Vyama vya upinzani badilisheni mbinu za kisiasa

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,839
Siipendi CCM lakini kwa upande mwingine nikiangalia vyama pinzani (chadem, act, cuf n. K) ambavyo ndio tunategemea viwe washindani na mbadala wa dubwana CCM, niwazi nawaona kama watu walioishiwa mawazo na utashi wa kisiasa, kwa kifupi hawajui ni njia gani sahihi ya wao kuiendea ili kuweza kukabiliana na dubwana ccm. Matokeo yake wamekuwa watu wakukurupuka hovyo na kudandia matukio (siasa za matukio) bila kufikia ukomo wa ufuatiliaji , na nidhahiri kuwa kamati za mahusiano ya kijamii za hivi vyama hazijui wajibu wake na pia viongozi wa vyama hivi ni either ni matapeli na madalali wa kisiasa wanaotafuta kujitajirisha kupitia siasa ama ni watu wasioijua jamii yetu ya waTanzania inataka nini na wakati gani au yote mawili.

Kuitoa ccm kupitia sanduku la kura sio kazi nyepesi, it's almost impossible!, inahitajika mbinu na mkakati wa muda mrefu, zaidi ya siasa za mkataba wa bandari, wamasai ngorongoro, mauji ya mamba mkubwa. Sisemi hawapaswi kuyakemea haya bali wasiyafanye kama ajenda kuu za kimkakati katika chaguzi sababu waTanzania walio wengi wanauelewa mdogo sana kuhusu masuala ya kimikataba hivyo kupanda majukwaani na kuwalisha nadharia hizo ni kuwachanganya.

CCM itatolewa madarakani na sisi wananchi kwa kushirikiana na wana ccm wenyewe kupitia mashinikizo makubwa ya kijamii kama MAANDAMANO na migomo ya amani. Lakini je? nyie chadema, Act wazalendo, cuf na vyama vingine pinzani, do you have all it takes kutengeneza haya mashinikizo na kupata uungwaji mkono wa walau asilimia 60 ya wananchi?. Je mienendo yenu ya kisiasa na kimaisha inatosha kuwafanya waTanzania wanyonge na masikini wahamasike kuacha shughuli za kulisha familia zao kisha wayaweke maisha yao rehani kwa ajili ya mabadikiko?.

JIBU NI HAPANA! Nyie wapinzani, you don't have all it takes kutuhamasisha. Maandiko yanasema "yule atakayetaka kuilinda nafsi yake ataipoteza, na aliye tayari kuipoteza ataokolewa" hamuwezi kuja kukurupuka na kuwaambia watu waandamane huku mkiwa ndani ya mahekalu yenu, Je mnamahusiano gani na wananchi mbali na kuwahutubia kuhusu bandari, ngorongoro, na mamba?.N sacrifices zipi mmefanya kwa ajili ya waTanzania masikini mbali na zile za kutetea ubunge wenu na uongozi ili mtunishe mifuko yenu?

Kundi kubwa la sisi waTanzania ni illiteracy, na masikini wenye uhitaji wa karibu kila kitu, hivi mnajiuliza kwanini huko vijijini watu wako radhi hata wauliwe kwa sababu ya ccm?. Ni kwa sababu masikini anaishi kwa ajiri ya Leo tu, masikini haiwazi kesho yake isipokuwa kushiba siku husika kwanza, ndio maana kupitia kanga na kofia na elfu 3 mkononi CCM inapata uungwaji mkono, sababu sisi masikini hushukuru kwa kidogo. Hivyo katika kulipa fadhila hizo, watu hao wa vijijini wako tayari KUFA kwa ajili ya nyerere au kingunge ambaa hata hawajui kama wako hai au walikufa, ila tu sababu ndie baba wa taifa, baba wa ccm chama kilichowapa känga, maandazi na skonzi

Wito wangu kwenu enyi wapinzani, nendeni mkaguse maisha ya wananchi moja kwa moja, tengenezeni miradi ya kijamii, saidieni mashule, saidieni mayatima, somesheni watoto wa masikini pale mnapoweza, tuonyesheni nia yenu njema kwanza kisha mje mtuambie tuandamane muone kama hamto pata maelfu ya watu barabarani. Lakini siasa zenu za matukio na majigambo ya kifedha kwa wananchi wanyonge, nasikitika kuwa kamwe hazitowapatia ushindi. Kwa kusema hayo nihitimishe kwa kuweka wazi kuwa uchaguzi wa 2025, wapinzani utumieni kama mechi ya kirafiki sababu hamna sifa stahiki za kukabiziwa taifa kupitia sanduku la kura katika uchaguzi huo. Kwa kifupi hamkopesheki na wala hamuaniki
 
Back
Top Bottom