Vote for Mount Kilimanjaro to become among new 7 wonders

Status
Not open for further replies.
niupigie kura kwa faida ya nani.kama rasilimali za taifa zingekuwa na faida kwa watanzania ningepiga.siwezi kuendelea kuneemesha mafisadi
 
halafu ukishinda hela zitanunulia flana na kofia za kijani. sipigi kura ng'ooo.
 
It is like girls on a beauty pageant awaiting for the judges to tell them that they are beautiful. Mt. Kilimanjaro is already a wonder. No vote needed.
 
Inasikitisha na kuhudhunisha sana,hili zoezi la kuupigia kura mlima wetu kumbe lilianza kitambo na lilishika kasi miaka 2007 na hadi 2009 ndio likawa kwa kasi zaidi hasa wageni ndio waliokuwa wakiupigia kura huko nchi za nje.Iweje wananchi wa Tanznia tupewe taarifa kwa kuchelewa hivi,hasa watu wa vijijini.Wapi watangaza vivutio vyetu waliopewa dhamana? Anyway,tujitahidi kupiga kura,Ijumaa si mbali tena mwisho ni saa nne usiku (Majira ya Africa Mashariki).
 
Hv mlima kilimanjar uko ktk mkoa wa kigoma,lakin wasukuma hawautaki.Swl mt.kilimanjaro uko Tanzania au songea,maana mke wa ***** wa Tz anausifia kwl.
 
tunapigia kura kwa kigezo kipi iingie kwenye maajabu 7 ya dunia???????

shimo lililobaki??????????

urefu wa mlima?????????

tulikua wapi au shindano hili ndo la kwanza??????????
 
jamani marafiki hebu tuweni wazalendo na tuupigie mlima kilimanjaro ili uingie kwenye maajabu saba ya dunia kwa kutumia namba ( 15771 ) ni bure kwa mitandao ya airtel na vodacom hivyo jamani tuupigi kura mlima wetu mpaka simu ziishe charg.

sipigi kura, siwapi washenz chakula
 
Jamani marafiki hebu tuweni wazalendo na tuupigie mlima kilimanjaro ili uingie kwenye maajabu saba ya dunia kwa kutumia namba ( 15771 ) ni bure kwa mitandao ya Airtel na Vodacom hivyo jamani tuupigi kura mlima wetu mpaka simu ziishe charg.

haaa, siku hizi ni bure? ohhh maajabu hayaaaaa!! mie nshapiga kitambo kwa mtandao, ncikia hii namba ni dili la kula ela. kama ni bure basi wametoa ofa!!!
 
Hata mkinijia kwa marungu na mapanga kamwe sintopiga kura yangu kwa manufaa ya wachache. Tuache tutakuja kupigia kura pindi nchi hii itakapochukuliwa na wazalendo
 
upuuzi mtupu!badala kuhamasisha utalii wa ndani ukue tunakomalia maajabu feki ya dunia.
 
Nyie pigeni tu mimi mmnh, sipigi ng'o! Kakwambia nani maajabu yanaamuliwa kwa kura. Sawa, ukishakuwa wa ajabu, what next? Sijajua tu nini kingine kinashindana manake ningepigia hicho na sio mlima wetu. Wakati ndege ya Qatar inachukua twiga wetu hapa tulipiga kura? Au hayo siyo maajabu kwa ndege ya jeshi la nchi nyingine kutua hapa na kuondoka na twiga bila mamlaka kuwa na taarifa?
 
Kura ya nini, niambie kwanza Maajabu mengine yamesaidia nini kuinua uchumi wa nchi. Matokeo yake mmetengeneza maajabu yenu 7 yaani 1. Meremeta, 2. Deep Green, 3. EPA, 4. Kagoda, 5. Import Support Commodity, 6. Richmond, 7.Dowans.

Huu ni upuuzi tu, haina haja ya kuwa na ajabu la asili wakati Mungu ametupatia maajabu mengi tu, yaani Ardhi, Watu, Amani, Mito, Maziwa, Bahari, Mabonde, Wanyama, Milima, Dhahabu, Almasi, Shaba, Uranium, Gas, Mlima kilimanjaro na mengine mengi.

Sasa mnatafuta ajabu gani hilo la kupigia kura wakati ajabu lenyewe lipo tu hata kama watapiga kura au hawapigi.

Sipigi kura hata kama ni bure, kwanza sipendi vitu vya bure kama Mafisadi.
 
Ingawaje sio ajabu kuwa na mlima wa kilimanjaro ulo na theluji kileleni karibu na ikweta. Lakini kuufanya kuwa kivutio zaidi ni bora ikiwa mapato kweli yatawafikia watanzania na sio kwenye mifuko ya mafisadi. Tanzania mafisadi ni wengi na wapo kidedea kuufanya huo mlima kuwa ni mradi wao. Mimi nimeshupigia kura.
"Mungu ibariki Tanzania na watu wake"
 
Tuwe wazalendo wa Ukweli

Tuupigie kura Mlima Kilimanjaro ili uingie maajabu SABA (7 ) mapya ya Dunia

Ili kuupigia tuma Neno " KILI " kwenda 15771
 
Dili la sms hizo.
kama sms 1 ita cost sh.150 ukatoa sh. 58 unabakiwa na 92 ukizidisha mara watu milioni 3 kwa siku mara siku 20 huoni ni utajiri wa kutupwa?
 
Tuwe wazalendo wa Ukweli

Tuupigie kura Mlima Kilimanjaro ili uingie maajabu SABA (7 ) mapya ya Dunia

Ili kuupigia tuma Neno " KILI " kwenda 15771

Naomba nijue kwanza hizo Tsh.300/= nazo katwa ni nani atakula?
Inaonyesha zoezi hili lipo kisanii na kutajirisha watu flani flani kama sio makampuni ya simu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom