuna mchora vibonzo (cartoons) anaemfikia masoud kipanya (KP).

Kumekuwa na kasumba hapa tanzania watu hawapongezi au hawaoni juhudi za mtu mpaka afe, mtu akifa kila mtu anasifia ooh alikuwa Mwanaharakati, ooh mpambanaji ooh kaacha alama kwenye jamii.

Swali kwa hivi vyuo vikuu hapa tanzania (UDSM, UDOM) ni lini mtampa kipanya udaktari wa heshima kwa kazi kubwa anayoifanya ya kufikisha ujumbe ktk jamii bila woga??? Au mnasubiri mpaka afe ndio mujifanye kutoa udaktari wa heshima!!! Mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni KP APEWE udaktari wa heshima.



~Gai da Seboga

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Huyu ndio masoud Kipanya`

Wengi humfahamu kwa jina la Masoud Kipanya, lakini hilo si jina lake halisi, tunaweza kusema hilo ni jina lake la sanaa kwani limetokana na na katuni za Kipanya ambazo huwa anachora.

Jina lake ni Ali Masoud, jina la Kipanya ni matokeo ya katuni ya Kipanya aliyoibuni zaidi ya miaka 28 iliyopita. Alizaliwa tareha 23 Juni 1972 jijini Dar es salaam.

Kipanya alianza kuchora katuni akiwa darasa la pili, na alianza kwa kuiga tu katuni za ndani na za nje kama ilivyo kawaida kwa yoyote anayeanza kufanya kitu, ila ‘professionally’ alianza rasmi mwaka 1988, huo ndio mwaka ambao katuni yake ya kwanza ilitoka katika gazeti la Heko.

Amewahi kufanya kazi kama mhariri wa katuni kwenye gazeti la Sanifu na mhariri mtendaji wa katuni gazeti la majira, pia katuni zake hutokea gazeti la Mwananchi.

Licha ya kujizolea umaarufu mkubwa katika uchoraji katuni, katika familia yake hakukuwa na mchoraji kabla yangu, isipokuwa baada ya yeye, mdogo wake naye ameshaanza kuja juu katika fani ya katuni. Licha ya kuwa wazazi wake si wachoraji, lakini mfumo wa maisha yao unatosha kabisa kusema nao pia ni wasanii.

Akizungumzia kazi yake ya uchoraji katuni, Kipanya alisema kuwa, changamoto kubwa anayokumbana nayo ni censorship. Kwa wasioelewa, censorship ni ile kitendo ambacho unachora katuni halafu kabla haijachapishwa inapitiwa na kama itaonekana ina madhara kwa mtu ama jamii Fulani, basi itarekebishwa ama isichapishwe kabisa.

Amesema hayo yamemtokea mara nyingi tu katika maisha yake akiwa katika magazeti mbalimbali. Mara nyingi censorship hutokea pale inapoonekana unachora katuni zinazosumbua mioyo ya walengwa hususani wanasiasa wasiopenda kukosolewa.

Alipoulizwa kama amewahi kupata misukosuko kutokana na katuni zake, Masoud alisema, “nakumbuka siku niliyomchora mtu mnene akiwa amemshika kamba iliyomfunga mbwa ambaye ameandikwa ‘polisi’, maana ya katuni hii ukiangalia kwa haraka haraka ni kwamba jeshi la polisi haliko kwa manufaa ya umma bali kwa manufaa ya watu wachache hasa viongozi wa chama tawala.Hiki kilikuwa ni kile kipindi ambacho wapinzani walikuwa wakibughudhiwa na polisi kila walipotaka kufanya mikutano yao ya hadhara.”

“La pili ni wakati ule mbunge mmoja aliyejulikana kwa jina la Tuntemeke Sanga alipokuwa anaumwa, nilichora katuni inayomuonyesha mheshimiwa Sanga akiwa amelazwa huku akiwa ametundikiwa damu, halafu pembeni yuko serikali akiwa amegeukia upande mwingine huku akivuta sigara kana kwamba hajali, bahati mbaya siku iliyofuata Mzee Sanga akafariki, naikumbuka siku hiyo vizuri, aliyekuwa katibu wa bunge wa wakati huo, Mzee Mlawa, alivamia ofisi za gazeti la majira, bahati nzuri, wakati anaingia mimi nikawa natoka, na pengine kutokana na umbo langu, hakuweza kudhani kwamba pengine huyu ndio masoud kipanya. Kilichoendelea kati yake na mhariri wangu kwa kweli sikukifahamu.”

