Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Dah Voda bwana ni mtandao wangu toka zamani naupenda, kasi yake hata umaarufu wake mkoani ninakotokea. ila nimejikuta sithamini kama mwanzo baada ya kukutana na tigo hapa mjini dar chanzo kikubwa mimi kudharau voda ni huduma mbovu za wa hudumu, uhaba wa ofisi zenye huduma zote japo mpaka sasa sijui ofisi hata moja ya vodacom yenye huduma zote, hali ambayo inanifanya nikidukuliwa pesa kwenye mpesa, au salio la kawaida sina sehemu ya kukimbilia, na nimeshapoteza hela nyingi sana.
kwa hiyo vodacom, ofisi zenye ukamilifu kivifaa na wahudumu kwa hapa mbagala dar hamnaa.
kwa hiyo mtanipata kwenye masuala madogomadogo ya muda tu mpaka nikirudi kijijini ndo nitakuwa mteja wenu.
 
Vodashops au maduka ya Voda ni mengi kila mahala hapa Dar inategemeana unakutana na muhudumu gani nenda Kariakoo, Mlimani City au Samora au Qualify Plaza
 
Vodacom mna mambo ya ajabu sana. Siku ya Jumanne tarehe 12 july nililipia Motor vehicle road licence shilingi 170,000 kupitia namba 0754327452. Mkakata hiyo hela ila meseji haikurudi. Nimejaribu kuwapigia customer care zaidi ya mara NNE kila mmoja ananipa jibu lake. Nyie hamjielewi kweli kweli. Mmoja aliniambia linashighulikiwa nitapata meseji baada ya muda mfupi, nikasubiri weeee! Mwingine aLIniambia nisubiri hiyo hela iko "hewani" eti muamala utakuwa cancelled nitarudishiwa BAADA YA MASAA SABINI NA MBILI! NIMESUBIRI HADI LEO NI WIKI NZIMA SASA!! HAMNA KILICHOENDELEA!! Kwa hiyo nitakuwa penalised na TRA kwa kuchelewa kulipia road licence kwa sababu ya uzembe wenu uliotukuka!! Kama "mtandao ulikuwa unasumbua" kwa nin mkate pesa yangu??
Wapuuzi sana nyie. Mmenitia hasara sana kiukweli. Na siku zote hizo mlizokaa na pesa yangu, mtanilipa na riba??
This ia so disappointing!!!
Vodacom Tanzania


Yaani kwa uliyosema hapo kwa kweli voda wanakera Sana,
Hao wapokea cm sijuh Kama wanajielewa kweli bora wafunge Tu hicho kitengo Ni uhun mtupu
 
Inakuaje matatizo yenu alaf mnatupa usumbufu wa ajabu ajabu

Mtu anatuma hela mnakata alafu mnasema hela ipo hewani itarudishwa baada ya masaa 72,

Masaa yanapita na hela hamrudishi alafu wahudumu wanajibu kwa nyodo, na kila mmoja anajibu lake.

Bora hicho kitengo cha cm mkitoe tu mana ni kero mnakaaje na hela ya mtu week na zaidi na bila maelezo yanayoeleweka!
 
Na hili la kununua kifurushi aidha cha mdomo ama internet cha saa24 unapoanza kuvitumia tu, sms za muda wa matumizi kumalizika zinaanza kumiminika mfululizo!
Ukiuliza salio unakuta vifurushi bado vimejaa. Hapo inamaanisha usipoangalia salio ukaziamini sms, utalazimika kununua kifirushi kingine wakati ulichotangulia kununua bado kipo!
Uhuni wote huo ni kwa faida ya nani?
Ninaelewa siyo kampuni kubwa kama Voda inaweza kufanya uhuni wa kishenzi namna hiyo,ila ni wafanyakazi "pasoneli" kitengo cha IT na huduma kwa wateja.
Kila pahala pa huduma Voda ni kero,kero,kero!
Me ninasema kwa hii dunia ya ushindani wa kibiashara, ninawatabiria kufa kifo cha kawaida kabisa cha mende, miguu juu.
Kama mnadhani ninyi hakuna wa kuwapiku, waulizeni TTCL kilichowaua ni kitu gani?
Ni ujingajinga tu, mara EMS, halafu mtu akituma pesa wanajikopesha kwanza, mteja anaanza kusubiria.
Wakaja na simu zao za mtandao mmoja! Sasahivi wako wapi!
Hivi ajira zenu mnaziwekaje rehani kwa kuwajibika kihunihuni namna hii wakati ajira inatafutwa kama almasi?
Mwenye masikio na asikie!
Lakini kama ni sikio la kufa halitasikia dawa na hii sehemu yenu humu jf ya kuchukulia maoni na mapendekezo, sidhani kama kuna staff yeyote anayehangaika kusoma na maoni kuyafanyia kazi! Maana kero zinazoongelewa ni hizohizo zinazidi kujirudia na staff kukoment kujibu kero ni ngumu sana kama ngamia kupenya tundu la sindano. Inamaana hapa tunapigia gitaa mbuzi acheze.
 
wagumu sana kwa kutoa sio kama tigo,tigo kila wanatuma mb bureee,ila sio voda,vifurishi vingi havina ushawshi wa kujiunga
 
Nimekosea kutuma kumbukumbu namba customercare anashindwa kunisaidia nifanyeje?kama transaction niliyofanya imekosewa mteja sijui namba ya nilikokosea,hawa watu wako Kenya ila pesa zao kuja ama kwenda kwao zinapitia kwenye Mpesa nisaidie nimekosea au niko sahihi?
 
