Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, mimi Mzee wa "the voices from within" na Maswali Fikirishi.

Angalizo la Mambo ya Sauti.
Kuna mambo ni yetu, na mambo mengine sii yetu, mambo ambayo ni yetu, unaweza kuuliza, lakini kwa mambo ambayo sii yetu, huwezi kuuliza, miongoni mwa mambo ambayo sii yetu ni pamoja na haya mambo ya mtu kusikia sauti, ni unasikia tuu, hakuna sababu yoyote, wala ushahidi wowote ni unajikuta umeambiwa tuu.

Hapa nimesikia sauti ambayo mimi huwa naiita ""Voices From Within", hii voices from within, ni sauti ambayo unaisikia kutokea ndani yako, inakuambia kitu fulani, huwezi kuiuliza chochote ila unaweza kujiuliza kama hicho ulichoambiwa its makes sense, na kina logic?, then unajiuliza nikiseme au nisiseme, unajifanyia a self objectivity assessment tes na self censorship kwa kujiuliza nikisema kina faida, kitasaidia, au ninyamaze just to keep to myself. Unajifanyia self censorship, kisha unafikia maamuzi kusema ili kuwajulisha na wengine lakini sio lazima useme kila ulichosikia.

Hizi sauti ziko za aina nyingi, wengine huoteshwa kama ndoto, wengine huonyeshwa kama visions, na wengine, haswa ma deep thinkers, likitokea jambo, ukalifikiria sana, wakati umetulia, usually usiku mkubwa, kwenye ukimya na utulivu, ndipo unaisikia hiyo sauti au vision, wabunifu na wavumbuzi wengi hivi ndivyo wanavyovumbua!. Archimedes alipovumbua law ya floatation, alikuwa bafuni akioga kwenye bath tub, alitoka hivyo hivyo alivyo from the bathroom hadi mtaani huku akipiga kelele "eureka!, eureka!, ... yaani nimegundua, nimegundua, wala hakukumbuka tena kama alitoka hivyo hivyo bafuni kama alivyozaliwa!, wastaarabu wakamdaka kwa kunshika kwa nguvu kumsitiri wakijua ni kichaa!. Hata Sir Isaack Newton, mvumbuzi wa Newton's laws of motion, kuna siku alikuwa anapima yai linaanza kuchemka dakika ya ngapi, akachukua saa akaiweka kwenye sufuria, na kuichemsha huku amelishika yai mkononi akipima muda!, alikaa hivyo muda mrefu hadi mkewe akamuuliza ndipo akashtuka.

Hiki nilichosikia, unaweza usiamini!., unaweza kuniona Pasco ni kichaa fulani, haijalisi ni sauti ya nani, just take it or leave it, ikitokea ikiwa kweli, wewe mwana jf, unakuwa na a jf advante "be the firts to know" kumbe aliyetoa a go ahead kwa kina Mdee na kundi lake, ni kigogo wa Chadema!. Mimi niliuliza humu mkaniona kama ni kichaa fulani.

Sasa sauti imeniambia the one behind hii saga yote ya kina Mdee, ni Kigogo mmoja mkubwa tuu wa Chadema!. Sauti hiyo imeniambia Kigogo huyo alikuwepo ukumbini, kwenye vikao vyote viwili vilivyowatimua kina Mdee!. Jee Kigogo huyu ni nani?, andamana nami....

Nilikuwa nachangia mada hii
..walifukuzwa na kamati kuu.
Kamati Kuu ni mamlaka ya nidhamu ya wabunge but not Halima. Kesi ya wabunge iliendeshwa kikangaroo hivyo hukumu ile ya CC ni batili.
..wakakata rufaa ktk baraza kuu.
Baraza Kuu ndio mamlaka ya rufaa ya wabunge. Baraza Kuu lilipaswa kwanza kujiridhisha kama CC ilitenda haki, halikufanya, likaubariki ukangaroo wa CC!. Hapa sasa ndio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee. Hakuna kesi yoyote ya Halima iliyowasilishwa Baraza Kuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka kufukuza Halima wakati hata Baraza Kuu halina mamlaka hiyo?!. Kesi ya Halima ingetoka Baraza Kuu na kuingia Mkutano Mkuu ndio pekee wenye mamlaka hiyo. Kilichofamyika ni uhuni, ambao mimi nimeuita ni ukangaroo.
..baraza kuu likakazia hukumu ya kamati kuu.
Kitendo cha kukazia hukumu batili nao ni ukangaroo!.
..kama unayosema ni kweli kwanini Halima na wenzake walikata rufaa kwa baraza kuu?
Rufaa zote lazima zifuate kikao kinachofuatia, Halima alikata rufaa Baraza kwasababu CC sio mamlaka yake ya nidhamu na haina uwezo wa kumfukuza!.
..lakini kwanini tuzunguke kote huko? Kwanini Halima na wenzake hawaelezi kikao kilichowateua, wala kiongozi aliyepeleka majina yao kwa tume ya uchaguzi?

Cc Erythrocyte
Hawaeezi chochote kwasababu hakuna kikao chochote kilichowateua, kule NEC hawahitaji taarifa za kikao, wanahitaji barua ya uteuzi na fomu zilizosainiwa. Barua ilikuwepo na fomu zilikuwepo na hapa ndipo nikaisikia sauti from within kuwa mtu aliyewapa go ahead kina Mdee ni Kigogo mmoja wa Chadema, ni mjumbe wa CC na siku ya kikao cha Kamati Kuu Chadema, kilichokaa kama a Kangaroo court na kuwatimua, alikuwepo!. Siku ya Kikao cha Baraza Kuu, kubariki ule Ukangaroo wa Kamati Kuu Chadema alikuwepo ukumbini!. Sauti Imeishia hapo.

Jee Kigogo Huyu ni Nani?.

Kule nyuma nimawahi kutoa tuhuma kuwa Chadema kuna kirusi, leo nilitaka ku update huu uzi CHADEMA Kuna Kirusi! Je, Unajua kirusi hiki ni Nani?! Na The Motive Behind? kwa kirusi hiki kipya, nikakuta umefungwa!, kumbe I was wrong, sio kuwa Chadema kuna "ki"- rusi!, Chadema kuna "vi" rusi! maana ni more than one!. Jee unaweza kuamini aliyasaini barua za kina Halima ni mnene mmoja wa Chadema ambaye ni mjumbe wa CC na alikuwepo ukumbini kwenye kikao cha Kamati Kuu na Kikao cha Baraza Kuu?!.

Can you mu imagine Kigogo huyu ni nani?. Anza kutafakari, mimi nitakusaidia

Nilitamani kumalizia nikupe kitu kamili lakini sisi sekta binafsii maisha yetu ni ya kukimbizana, kufukuzia tenda, tenda nyingi deadlines zake ni Monday, hivyo kuna tenda nakimbizana nayo, deadline yake ni saa 4:00 asubuhi hii

Nitarejea...
ila Matokea ya Kikao cha Baraza Kuu Chadema kuwatimua waanawake wa shoka, mashujaa 19 wa Chadema waliokipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, bado yanatawala mijadala mbalimbali humu jf.

Anza kwa kutembelea haya mabandiko haya anzia
hapa Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?
na A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?
na Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?
na Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
na CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
na Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
na Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu
na Kufanya Kosa Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa, CHADEMA is Almost Dead, Due to deadly mistakes!, This Your Only Survival, Do or Die!, Msirudie Kosa!.
na Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!
na Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

na JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

na For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?

Paskali
 
Kaka Pascal Mayalla, kwanini jambo hili likunyanyase na kukunyima usingizi kiasi hiki? Uliwahi kuchambua, kama ufanyavyo hapa, alipofukuzwa uanachama wa CCM Mama Sophia Simba?

Halafu, unapotaka kueleweka pale unapozungumzia sheria ni vyema kuweka vifungu vya sheria husika. Viko wapi vifungu vya Katiba ya CHADEMA unavyojengea hoja yako? Hebu waache CHADEMA wamalizane wao kwa wao, pilipili usioila yakwashia nini kaka? Ha ha ha ha ha
 
Paskali kulingana na taaluma Yako umefanya vizuri, Kwa hili swala inaonekana una taarifa za uhakika tena za kina. Ninachotaka ufahamu sio kwamba wanachama wote na wapenzi wote wa chadema ni ma mbumbumbu na awafahamu kwamba Halima na wenzake hawakujipeleka bungeni, Wanafahamu hakuna kinacho fanywa ndani ya chadema bila mkono wa DJ.

DJ ndiye mratibu wa Kila jambo ndani ya Chama uku chawa wake Lema akiwa mshauri mkuu.Sauti ya Lema ndio sauti ya DJ.Ni swala la muda tu baadhi ya watu wataziona rangi halisi za DJ.
 
Voice from within, ujinga mtupu.

Baadhi utapeli wa namna hiyo, unawapa maisha ya kuokoteza, utakuta wamebandika mabango, "mganga maarufu toka Sumbawanga", lakini ni wajanja, mara nyingi utakuta mabango hayo kwenye maeneo wanayoamini kuwa wajinga ni weng.


"Hakuna kesi yoyote ya Halima iliyowasilishwa Baraza Kuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka kufukuza Halima wakati hata Baraza Kuu halina mamlaka hiyo?!. Kesi ya Halima ingetoka Baraza Kuu na kuingia Mkutano Mkuu ndio pekee wenye mamlaka hiyo. Kilichofamyika ni uhuni, ambao mimi nimeuita ni ukangaroo."

Eti mamlaka ya kuwafukuza akina Halima ni mkutano mkuu, na siyo Baraza Kuu! Unaelewa ulichoandika. Hivi, tangu lini CHADEMA wana Mkutano Mkuu? Au unazungumzia CHADEMA, huku fikra zako zipo kwenye vikao vya CCM?

Wewe Mayala, kwa kiwango kikubwa, ndiye kangaroo, unayetuletea hoja za kikangaroo.
 
Me ninachojua Pasco ameamua kuwa awe vile anavyojiskia,maana asikii mtu anatukanwa kila akipost,anakosolewa kwa mapungufu ya ujuaji wake juu ya chadema lakini asikiagi huyu mzee.

Niliamua kuacha Kama alivyo napitia maandiko yake juu juu Kisha nasoma reply za wakuu jinsi wanavyo mkomesha.
 
Kaka Pascal Mayalla, kwanini jambo hili likunyanyase na kukunyima usingizi kiasi hiki? Uliwahi kuchambua, kama ufanyavyo hapa, alipofukuzwa uanachama wa CCM Mama Sophia Simba? Halafu, unapotaka kueleweka pale unapozungumzia sheria ni vyema kuweka vifungu vya sheria husika. Viko wapi vifungu vya Katiba ya CHADEMA unavyojengea hoja yako? Hebu waache CHADEMA wamalizane wao kwa wao, pilipili usioila yakwashia nini kaka? Ha ha ha ha ha
Amepata pa kupandia, ukitaka kupata umaarufu andika kuhusu Mbowe au CHADEMA. Nje ya mada, unasalimiwa.
 
Back
Top Bottom