Vunjeni Muungano lkn mimi nitabaki Mtanzania

Najua wengi wenu mtahisi au mtaniona kama mropokaji lkn kamwe damu ya kitanzania na kamwe haitakuwa ya tanganyika wala ya kizanzibari. kwangu hupatwa na mfadhaiko nikimsikia mtu anajitambulisha yy ni mzanzibari au yy ni mtanganyika. uchezeeni muungano leo lkn kesho mutajuta. tunachotakiwa ni kuurekebisha mfumo wa muungano wa si kutengana haswa ktk wakati huu ambao tuhitaji kuujenga uchumi wetu. lkn mkiamua kamwe sitokuwa mtanganyika wala mzanzibari.

Mwanaone ukisema wewe mtanzania maana yake ni kuwa wewe ni zao la muungano wa jamhuri za Tanganyika na Zanzibar. Muugano ukivunjika hakutakuwa na watu watakaoitwa watanzania. Kutakuwa na Watanganyika na Wazanzibar. Wewe itabidi uchague tu kati ya hayo majina mawili.
 
Nikujibu ndugu,
Hakuna mtanzania yeyote anapenda kuona muungano uvunjike lakini muundo wa muungano uliopo hauvumiliki kwa watanganyika na wazanzibar. Linalotakiwa ni kuwauliza watanzania ni aina gani ya muungano wanapenda au wanapendelea. Jibu la wengi ni kuwa na serikali tatu ingawa mwalimu Nyerere alitahadhalisha gharama ya kuendesha serikali tatu hatuwezi na mzigo mkubwa utaiangukia Tanganyika, kuwa na serikali moja kamwe visiwani hawatokubali. Kama itatokea tusielewane ni heri tuachane salama kila upande uwe na serikali yake ili tujenge nchi zetu. Tanganyika waijenge tanganyika yao na wazanzibari waijenge zanzibar yao. Tutashirikiana kiuchumi, kijamii na kisiasa. Iwapo hili likitokea, basi utanzania umeisha na hakutokuwa na taifa la Tanzania. Sasa basi, kama hutakiwi kuwa mtanganyika au mzanzibari basi jiandae kuwa raia wa nchi nyingine tofauti na hizo mbili tajwa hapo juu. Sijui utasafiria passport gani, utakuwa na kitambulisho gani, nadhani unayasema haya kwa kuwa hayajatokea, ikitokea huna pa kwenda ndugu yangu. Tusingependa kuona hayo yote yakitokea kwa kuwa na mimi mwenyewe naupenda muungano wetu. Serikali 2 ni mzigo kwa raia wote, tujadili la serikali 3 au moja.

katika wachangiaji wote hadi kaka nakupa hongera hujakurupuka kutoa maoni. umetoa maoni ambayo kwa namna moja ama nyingine naona ni sahihi.
kwa wale wanaosema kama muuongano una faida basi dunia nzima ingeungana yaani kwa ufupi wanaona hakuna sababu za muungano. nasema wanajidanganya muungano unafaida kwa kila nchi ulimwenguni. na kama hawajui MAREKANI ambalo ni taifa kubwa duniani ni muungano states ambazo ni zaidi ya 50. kwa hiyo marekani isingekuwa taifa lenye power duniani kama isingeungana. simaani kama na kuungana kwetu na sisi kuna siku kutatufikisha hapo ilipo fika mareka kamwe hilo halitatokea. cha muhimu ni kuuboresha muungano wetu ili tufikie na sisi hatua fulani za kiuchumi. MUNGU TUDUMISHIE MUUNGANO WETU. NARUDIA TENA KWA WALE WASIOTAKA MUUNGANO WANITAJIE HASARA WANAZOZIPATA KUTOKANA NA HUU MUUNGANO. NA WASISEME TU MUUNGANO UVUNJWE BILA KUTUAMBIA AU KUTUOA USHAHIDI NI HASARA GANI WANAZIPATA KUTOKANA NA KUWEPO KWA HUU MUUNGANO.
 
Hakuna mtanzania yeyote anapenda kuona muungano uvunjike
Jiongelee mwenyewe, we mgeni hapa? Ulifanya poling ukapata 100% ya Watanzania wanataka Muungano?

Jamani mbona mnatulazimisha? Sio wote tunataka Muungano!
Tutofautiane kimawazo, lakini tusiburuzane, jiongelee mwenyewe.
 
Sioni na bado sijaona faida ya MUUNGANO.. Ila naona kama usivunjwe vile. Hebu tuone mataifa makubwa kama German baada ya kuungana wanafaidika vp?
 
