OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,667
- 105,968
Bongo bahati mbaya
Sijui kama nchi zingine kuna taasisi kubwa kikatiba lakini zimejaa ujanja ujanja kama Bongo.
Siri zimevuja toka kwa Bonny Jacob kwamba sekretariati ilimwambia hakuna mtu aliyewahi kulalamika vikao vya chama kufanyika ikulu. Ikimaanishwa kwamba tume inapokea malalamiko tu na sio kazi yake kuhakikisha maadili ya viongozi yanafuatwa hata kama habari zimezagaa ni lazima waletewe malalamiko.
Kwa maana nyingine hata picha na ushahidi wa maana ukizagaa kwenye media kuna kiongozi anafanya ngono ofisini,tume haina cha kufanya mpaka iletewe malalamiko.
Nimeshtushwa sana. Sheria ya ya maadili ya viongozi wa umma ya 1995 imeweka wazi. Kifungu cha 19(2)(a) kinasema tume itapokea malalamiko.............kifungu cha 19(2) kifungo kidogo cha ''c" kinasema tume itachunguza au kudadisi malalamiko au madai ya kiongozi kukiuka maadili.
Kwa maana nyingine kama kuna jambo la kukiuka maadili linazungumzwa huko duniani tume itamuita muhusika na kumuhoji,sio lazima mtu wa nje alete malalamiko
Hitimisho
Tunaitaka tume imuite Rais Magufuli imuhoji kwa nini anakiuka maadili kwa kufanya vikao vya chama ikulu