“Alarm inaniamsha saa 11 alfajiri, naoga, navaa na kuelekea studio. Naanza kipindi saa 12 mpaka 3 asubuhi, baada ya hapo napumzisha akili kwa kama nusu saa kwa kupitia magazeti mbalimbali then naanza kufikiria wazo la katuni, wakati mwingine kama sina wazo hunichukua mpaka nusu saa kudevelop wazo la katuni, by saa 4 asubuhi naanza kuchora editorial cartoon.

Huwa natumia mpaka masaa mawili kutegemeana na aina ya katuni, baada ya hapo, saa sita mchana namkabidhi dereva (wa taxi, sio wangu jamani) apaleke katuni ofisi za gazeti la mwananchi kwa ajili ya kesho yake. Baada ya hapo nageukia upande wa illustrations, mara nyingi huwa nina kazi za taasisi mbalimbali za ku-Simplify text into cartoons kwa ajili popular versions za machapisho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi. By saa 8 mchana huwa nimemaliza, kama kunakuwa na mikutano ofisini naingia, kwa kifupi by saa 10 jioni nakuwa nimemaliza ingawa wakati mwingine humaliza jioni zaidi, baada ya hapo narudi nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo then naenda mazoezini. Nikitoka mazoezini huwa sitoki tena nyumbani,” alisimulia Kipanya wakati akijibu kuhusu ratiba yake kwa siku.

Kipanya, ameshiriki maonyesho mbalimbali Tanzania na Afrika Kusini kama mtaalam wa matumizi ya rangi ‘Painter’ na amejishindia tuzo nyingi ikiwa pamoja na tuzo ya kwanza ya katuni Afrika Mashariki.

Mbali na kuchora katuni, Kipanya ni mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, ni mwanamitindo lakini pia ndiye mbunifu wa vipindi vya runinga vya ‘Maisha Plus’ na ‘Inawezekana.’

IMG_20210201_192505.jpg
IMG_20210201_192936.jpg
IMG_20210201_193344.jpg
images%20(9).jpg
images%20(7).jpg
images%20(8).jpg
 
Ni Ombi la Msingi kabisa.. LAKINI Kuna hili.. kutokana na "nature" ya anachofanya hilo HALIWEZEKANI!

Katuni ni unavyoitafsiri wewe hivyo huwezi kujiamlia kuwa umeelewa kamaanisha hiki kumbe halikuwa alilolenga yeye na pia unavyoitafsiri hivi, mwingine anaitafsiri vile na mwingine HAELEWAGI KABISA katuni hivyo suala la kumtunuku shahada ni gumu kwani anachofanya hakiko wazi kwa UMMA!

Mimi napendekeza wakupewa tuzo ya Shahada ya Uzamivu ya Heshima ni MALISA GJ kwa kujitoa kwake maisha yake kujishughulisha na mambo ya wahitaji!
 
sawa bwana Caisar wa hapo mawingu fm,we mchonganishe tu huyu utamponza
 
Ni Ombi la Msingi kabisa.. LAKINI Kuna hili.. kutokana na "nature" ya anachofanya hilo HALIWEZEKANI!

Katuni ni unavyoitafsiri wewe hivyo huwezi kujiamlia kuwa umeelewa kamaanisha hiki kumbe halikuwa alilolenga yeye na pia unavyoitafsiri hivi, mwingine anaitafsiri vile na mwingine HAELEWAGI KABISA katuni hivyo suala la kumtunuku shahada ni gumu kwani anachofanya hakiko wazi kwa UMMA!

Mimi napendekeza wakupewa tuzo ya Shahada ya Uzamivu ya Heshima ni MALISA GJ kwa kujitoa kwake maisha yake kujishughulisha na mambo ya wahitaji!
Sio kla katun ya kipanya ni ngumu kuielewa, nyingne zpo waz tu znaeleweka na ujumbe unafika ktk jamiii
 
Mbona umetaja vyuo vikuu viwili (UDSM & UDOM)???
Kwani KP alisoma vyuo vyote hivyo??
 
Back
Top Bottom