Hatuwezi kujuta, muungano sio lazima, viinchi vingapi vidogo kama karanga vina nguvu kuliko Tanzania na li muungano lake?

Swaziland, Lesotho, Botswana, wameungana na nani?

Hatujaenda Ulaya, viinchi kama Belgium, Luxembourg, Uswizi wameungana na nani?

Kill the Muungano!

Hapo hujaongelea visiwa kama Mauritius, Singapore, Taiwan etc.
 
Najua wengi wenu mtahisi au mtaniona kama mropokaji lkn kamwe damu ya kitanzania na kamwe haitakuwa ya tanganyika wala ya kizanzibari. kwangu hupatwa na mfadhaiko nikimsikia mtu anajitambulisha yy ni mzanzibari au yy ni mtanganyika. uchezeeni muungano leo lkn kesho mutajuta. tunachotakiwa ni kuurekebisha mfumo wa muungano wa si kutengana haswa ktk wakati huu ambao tuhitaji kuujenga uchumi wetu. lkn mkiamua kamwe sitokuwa mtanganyika wala mzanzibari.

nakuunga mkono mkuu,

hata mimi nitabaki mtanzania daima.

Tanganyika siijui,
sikuzaliwa Tanganyika,
wakoloni ndio wanaoijua Tanganyika,
hii Tanganyika ilikuwa shamba la bibi kwa wakoloni,
ha wao wanjua kuwa hawatathubutu kuigeuza Tanzania koloni lao, haiwezekani
Tanzania ni huru na haijawahi kutawaliwa
Tanganyika na Zanzibar yote ni makoloni na hayajawahi kuwa huru
muungano ndio uliokamilisha uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Tanzania ni jina la kizalendo
tena linaakisi uhuru na azma ya kujitawala
tanganyika inaakisi utumwa, ukoloni, na unyonyaji

siipendi Tanganyika,
siipendi Zanzibar
napenda Tanzania
daima nitaililia Tanzania
Mungu ibariki Tanzania!!!
 
Hivi tunaunganisha mipaka, serikali utaifa au watu?

Mpaka usawa huu wengi hawaelewi tumeunganshwa kitu gani au tunataka kutenganisha kitu gani
 
Kwa uhalisia mimi naona tumeunganisha vitu na si watu. Watu wanapokuwa kitu kimoja vitu huwa sio issue lakini vinapounganisha vitu watu wakabaki pembeni ndiyo haya tunayoyaona sasa yanatokea.
 
nionavyo mimi,
serikali moja tosha,
kama haiwezekani tunaweza talakiana,
tumewabeba hawabebeki,
ndio theory ya mahusiano hiyo, hata ikiwa kati ya nchi,
ipo siku, sio mbali saana kivile.
 
Najua wengi wenu mtahisi au mtaniona kama mropokaji lkn kamwe damu ya kitanzania na kamwe haitakuwa ya tanganyika wala ya kizanzibari. kwangu hupatwa na mfadhaiko nikimsikia mtu anajitambulisha yy ni mzanzibari au yy ni mtanganyika. uchezeeni muungano leo lkn kesho mutajuta. tunachotakiwa ni kuurekebisha mfumo wa muungano wa si kutengana haswa ktk wakati huu ambao tuhitaji kuujenga uchumi wetu. lkn mkiamua kamwe sitokuwa mtanganyika wala mzanzibari.

wewe mropokaji.
 
nakuunga mkono mkuu,

hata mimi nitabaki mtanzania daima.

Tanganyika siijui,
sikuzaliwa Tanganyika,
wakoloni ndio wanaoijua Tanganyika,
hii Tanganyika ilikuwa shamba la bibi kwa wakoloni,
ha wao wanjua kuwa hawatathubutu kuigeuza Tanzania koloni lao, haiwezekani
Tanzania ni huru na haijawahi kutawaliwa
Tanganyika na Zanzibar yote ni makoloni na hayajawahi kuwa huru
muungano ndio uliokamilisha uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Tanzania ni jina la kizalendo
tena linaakisi uhuru na azma ya kujitawala
tanganyika inaakisi utumwa, ukoloni, na unyonyaji

siipendi Tanganyika,
siipendi Zanzibar
napenda Tanzania
daima nitaililia Tanzania
Mungu ibariki Tanzania!!!

Ndugu yangu hatuwezi kuwa na mfumo ule ule wa maisha milele. Usipoamini katika mabadiliko hutakaa ufanikiwe.

Watanzania wengi hatukuamini mfumo wa vyama vingi tukidhani kuwa tutapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini baada ya kulazimishwa kuyakubali mabadiliko leo tunafurahia. Kama tungeachwa na mfumo wa chama kimoja unadhani tungekuwa hivi tulivyo leo?

