Vyeti feki: Boniface Jacob afika kamati ya maadili, Makonda amemfanyia vitisho, ahoji uhalali wa Vikao vya CCM Ikulu

Ya leo kali mkuu katoa

Ova
Mkuu inasikitisha kuona kwamba ambaye alitakiwa kutuongoza tuwe na taifa lenye watu wenye uchu wa elimu na wasomi anatusaidia tujenge taifa la watu wasiohitaji kuwa na kiu ya elimu, hii ni hatari sana.
Wakati wao wakisomesha wa kwao ughaibuni waje kuwatawala wa kwetu wasio na elimu kwa dharau ya elimu itakayofuatia.
Kweli Derek Bok alisema "If you think education is expensive, try ignorance" lakini hatujiulizi leo hii chuo kikuu cha Harvard kina nafasi gani kielimu duniani.
 
Muafaka kati ya stelingi na adui kuu huishia kwa adui kuu kumalizwa!


Inabidi hao wawili wajijue nani stelingi na nani adui kuu ili wacheze nafasi zao kwa ufanisi.
 
JInai ni jinai - wote tunajua uteuzi wa mkuu wa Mkoa, wilaya, na teuzi nyingi haziihitaji mtu kuwa na elimu yeyote ndio maana hatuwezi kuendelea kwani tunaongozwa na vilaza wa kutosha- ila katiba yetu inaruhusu hizo teuzi za vilaza na hakuna kipimo cha utendaji wala maadili.

Sheria zetu mama yaani katiba hairuhusu kutumia nyaraka za kughushi hata kama kazi unayoomba haihitaji vyeti.

Kinachopigiwa kelele na kuhusu Bashite sio cheo chake au uteuzi wake la hasha ni kughushi nyaraka au kutumia nyaraka za mtu mwingine kwa udanganyifu.

Leo nchi inasema inahakikia tarehe za kuzaliwa za watu maana yake akikutwa mtu alighushi tarehe yake ya kuzaliwa anakimbizwa kazini.

Vile vile vyeti wengi wamekimbizwa makazini kwasababu ya kuwa na vyeti fake au vya watu wengine.

Hakuna mtu ana wivu ana chuki na teuzi ya aina yeyote anayoifanya Rais anaweza kuteuwa yeyote muda wowote mwenye elimu hata ya darasa moja katiba inamruhusu - ila mteuliewa akiwa na makosa ya jinai -utaratibu unataka uchunguzi ufanyike na kama kuna makosa ashitakiwe.

Mpaka leo hakuna uchunguzi, mhusika hajakanusha na hakuna mtu mwenye mamlaka anataka kuliongelea hili la mkuu wa mji kuwa na vyeti au majina ya kughushi au ya watu.

Hili ni hatari sana kwa ukuaji wa nchi maadili na thamani ya elimu, kuwa safi bila kashfa kwa kiongozi yeyote inatakiwa kuwa ni sharti moja kubwa.

Mamlaka za uteuzi zinakosa weledi wa kushughulikia makosa ya kughushi na ulaghai kwani inaonekana inayabariki.

Kosa ni Kosa hata lifanywe na nani !
 


Meya Boniface Jakob amedai Makonda amemtafuta akitaka wamalizane, jambo ambalo analitafriri kama vitisho.

Meya huyo pia amesema ushahidi wote alioupeleka kwenye shauri hilo, haujapingwa mpaka sasa.

Pia amesema ameambiwa na Makonda afute hiyo kesi kwa kuwa naye alikiuka maadili kwa kufanyia vikao vya chama kwenye ofisi yake ya Meya

Amejibu hilo na kusema yeye hakufanyia kikao cha chama ofisini ila alitembelewa na Sumaye ofisini.

Na akahoji mbona Magufuli anafanyia vikao vya CCM Ikulu?

Akasema sekretarieti ya maadili ya viongozi wa uma itaheshimika milele au itadharaulika milele kulingana na maamuzi watakayofanya juu ya swala hilo.

Amesema pia lengo lake sio kumdhalilisha au kumfanya asiwe mkuu wa mkoa ila kuweka rekodi sawa kuwa amefoji vyeti.

Na wanaopinga kuwa anamfungulia kesi wakati Dar ina matatizo lukuki, anahoji mbona kuna watu waliokuwa wanakaribia kustaafu wamefukuzwa kazi na mafao yao yamegubikwa na utata?

Tupeni Mrejesho...
 
Back
Top Bottom