Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,599
Wazanzibar mnajua sana Kiswahili, labda utanielewa kwa hili: Inzi akikuzunguka zunguka usoni ndio kero. Mbu akikuuma, au nyoka, ni tatizo, anaweza kukuua. Muungano sio kero, ni matatizo. Kwa nini hatutumii Kiswahili fasaha kuelezea matatizo yetu?
Mtanganyika nikilipishwa ushuru wa mamilioni kwa kuingiza gari Tanganyika kutokea Zanzibar, hayo mamilioni ni kero au tatizo?
Ninapoona nyumba za ibada za dini isiyokuwa popular Zanzibar zinachomwa moto wakati wao wamejaa Bara huku wanafanya shughuli zao hakuna anaewabughudhi hiyo ni kero au kutafutana vita?
Ninapoona Bunge limejaa wawakilishi kutoka Zanzibar tofauti na uwiano wao, hayo mabilioni ya kugharimia hawa wabunge wa kigeni ni kero au balaa?
Ninapoona waziri wa Zanzibar anatangaza hadharani kimabavu kwamba hatalipia Umeme wakati mimi Mtanganyika sithubutu kuikoromea TANESCO, hiyo ni kero au uonevu?
Ninapoona nusu ya mabalozi, mawaziri wa Muungano, viongozi wa vyama, wanatoka sehemu moja ndoooogo ya nchi, hiyo ni kero au upendeleo?
Ninapoona kura yangu haina nguvu ikilinganishwa na Mzanzibar kwa sababu ya uwakilishi mkubwa wa Wazanzibar kwenye vyombo vya maamuzi, Bunge na Baraza la Wawakilishi, hiyo ni kero au nimebakwa kidemokrasia?
Ninapoona Mtanganyika hawezi kununua kiwanja kirahisi Zanzibar, kujenga, kuendesha biashara, hiyo ni kero au ubaguzi dhalimu?
Ninapoona Zanzibar inaandika Katiba inayokinzana na Katiba ya Muungano na kutangaza unilaterally kufuta kitu fulani katika orodha ya mambo ya Muungano, hiyo ni kero au jinai ya dharau?
Ndio maana wengine tunasema to hell with the Muungano!
Ahsante sana Taso kwa uchambuzi wako.
Hakuna ubishi kwamba Muungano ni ndoa ya kulazimisha. Ni kiloba cha misumali. Labda tujiulize kitu kingine...Nani analazimisha kuendelea kuwemo katika hii ndoa batili na kwa maslahi gani?