Tanganyika ilishakuwapo bila shida hata baada ya uhuru, Zanzibar imeendelea kuwepo kama zanzibar bila tatizo.

Lazima tukubali mabadiliko. kama vile ambavyo binadamu tunabadilika.
 
daima tanzania idumu mungu tupe hekima tuache fikra potufu za kuuvunja muungano wetu. MUNGU ILINDE TANZANIA NA KAMWE USIWAPE NAFASI WANAOTAKA KUUVUNJA MUUNGANO.
 
Najisikia Fahari Kuitwa Mtanzania! Naomba Mungu aniepushe hapa duniani nisije ishi kwenye Nchi itakayo itwa Tanganika!
 
Mnaotaka muungano uvunjwe mbona hamsemi hizo hasara mnazozipta kwa uwepo wa muungano. Tunataka ushahidi uletwe jamvini.
 
kinachotukwaza kwenye huu muungano ni kukosekana kwa umahiri wa uongozi! hatuna kiongozi mahiri, ila kitu shaghalabaghala!!

enzi njelu kasaka anahamasisha uundwaji wa serikali ya Tanganyika akidakia hoja za mch. mtikila, mwalimu nyerere aliinuka kutoa mwongozo wake kuwa, serikali ya tanganyika inaweza kuundwa wakati wwowte kama sera ya chama tawala itataka iundwe laki ikiwa tu nia ya kuundwa kwa serikali tatu kama muundo rasmi wa muungano itwekwa bayana kwenye ilani ya uchaguzi na inadiwe na mwisho wa siku chma chenye ilani hiyo kichaguliwe kuunda serikali. kwa hiyo kudai serikali tatu sio dhambi lakini lazima tuanzie na sera kisha tutengeneze ilani na mwisho baada ya uchaguzi tuje na marekebisho ya katiba, hiyo ndiyo process!

sasa nani yuko kutuongoza tuifuate?
na wa kutuelimisha je, yuko wapi?
wa kuielezea tanzania yetu nzuri je, yuko wapi?
wa kutetea huru wetu na mapinduzi yetu je, yuko wapi?
wa kukataa kurudi kifikra kwenye usultani na utumwa je, yuko wapi?
wa kutetea umoja na mshikamano wa kindugu je, yuko wapi?
wa kupigia kelele umoja wa afrika nzima unaoanza na muungano wa Tanzania je, yuko wapi?
wa kuendeleza njozi za baba zetu mashujaa wa ukombozi wa afrika za umoja wa nchi huru za afrika je, yuko wapi?
wa kuwakemea mabeberu kuwa afrika haitakuja kutawaliwa tena na mabwanyenye je, yuko wapi?
wa kufuta nadharia za kitumwa na ukoloni mamboleo vichwani mwetu je, yuko wapi?
wa kuongoza watanzania kuzishinda mbinu za adui za "divide and rule' je, yuko wapi?

nani mtetezi wa Tanzania?
nani mtetezi wa Africa?
nani mtetezi wa uhuru wetu?
 
Mnaotaka muungano uvunjwe mbona hamsemi hizo hasara mnazozipta kwa uwepo wa muungano. Tunataka ushahidi uletwe jamvini.

Kitu chochote kisicho faida basi ni hasara. Kama watu hawaoni faida ya Muungano basi huo Muungano ni hasara by default

Labda mnaojua faida za Muungano ziwekeni hapa tuzichambue.

Mtuambie bila Muungano tulioporwa utaifa wa tanganyika tunapoteza nini. Na kwa huu muungano tuliokuwa watanganyika tunapata nini?
 
Ndugu yangu hatuwezi kuwa na mfumo ule ule wa maisha milele. Usipoamini katika mabadiliko hutakaa ufanikiwe.

Watanzania wengi hatukuamini mfumo wa vyama vingi tukidhani kuwa tutapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini baada ya kulazimishwa kuyakubali mabadiliko leo tunafurahia. Kama tungeachwa na mfumo wa chama kimoja unadhani tungekuwa hivi tulivyo leo?

Tanganyika ilishakuwapo bila shida hata baada ya uhuru, Zanzibar imeendelea kuwepo kama zanzibar bila tatizo.

