Vurugu za kidini: Serikali yaifungia Sekondari ya Magambani

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]06/11/2012





Serikali wilayani Bagamoyo leo imetangaza kuifunga Shule ya Sekondari Bagamoyo maarufu kama Magambani kwa muda usiojulikana kutokana na madai ya kuzuka ghasia za kidini.


Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, imeelezwa kwamba ulifanyika uchaguzi wa Kiongozi wa wanafunzi shuleni hapo ambapo wagombea walikuwa ni wawili, mmoja wa dini ya Kikristo na mwingine Kiislamu.


Baada ya matokeo kutangazwa na mgombea kutoka dini ya Kikristo kushinda, inadaiwa kwamba wanafunzi wa Kiislamu walipinga matokeo hayo na ndipo ghasia hizo zikazuka.


Pia kulikuwa na madai kwamba wanafunzi wa Kiislamu walipanga kuchoma moto majengo ya shule hiyo, hivyo wanafunzi wa Kikristo kutakiwa kuondoka haraka kwenye maeneo ya shule hiyo.


Lakini chanzo cha habari kimesema baadhi ya wanafunzi wa shule waliohojiwa kwa nyakati tofauti wamekanusha kuwa na tofauti hizo za kidini na kusisitiza kwamba ni kampeni chafu ya baadhi ya walimu wanaopandikiza mbegu mbaya ya udini miongoni mwa wanafunzi ili kuleta mtafaruku shuleni hapo.


Wameendelea kukieleza chanzo cha habari kwamba, katika siku za karibuni walimu hao wamefikia hata kuwapachika majina wanafunzi hao kama Al-Shaabab, Al-Qaeda n.k.


Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wameelezea kusikitishwa kwao na hatua hiyo ya kuifunga shule hiyo hasa kwa kuzingatia kwamba wanakabiliwa na mitihani yao ya mwisho na hivyo kushindwa kujua hatima yao.


Shule hiyo imeelezwa kwamba inamilikiwa kwa pamoja na Wizara ya Elimu na Tamisemi.


---
via Ziro99 blog



Source: wavuti.com - wavuti
 

Lazima SERIKALI ya CCM na Wanaopenda USALAMA wa NCHI - Kuhakikisha kuwa MASUALA kama haya HAYATOKEI TENA NCHI yetu kama hata WASOMI wanaanza KUJIGAWA; TUNAELEKEA SOMALIA...

Nasema hivyo kwasababu TUMECHANGANYIKA kweli kati YETU WAISLAMU na WAKRISTO
 
Huu ni mwanzo tu, mengi yanakuja.

Daima vizazi vyote vya Tanzania vitamkumbuka Kikwete kwa kupandikiza udini ndani ya nchi yetu.
 
Mkuu je hii ni shule nyingine tofauti na ile ya mwanafunzi wakiislam wanaotaka kumfukuza mwalimu mkuu wao, maana nayo iko bagamoyo?
 
Huu ni mwanzo tu, mengi yanakuja.

Daima vizazi vyote vya Tanzania vitamkumbuka Kikwete kwa kupandikiza udini ndani ya nchi yetu.

burned but no flames yet in a moment it will smoke and rapidly the flame will consume us all nothing/nobody will remain standing, you will only find peace in your grave.
 
Kweli tunamhitaji Mungu katika hili. Kila anayeliona hili aingie magotini, lawama hazitatufikisha mbali ndugu zangu. Mungu atupe macho ya Rohoni tuone wajibu wetu katika masuala haya. Ni kweli JK alitufikisha hapa lakini omba macho ya ndani uone nyuma ya pazia ili ufanye kazi yako
 
wapandaji wa mbegu hizi ni KANISA KATOLIKI NA CHADEMA ILI WAMPELEKE PADRI SLAA IKULU lakini akawapiga laana hawakufanikiwa. JK alipokuja kulisema katika viwanja vya jangwani MAASKOFU wakamrukia miguu miwili, mmelikoroga sasa mtalinywa.
 
Kikwete, lengo lako ni kutumia damu ya watu kupigia mswaki na kunawia uso kila uamkapo asubuhi. Utatimiza adhma yako, but the history will leave no stone unturned.
 
wapandaji wa mbegu hizi ni KANISA KATOLIKI NA CHADEMA ILI WAMPELEKE PADRI SLAA IKULU lakini akawapiga laana hawakufanikiwa. JK alipokuja kulisema katika viwanja vya jangwani MAASKOFU wakamrukia miguu miwili, mmelikoroga sasa mtalinywa.

vipi, umeandaa mapanga mangapi? . Shetani hupenda damu. Damu ni juisi ya shetani. Yeyote afurahie kumwaga damu ni wakala wa shetani.
 
watu wenye ubongo mdogo wanabaguana kwa misingi ya dini, ni bahati mbaya kuwa katika nchi hii watu wenye ubongo mdogo wanaongezeka kwa kasi, wanatoka dini zote, rika zote, wasomi kwa wasio wasomi, wanasiasa kwa wanazuoni, agggh tumekwisha!
 
Back
Top Bottom