Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Wadau naomba maelekezo kwa anaye fahamu jinsi ya mtu kumrushia mwenzie Vocha baada ya yeye kuijaza kwake na aweze kui forward kwangu..??

Labda kama kuna code za kutumia au mfumo wowote! Tafadhali.
 
Mtandao wenu haupatikani vizuri kata yote ya mabogini kata hii ipowilaya ya moshi vijiji na vijiji vyake vyote ambavyo ni chekereni maendeleo muungano mserekia nyulend muungano na mabogini na karibu na moshi mjin
 
Mnakera na mnakera saana. Hili tangazo lenu la U tube ( You) tube ati mtu anabembeleza mtoto wake kwa. Mb zangu mbona htujakubaliana kuniibia hivyo , Acheni acheni kabisaaa
 
Polen sana mnao lalamika,kiukweli,mm natumia lain yavoda kwa mda mrefu sana kwaupande wangu sjaona tatizo nanatumia huduma zote ikiwemo mpesa.nnacho waomba vodaCom wajaribu kuboresha huduma ya tusua mapene angalao wawe wanatoa zawadi ndogo ndogo haswa tunaonunua kete kwa diskaunt kwanjia ya mpesa angalao hamsini au laki, wengine tuna kete kibao.nahatukati tamaa
 
Kwaupande wangu sina mashaka na mtandao wa voda pamoja na washkaji ila boresheni huduma ya tusua mapene angalao muwe mnatoa zawadi ndogo ndogo kama mlivyofanya katika mgao wajanuari ili kututia moyo tunaonunua kete yakifurushi cha mwezi kwanjia yadiskauti,kwakua wanaonunua kifurushi cha mwezi ndio wenye nafasi kubwa ya kushinda hadi milioni100,000,000
 
Nadhani TCRA nayo haizingatii wadau tunavyoibiwa ,na Vodacom katika maeneo haya
1. Video yanu ya YOU TUBE inayomuonyesha mama aliyebeba mtoto anayelia na kutulizwa na video ya catoon . Kitendo hicho kinasababisha matumizi ya Mb kadhaa nilizonunua zitumike kuihudumia tangazo nisilolihitaji , yaani nanunua tangazo!!! Kwa manufaa ya nani hasa

2. Tangazo la moja bet , wapi na wapi kwa mimi mteja ambaye sijabet ,mbona mnasumbua Voda
3. Tusua mapene ,huu nao ni usanii mtupu ,sijui kwa nini hizo mamlaka zinakaa kimya kwa jambo hili , unakuta ati unazo kete 10,000 (elfu kumi) hadi zinaisha unaambiwa mteja. Leo umekosa zawadi , nunua nyingine .
kichekesho ingia kwenye website yao uone wanaoshinda na maeneo wanayotoka hutatashanga unayejua usanii wanaotumia. Jamani mbumbumbuu tunaelimika sasa muwe na habari eeeh
Acheni kabisa hii tabia
 
M-PESA (VODACOM TANZANIA)

Jamani, mimi binafsi siwaelewe VODA NA MPESA, hivi kwa nini ukikosea kutuma pesa au kufanya malipo inachukuwa muda mrefu sana kurudi kwenye akaunti, Yani nimeongea na Huduma kwa mteja ananiambia nisubili siku saba, kati ya siku zote nimekuwa discouraged sana kutumia VODACOM kwenye transactions za pesa..


MY.QNS Hivi hili tatizo la kuchelewa kufanya reversal nakumbana nalo mimi tu, au na wadau wengine, kwa sababu inaumiza sana,,,,,
 
Hii mitandao ni wababaishaji wanavamia huduma bila kuwa na uwezo wa kuhudumia mfn tumapesa kwenda mitandao mingine ukikosea pesa imepotea mjomba yaani kampuni na kampuni hawako na mahusiano mazuri
 
Back
Top Bottom