Lazima tukubali mabadiliko. kama vile ambavyo binadamu tunabadilika.

mabadiliko ni ya kwenda mbele au nyuma, kwa nini tubadilike kwa kuyarudia matapishi yanayoitwa Tanganyika? kwa nini tusibadilike kwa kwenda mbele mfano kwenye jumuiya ya afrika mashariki, SADC, umoja wa afrika? au hata kuimarisha ushiriki wetu katika UN? kwa nini tubadilike kutoka wakubwa (Tanzania) kwenda kuwa watoto wadogo (Tanganyika)? wakati trend ya asili ni kutoka utoto kwenda ukubwa? kwa nini tubadilike toka nchi huru (Tanzania) twende nchi koloni na shamba la bibi la wajerumani, waingereza, na waarabu wafanya biashara za utumwa?

unaipendea nini tanganyika?
utumwa unakufurahisha nini ndugu yangu?
ukoloni una passion gani?
unyonyaji unakufaidia kitu gani?
 
Kitu chochote kisicho faida basi ni hasara. Kama watu hawaoni faida ya Muungano basi huo Muungano ni hasara by default

Labda mnaojua faida za Muungano ziwekeni hapa tuzichambue.

Mtuambie bila Muungano tulioporwa utaifa wa tanganyika tunapoteza nini. Na kwa huu muungano tuliokuwa watanganyika tunapata nini?

utaifa ulioporwa ni utaifa gani?
baada ya kuporwa huo utaifa wako ulioasisiwa na wakoloni walioitawala Tanganyika, unajutia uhuru wako uliokukirimu utaifa mpya?
wewe huna utaifa?
unayo passport?
umeishawahi kusafiri nje na kuchanganyikana na watu wa mataifa mengine ukakosa kutambuliwa?
utaifa uliopachikwa na wakoloni wako ndio bora kuliko utaifa tunaouchukua vifuani mwetu na ulioasisiswa na watanzania wenzako wanamapinduzi?
je, mwalimu nyerere, karume na wanamapinduzi wengine walaaniwe kwa kuwa tu waliasisi utaifa mpya wenye heshima kwa mwafrika na usioakisi ubeberu wa magharibi uliozaa ukoloni wa mataifa ya kiafrika?
kwako utaifa wa kutuniukiwa na mkoloni ni bora kuliko utaifa wa kizalendo?
 
wakati wa shida walipenda muungano, sasa wamevimbiwa hewa inawatoka ovyo wanataka nafasi.... labda hewa inanuka sana yakhe!!!
wapende wasipende wataendelea kuitegemea Tanganyika kwa kila kitu, jeuri yao mafirauni wa kiarabu? kwani Somalia, yemen inayopakana na Saudia au Uganda, wote hawa wako kwenye jumuiya ya nchi za kiislam na kiarab ligi, je wana nini kuliko sisi? sema jawako sawa kimentali hao jamaa zetu wazenji, sema kwa mademu si haba alhamdulillahi, japo mademu wenye mara wanagoma kutoa mpaka uzunguuke mlango wa uwani...

Wewe unayejiita Pharaoh hata adabu huna yakhe! Wakati wa shida gani hebu kasome historia halafu ndiyo ujifunze adabu ya kujibu masuala nyeti kama haya hapa kwenye forum.

Nani amevimbiwa? Wewe unajua Zanzibar ilikuwa na hali gani ya kiuchumi wakati inaungana na Tanganyika ukilinganisha na sasa? Unajua ilikuwa na kiwango gani cha elimu ukilinganisha na Tanganyika?

Kasome historia ujitambue na ujue mchango wa Zanzibar pale Nyerere aliposema 'haturudi nyuma tusijegeuka jiwe' halafu Tanganyika ikawekewa vikwazo vya kila aina na IMF na nchi za magharibu. Huo ni wakati Mtei alipokuwa Waziri wa Fedha na si ajabu ulikuwa hujazaliwa ndiyo maana unasema utumbo usiokuwa na mpango.
 
naombeni wale wote ambao wanasema muungano uvunjike wataje hasara mbili 2. mimi nimeshataja faida ninazoziona
1: elimu - wazanzibari wanfaidaka ktk elimu ya juu wakija kusoma tanganyika wankopeshwa sawa na wanalip[a ada sawa kama watanganyika na watanganyika wakienda zanzibar hivyohivyo wanapata fursa hiyo.
2; kuna free trade btn zanzibar na tanganyika. mzanzibar hapati aina yyte ya kikwazo akitaka kufanya biashara tanganyika kwa sababu ya uzanzibar wake na mtanganyika hivyohivyo hapati vikwazo akitaka kufanya biashara zanzibar.

sasa nyinyi munaouona hauna faida tajeni hasara mbili mnazozipta kwa ajili ya huu muungano wetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU UBARIKI MUUNGANO WETU.
Hivii, naweza kuruhusiwa kugombea uwakilishi au ubunge huko Zenji bila kikwazo?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom