Vurugu Bugando: Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa inadaiwa kakamatwa na Polisi

At least wewe tumeongea neno la busara..
Kuna issues zingine police hawatumii busara kabisa, watu wamefiwa wanapeleka mwili wa mpendwa wao alafu police wanawatawanya kwa mabomu.
Ukizingatia kifo cha mawazo lazima tension ntakuwa high kuanzia siku ya kifo Chale hadi siku ya mazishi.so kwa kutumia busara za buree ambazo hauitaj rocket science polisi wangekaa pembeni coz hao wapendwa wa mawazo washajazwa simu kwamba police wa naweza kuwa wameusika kwa namna moja au nyingine.
Nashangaa vitu vyepesi kama hivi hata makamanda wa police wanashindwa kuvielewa.!!

Hapa ndo napata wakati mgumu, kwenye msiba kama ule wenye tension kubwa sana tena ktk kipindi hiki wangeshiriki kuwalinda wananchi wausindikize mwili wa mpendwa wao mpaka eneo husika na sio kuwatawanya kwa mabomu, naamini watu wasingeufanyia jambo baya mwili wa marehemu wao wanahuzunika na huo ndo utamaduni wetu kisindikiza misiba kwa mapambio na hata vilio. Polisi wetu wajifunze kutumia akili na busara zaid na sio nguvu kwani saa nyingine zinazaa uhalifu na chuki.
 
Hivi ukishakuwa polisi ubinadamu unakutoka kana kwamba hukuzaliwa kama Alphonse Mawazo,mtu kanyang'anywa kinyama haki yake ya kuishi wapendwa wake wanataka kuhifadhi mabaki yake nao wanapatilizwa na dola,je mzee wa HAPA KAZI TU tumueleweje. Tafakari
 
Nitafurahi kama huyo mwenyekiti wa bavicha kipelekwa mahamani na kufungwa liwe fundisho kwa nyumbu nyie mjue kuheshimu sheria

kwani CDM wameanza kukamatwa na polisi Leo? huyu ataachiwa huru kama wengine
 
At least wewe tumeongea neno la busara..
Kuna issues zingine police hawatumii busara kabisa, watu wamefiwa wanapeleka mwili wa mpendwa wao alafu police wanawatawanya kwa mabomu.
Ukizingatia kifo cha mawazo lazima tension ntakuwa high kuanzia siku ya kifo Chale hadi siku ya mazishi.so kwa kutumia busara za buree ambazo hauitaj rocket science polisi wangekaa pembeni coz hao wapendwa wa mawazo washajazwa simu kwamba police wa naweza kuwa wameusika kwa namna moja au nyingine.
Nashangaa vitu vyepesi kama hivi hata makamanda wa police wanashindwa kuvielewa.!!
Sio kwamba hawaelewi, ni makusudi....utemi....utemi
 
Imekuwa ni kawaida hasa kwa viongozi wa Chadema@Ukawa mara nyingi kutoa vitisho vya kumwaga damu. Sisi wapenda nchi yetu na mabadiliko ya ukweli tunasema tuko tayari kwa lolote iwe vita iwe chochote. Tunawataka viongozi wa juu wa Ccm nao watoe tamko tuanze kunoa shoka zetu.

Hawa jamaa wa ajabu sana wanamtafuta mchawi aliyemkosea mgombea waliemkodi ambaye ni Mbowe na genge lake mnalia na tume,serikali na Ccm.

Kama tulivyomwambia Lowassa ni mamluki na wanafiki ndio watamfata naona hajatuelewa bado licha ya kuukosa urais.
TUNASEMA TUKO TAYARI ANZENI TUMALIZE
kamanda Mbowe itisha mkutano na wanahabari mara moja na kutoa tamko zito na hali ya hatari,hatukubali na hatutakubali unyama huu
 
Hapa ndo napata wakati mgumu, kwenye msiba kama ule wenye tension kubwa sana tena ktk kipindi hiki wangeshiriki kuwalinda wananchi wausindikize mwili wa mpendwa wao mpaka eneo husika na sio kuwatawanya kwa mabomu, naamini watu wasingeufanyia jambo baya mwili wa marehemu wao wanahuzunika na huo ndo utamaduni wetu kisindikiza misiba kwa mapambio na hata vilio. Polisi wetu wajifunze kutumia akili na busara zaid na sio nguvu kwani saa nyingine zinazaa uhalifu na chuki.
Wanatii amri halali.
 
ukimpiga ocd kutokana na ukorofi wake utakuwa umenyea kambi na utaisoma namba,ila ukimuua Alphonce mawazo kutokana tu na itikadi yake utapewa heshima kubwa na kuonekana shujaa kwa wana ccm,kipimo kilekile ulichopimia ndicho utakachopimiwa.

Mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu! iweje polis wanakuja kupiga mabomu hospital wanawasumbua wagonjwa? Tena wale wagonjwa wa moyo wamepata mishituko mikubwa sana.
 
kwani CDM wameanza kukamatwa na polisi Leo? huyu ataachiwa huru kama wengine

Huo ndio udhaifu wa sheria zetu,hata wale waliomuua walijua huyo Mawazo akipelekwa Polisi kwa amri aliyotoa ya kupigwa wanaccm angetoka tu ndio maana wakammaliza kabisa
 
Haya ni majungu, inaonekana mtoa mada anamihemko.

Nakushauri mtoa mada tulia weka pembeni mihemko na andika tena thread hiii upya na kwa taarifa hii yako tuiamini Jeshi la Polis na kama mnajisifu kumpiga OCD Wa Wilaya sasa mmenyea kambi na mtaisoma namba

Oh really? Unadhani tutakuwa tunauawa sisi tu?

Wwe na polisi mtakuwa mnakaa, mnashinda na kulala wote pamoja na familia zenu kila siku?

Unadhani polisi wote wanafurahia mauaji ya wapinzani?

Hatuna bunduki lakini tuna mioyo na Mungu.

Ikibidi bunduki, hatutazipata kutoka sehemu yoyote zaidi ya maghala ya silaha ya polisi na jeshi na tutapewa na polisi hao hao.

Ccm mko wachache sana usisahau.

Sasa mmelianzisha, tazameni nani ataisoma namba.
 
kamanda Mbowe itisha mkutano na wanahabari mara moja na kutoa tamko zito na hali ya hatari,hatukubali na hatutakubali unyama huu

Hivi wewe unaelewa unachosema hapa? Mbowe ndio nani? Ana mamlaka hata ya kumuamuru askari mmoja tu cha kufanya? Hebu tushirikishe na ubongo tunapoandika. Nchi ina dola na majeshi, Mbowe hana mamlaka hiyo. Yeye mwenyewe anaweza kukamatwa akaswekwa ndani kwanza akithubutu kuchezea dola.
 
hapo kwenye polisi na ocd kupigwa kama pana ukweli nimepapenda

Ujue wananchi ni wengi kuliko polisi wakiamua kufanya chochote polis hawataweza kuwazuia, inapaswa polis waache kufanya kazi kwa niaba ya ccm wafanye kazi kwa manufaa ya Taifa.
 
Nitafurahi kama huyo mwenyekiti wa bavicha kipelekwa mahamani na kufungwa liwe fundisho kwa nyumbu nyie mjue kuheshimu sheria

naona unaongea uku umepakatwa na Kinana mshedede ukikuingia vizuuuli!!kazi njema.....
 
Mimi naomba nielimishwe tu, nipo Dar lakini picha nilizoziona Mawazo ameuwawa kwa kushambuliwa na alipoteza damu nyingi akakata roho, bado sioni mantiki ya mwili kupelekwa Bugando wanakwenda kuchunguza nini? wakati hata miye nisiye daktari najuwa kilichomuuwa? Nilitegemea kusikia walioshiriki mauwaji haya wamekatwa na si vinginevyo
 
Sio kwamba hawaelewi, ni makusudi....utemi....utemi

Ukiona police wanatumia nguvu isiyo ya kawaida basi ujue raia wanakaidi na kutunisha misuli kwa jeshi. Na jeshi halina muda wa kubembelezana, wao ni amri, hutaki basi lazima upate kichapo. Raia ni wakorofi na wengi ni viroba. Mtu anayejielewa hawezi kushindana na maagizo ya jeshi. Ni kujitoa ufahamu tu ili ionekane polisi wanaonea lakini ukweli ndio huo.
 
Back
Top Bottom