ZANZIBAR: Vyama 9 havitashiriki Uchaguzi wa Marudio wa Machi 20

Green Bird

Senior Member
Jan 26, 2016
101
81
Vyama tisa vya siasa kati ya 14 vilivyosiriki uchaguzi Mkuu mwaka jana vimeungana na CUF kutoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika machi 20, hadi utakapo patikana muafaka wa kumaliza mgogoro wa kisiasa.

Mratibu wa umoja wa vyama hivyo, Kasim Bakari Ali Alisema jana kuwa Vyama hivyo vilikutana unguja na kupitisha maazimio mawili ya kutoshiriki uchaguzi huo.

Vyama hivyo ni UMD, Jahazi Asilia, Chaumma, UPDP, DP, CCK na ACT Wazalendo. Ushiriki wa vyama vya ADC na CCK bado una utata kutokana na wagombea wake kutangaza kushiriki licha ya vyama vyao kuwa na msimamo tofauti, hali iliyosababisha wagombea hao kusimamishwa.

Vyama ambavyo vimetangaza kushiriki marudio hayo hadi sasa ni CCM, Tadea, TLP, Sau na AFP.
Kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita, Zanzibar imeendelea kuwa kwenye mgogoro wa kisiasa kati ya vyama vikubwa vinavyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) baada ya CUF kususia marudio ya uchaguzi baada ya ule wa awali kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Akitaja maazimio ya vyama hivyo, Kassim alisema wamekubaliana kutoshiriki marudio ya uchaguzi huo hadi mgogoro wa CCM na CUF utakapomalizika na wameunda kamati ya wajumbe 18 ya wenyeviti na makatibu wa kila chama ili kuanzisha meza ya kutafuta suluhu ya mvutano uliopo kati ya CCM na CUF.

“Tutaanza kukaa na viongozi wa vyama hivyo kila upande kujua ni nini hasa hatima ya mvutano huo na tunajikwamuaje,” alisema.

Ali ambaye pia ni mwenyekiti wa Jahazi Asilia alisema mgogoro wa Zanzibar utamalizwa na Wazanzibari wenyewe, hivyo ni vyema viongozi hao wa kisiasa wakajenga uvumilivu katika kutafuta mwafaka.

Alisema tatizo la vyama hivyo siyo kushiriki marudio ya uchaguzi huo tu bali ni kuangalia chanzo na hatima ya mgogoro huo kwa masilahi ya Wazanzibari.

Mwenyekiti wa CCK, Constatine Akitanda aliwaambia waandishi wa habari kuwa uamuzi wa kusimamishwa uanachama kwa mgombea wake wa urais, Ali Khatibu Ali, unakwenda sanjari na kutoshiriki uchaguzi hadi maridhiano ya CUF na CCM yapatikane.

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia AFP, Said Soud Said alisema jana kwamba, chama hicho kimekubali kurudia uchaguzi huo.

“Lengo la chama chetu ni kushika dola, sasa tusiposhiriki itakuwaje? Kwanza hatuamini kama CUF haijatendewa haki kwa sababu ni kweli kulikuwa na udhaifu, mfano vurugu za kituo cha kupigia kura cha Matrekta Wawi,” alisema.

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema kama vyama hivyo viliiamini ZEC katika uchaguzi uliopita, vinatakiwa kuiamini kwenye marudio hayo kwa kuwa hakuna mbadala.

“Naomba wakubali kurudia uchaguzi kwani ‘maji yalishamwagika na kuzoleka haiwezekani… Nani aliyekwenda mahakamani kupinga? Wanachoogopa kurudia ni kitu gani kama walishinda?”alihoji Mrema. [/COLOR][/SIZE][/FONT]
 
Shukrani . makala nzuri
http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
Hahaha,usitishike mkuu.
Tuliopo Zanzibar tunajua kwanini hawashiriki.
Nchi za Africa ukisusia uchaguzi usifikirie kuna ushauri au msaada wowote unaoupata kutoa nje.
Ngoma itapigwa na wao watakuwa wapole,wenye kula bingo wanakula na waliochelewa imekula kwao.

Ni msimu wa mavuno kwa baadhi ya wajanja ndani ya vyama vya siasa,atakaekosa hapa ndio basi tena anakufa maskini.
Wabunge wa UKAWA kukubali tu,kuapa wakati walitakiwa kugoma ili shinikizo liwe kubwa,pale ndio wamewauza wenzao wa CUF.
Na hapa hata kikibakia cha kimoja ngoma inapigwa,maana CUF wao zamanii wabunge wapo mjengoni wanakula Bingo kwa mgongo wa mbele.Hahahahaha
CCM acha wafanye yao,hawa jamaa wengine kabisaaaa,Nawapongeza sana Chadema kwa kuwawekea mazingira hayo CUF,the super trap machine
 
Navpongeza vyama vyote vilivyojitoa kwnye uchaguzi, vinanyesha ukomavu na uelewa wa mambo ya udharimu unavyowaenyesha watu wa zanzibar
 
Baadhi ya vyama vilivyofikia uamzi huo ni,
Chauma, SAU, DP, Demokrasia Makini, Jahazi Asilia, NRA, UPDP na UMD.

Tunakoelekea mwisho Jecha atabaki na chama kimoja CCM, kwa maana hiyo hakutakuwa na haja ya kufanya uchaguzi na kupoteza pesa za mlipakodi, ni heri kumtangaza Shein mshindi.
 
Haya yasije kuwa yale ya 'wewe susa wenzio twala'...
Watu watapiga mihayo miaka mitano....
Ndio maana niliwasikia madiwani wa CUF wakisema hilo la kurudia uchaguzi haliwahusu maana wao walishatangazwa...chezea u jobless wewe
 
Hahaha,usitishike mkuu.
Tuliopo Zanzibar tunajua kwanini hawashiriki.
Nchi za Africa ukisusia uchaguzi usifikirie kuna ushauri au msaada wowote unaoupata kutoa nje.
Ngoma itapigwa na wao watakuwa wapole,wenye kula bingo wanakula na waliochelewa imekula kwao.

Ni msimu wa mavuno kwa baadhi ya wajanja ndani ya vyama vya siasa,atakaekosa hapa ndio basi tena anakufa maskini.
Wabunge wa UKAWA kukubali tu,kuapa wakati walitakiwa kugoma ili shinikizo liwe kubwa,pale ndio wamewauza wenzao wa CUF.
Na hapa hata kikibakia cha kimoja ngoma inapigwa,maana CUF wao zamanii wabunge wapo mjengoni wanakula Bingo kwa mgongo wa mbele.Hahahahaha
CCM acha wafanye yao,hawa jamaa wengine kabisaaaa,Nawapongeza sana Chadema kwa kuwawekea mazingira hayo CUF,the super trap machine
Uchaguzi uliokamilika hauna marejeo,huo unaosema ni uchaguzi wa ccm kwani uchaguzi wa nchi ulikwisha fanyika kitambo.
 
TLP ni jumuia ya ccm

Bungeni, Kumbe huku kuna raha hivi.gif
 
Back
Top Bottom