Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania naombeni mniambie hiki ni kitu gani na kwa nini napata hizi msg toka kwenu na ninawezaje kujitoa kwenye huu upuuzi wenu
Screenshot_20220607-102420_Messages.jpg

Kwa kweli sifurahishwi kabisa na hizi msg zenu mnazonitumia bila mimi kuomba. Naombeni muache huu ujinga
 
Vodacom Tanzania mmekuwa kampuni ya ajabu kweli.Naona mnachonga mzinga wa asali ya Rais Samia,nyambafu!!!MMEKUWA WEZI.

Ninaongea na mtoa huduma ananijibu utumbo.Bongo bahati mbaya,nihame nchi tu.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Wajinga ninyi kwa mwezi mzima mmekuwa mkinitumia message za TUSUAMAPENE!!
Mnanipotezea muda wangu na michezo ya kijinga.

Hii imenikera maana katika kufuta messge zenu nimejikut nafuta messge zote hata zile za maana.

VODACOM acheni mambo ya kijinga!
 
Leo nimejiunga kifurushi cha maongezi cha Tshs.2,000/=,kwa M-PESA,Kiasi kilichokuwemo kwenye akaunti ya M-PESA ilikuwa ni Tshs.17660.09/=,Kitu cha kushangaza salio likabaki 12,946/=.Na hawajasema pesa hiyo ya juu iliyokatwa ni kwaajili ya nini.

Na nikijaribu kuwasiliana na huduma kwa Wateja sipati ushirikiano,na hii si mara ya kwanza kuna siku nyingine badala ya kukata 2,000/= wao walikata 3,000/=.Vodacom mnatunyanyasa sana wateja wenu.
 
Kuna usumbufu mkubwa sana katika makato ya pesa za tusua mapesa kujilipa wenyewe toka katika yangu bila idhini kwa kipindi kirefu sana.Rejesheni pesa zangu!!
 
Leo nimejiunga kifurushi cha maongezi cha Tshs.2,000/=,kwa M-PESA,Kiasi kilichokuwemo kwenye akaunti ya M-PESA ilikuwa ni Tshs.17660.09/=,Kitu cha kushangaza salio likabaki 12,946/=.Na hawajasema pesa hiyo ya juu iliyokatwa ni kwaajili ya nini.Na nikijaribu kuwasiliana na huduma kwa Wateja sipati ushirikiano,na hii si mara ya kwanza kuna siku nyingine badala ya kukata 2,000/= wao walikata 3,000/=.Vodacom mnatunyanyasa sana wateja wenu.
Piga TCRA malalako utapata majibu chap kwa haraka
 
Coda jamani !Voda ni wafanya biasghara sio watoa huduma.Kila wanachofanya kinagharama za huu mno kulikoni mitandao yote.Ebu shusha/punguzeni gharama za matumizi kwa wateja mnatuumiza mno.
 
Vodacom ni mtandao nilikuwa ninapenda na nimeutumia sana Kwa huduma kama M_ pesa ,vifurushi mbali mbali na huduma mbali mbali. Kitu kilichonikera na kunichefua ni kile mnachoita Chongesha.

Tumezoea kupata packages nyingi kama vile gawio,unaambiwa umepata kiasi kadhaa kitumie kupata muda wa maongezi n.k. Sasa Songesha nayo imeingizwa Kwa mukthada kama huo kumbe ni mtego wa aina ya ukopeshaji wa kitapeli.

Unasema umepokea kiasi kadhaa kitumie kununulia vifurushi au kukamilisha muhamala. Mteja nikitumia ikuambiwa kama ni mkopo ,ninatumiwa meseji kuwa ninadaiwa kiasi hicho na riba.. Biashara ya mtindo huo ninaona ni kama utapeli wa aina Fulani.

Elimisheni wateja kabla wakuelewe kuliko kuonekana Vodacom Mtandao ulizokuwa na huduma Bora umegeuka Kanjanja.
 
Vodacom hamjambo.
Nawaulizeni Nina kiwango gani Cha Mpesa hamtoi jibu. App ya mpesa haifanyi kazi. Nini shida
 
Back
Top Bottom