Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nenda kwenye duka hizo za kupiga huwa wana limit za kurudisha walichofanya hapo ni kublock ukienda voda shop mara moja. Pole sana
 
Nenda kwenye duka hizo za kupiga huwa wana limit za kurudisha walichofanya hapo ni kublock ukienda voda shop mara moja. Pole sana

ipo haja gani sasa kutumia hii huduma kila kitu hakina tatizo, kesho naenda na fimbo ya ndugai kumbe watz bila mboko hawaendi
 
hii mitandao yote ni shida tu...labda hii mipya ya saiz ila voda na airtel na tigo ni kuna wizi sana, juzinilikuwa wakala wa tigopesa analalamika eti kuibiwa pesa na watu wa tigo..

Ndo maana hizi huduma ziko afrika tu kumbe za kishenzi hivi
 
nimejiunga bando wa wiki baada ya hapo natupa line, kwanza wanyonyaji haiwezekani nilipe elfu tano kutuma laki hata mastacard hawako hivyo bora nimpatie pesa konda wa zuberi nimpe na buku ya soda

Kutuma laki mbili kwa tiGO ni mia sita tu.
Hiyo lain ya voda itume kwenye Zuberi nitaipokea hapa Manyoni. Asante kwa ushirikiano
 
Nimetuma hela kwa mpesa ni wiki sasa pesa haijafika na hakuna msaada wowote kutoka Vodacom, kesho natupa sim kadi yao.

Voda wameanza ku decline. Mimi nina miezi kama 15 line iko on lakini siirecharge
 
Hasira hasara, voda wana wateja wengi bwana, kwa kutupa kwako SIM CARD yao wala hawatapata taarifa na wala hawatajua kama wamekupoteza. Wewe komaa nao tu wakurudishie pesa yako, mimi ilishatokea kama wewe haikuchukua muda wakarudisha. Usiwaachie, hilo ni jasho lako. Kama una maamuzi hasi na voda hakikisha unarudishiwa MTONYO wako kwanza ndio ufanye hayo maamuzi hasi. Makampuni yote simu ndugu yangu tabia zinafanana, hakuna kwa kukimbilia na wala sijakuona kwenye unafuu.
 
Mie huwa najiuliza mbona wazungu hawatumii simu na maisha yao yanaenda tu, tunapaswa kupitisha elimu ya umma juu ya kuachana na matumizi ya simu.
 
Wazungu wanatumia simu, lakini matumizi yao si kama yetu. Wao hutumia simu kwa matumizi ya maana sana si kama TZ tunazitumia simu hata kwa kupeana umbeya na kusalimiana wao sivyo hivyo na kupoteza muda kwa kuchati, Wao wana matumizi makubwa kwenye Komputa ukienda kwao kwenye coffee bar zao wako bize, wanakunywa kahawa huku wanachapa kazi kutumia Komputa zao.

Makampuni ya simu kwa wazungu si ya kibabaishaji kama huku kwetu!

Mie nadhani huku TZ serikali haiko serious kufuatilia utendaji wa haya makampuni! matokeo yake ni makampuni kutupandishia gharama kama yapendavyo na kila siku ufanisi wa makampuni haya kupungua. Mie nadhani haya matatizo mbalimbali ya makampuni ya simu ni changamoto kwa serikali kuzimaliza kama si kuzipunguza.
 
Voda kwa sasa mnanyang'anya hela za watu,Mimi hivi na mpango was kuhama mtandao,kiweka hela ili nijiunge kifurushi naambiwa sina Salio,nikiangalia Salio lipo baada ya muda Salio halipo na kifurushi hakuna nimevumilia hiyo hali nimechoka.Voda jilekebisheni huo wizi
 
Jilekebisheni,hivi hamuoni Wateja wanapungua Mbarali,sababu nikuchumua Salio bila utaratib,vifurushi kwisha hovyohovyo bila utaratib,ukiuliza kwa washauri majibu take hayaridhizishi kabisa
 
Walianza Tigo Nikaona Andiko Humu Watu Wakijinasibu Kutumiwa Pesa Bure Kutokana Na Wao Kutumia Huduma Ya Kifedha Itumiwayo Na Kampuni Hiyo, Juzi Alitumiwa Baba 40elf Mpesa Leo Nimetumiwa Mimi 78 Kutokana Na Kufanya Miamala Mingi, Nyinyi Mpesa Ni Watu Wazuri Mungu Awabariki.
 
Fanyeni mazungumzo na Benki ya NBC nao wajiorodheshe kwenye mpango wa MOBILE BENKING ili mteja wa mpesa aweze kubenk au kutoa pesa kwa kutumia simu yake
 
Vodacom sina hamu na nyie nimetoa hela kwenye mpesa kwenda kwenye account yangu bank cha kushangaza pesa bank hakuna wala mpesa nikiongea nao wananniambia subiri kidogo nazungushwa tuuuuu bila sababu za msingi
 
hali hiyo inakera sana.
 
Nyinyi Voda, Huduma Ya Kupiga Simu Haifanyi Kazi Nilipiga Saa 12 Mkaniambia Mafundi Wanashugulikia Ni Tatizo Limeripotiwa Na Wengi. Hadi Muda Huu!, Its Terible! Mnajua Tu Kula Vocha Zetu! Mbona Net Inafanyakazi! Mafundi Wanashugulika!? Ama Wanashugulika Na Mambo Yao, You Have To Push Them! As A Seniour Supervisor We Are The One Who Pay Ur Salaries!
 
Wakuu,

Nimeripoti tatizo la kutokupiga simu na SMS Vodacom Tanzania customer care, nikawaandikia kwenye thread yao humu JF, nimewafuata Facebook kwenye page yao yenye watu laki sita!

It seems they've got nobody concerning with social media all the time! Hii ni aibu kwa kampuni kubwa kama yenu! Na mnaweza kuwa mojawapo ya aliewataja pale Jangwani yule rais aliepita wa kusini..
 
Back
Top Bottom