Habari wadau! poleni na majukumu ya kulijenga taifa,
Niende Kwenye Mada Ambayo Kampuni Ya Mawasiliano Nchini Ya Vodacom Inahusika Kwa Ukaribu Sana. Nimekuwa Mtumiaji Mzuri Wa Huduma Zao Kwa Muda Mrefu Sasa, Ila Kuna Tatizo Nimeona Limeanza Kujitokeza Ndani Ya Miezi Mitatu Hii Ya Karibu, ni kuhusiana na Huduma Ya Kutuma Na Kupokea SMS Inasumbua sana kuanzia majira ya usiku saa moja hadi saa 5 usiku, unatuma sms inachelewa sana kumfikia mlengwa inaweza ikakaa kuanzia dakika 6 hadi 10 kumfikia mlengwa.,mwanzoni niliamini hii simu yangu ya kisasa itakuwa ndo chanzo nikaamua kuingia vodashop nikanunua simu ya kawaida inayoruhusu kukaa laini ya vodacom tu kwa elfu 18,000 tu, bado nikaona tatizo halijaisha, nikawaulizia jamaa zangu ambao wapo mikoa na wilaya tofauti nao wakanithibitishia kuwa wanasumbuliwa na tatizo hili.
Vodacom Chondechonde Tatueni Hili Tatizo Msijiharibie Sifa Yenu Nzuri Ya Kutoa Huduma Mliyojiwekea Katika Jamii. Mnakoelekea Mnatafafana Na Mtandao Flani Ukituma Sms Inafika Kesho Kwa Mlengwa.
 
Tafadhari Vodacom tunaomba mtuondolee kero za SMS nyingi za matangazo yenu ya kushiriki droo za bahati nasibu zenu. Meseji zinakuwa nyingi mmno zinaweza kufikia 12 aunzaidi kwa siku. Nilipiga simu huduma kwa wateja kuomba mniondoe katika list yenu ya mnaowarushia matangazo. Nazungumzia zile SMS zenu za "Namba 075xxxx imechaguliwa ...." au zile za "Kamata Mkwanja ...." au "Nyumba unayotafuta imepatikana..." zipo nyingi sana hadi ni kero, tafadhari wekeni sehemu ya kumuwezesha mteja ku-UNSUBSCRIBE kutoka ktk hizi huduma za matangazo. Simu imekuwa kama Bilboard sasa.
 
Nataka kubadili jina la usajili wa namba yangu niliwai fanya hvyo mpaka sasa sijafanikiwa nifanyeje???
 
Tafadhari Vodacom tunaomba mtuondolee kero za SMS nyingi za matangazo yenu ya kushiriki droo za bahati nasibu zenu. Meseji zinakuwa nyingi mmno zinaweza kufikia 12 aunzaidi kwa siku. Nilipiga simu huduma kwa wateja kuomba mniondoe katika list yenu ya mnaowarushia matangazo. Nazungumzia zile SMS zenu za "Namba 075xxxx imechaguliwa ...." au zile za "Kamata Mkwanja ...." au "Nyumba unayotafuta imepatikana..." zipo nyingi sana hadi ni kero, tafadhari wekeni sehemu ya kumuwezesha mteja ku-UNSUBSCRIBE kutoka ktk hizi huduma za matangazo. Simu imekuwa kama Bilboard sasa.
Tena wanatumalizia chaji tu. Matangazo wapeleke Itv na magazeti
 
. Nilituma pesa tangu juzi saa mbili jioni,
lakini cha kushangaza sms ya malipo
kwangu haikuja na wala kwa
niliyemtumia pesa haikumfikia pia.
Wakati huo huo huku salio langu
linaoneshwa nimekatwa pesa... !
Sasa tangu juzi na jana nimewapigia
mara nyingi nachoambiwa pesa ipo
hewani tayari nivute subira
wanarekebisha mitambo yao, uvumilivu
umenishinda aisee..Vodacom hiyo pesa
ilikuwa na umuhimu mkubwa na wala
sina pesa nyingine madhara
mlionisababishia ni makubwa mno. Sasa
basi mnirudishie tu pesa yangu ili nijue
nitaitumaje....
 
. Nilituma pesa tangu juzi saa mbili jioni,
lakini cha kushangaza sms ya malipo
kwangu haikuja na wala kwa
niliyemtumia pesa haikumfikia pia.
Wakati huo huo huku salio langu
linaoneshwa nimekatwa pesa... !
Sasa tangu juzi na jana nimewapigia
mara nyingi nachoambiwa pesa ipo
hewani tayari nivute subira
wanarekebisha mitambo yao, uvumilivu
umenishinda aisee..Vodacom hiyo pesa
ilikuwa na umuhimu mkubwa na wala
sina pesa nyingine madhara
mlionisababishia ni makubwa mno. Sasa
basi mnirudishie tu pesa yangu ili nijue
nitaitumaje....
Hawa jamaa wakati mwingine ni kama manyang'au. Walikwangua mb zangu zote na kisha kunikwangulia salio langu la kawaida ndani ya dk kama 4 hivi lote kisha wakanitumia sms eti nimetumia 100 kutoka ktk salio langu la matumizi ya internet ya 50,000/=
Leo imepita kama wiki ndiyo wananitumia sms kuwa nimetumia 7,000 kama inavyo onekana hapo kwenye kiambata ambacho ni kiasi cha salio nililo kwapuliwa siku hiyo.
Na wanafanya hivi baada ya kuwa nimeishiwa bandle utadhani sikuwa na bandle kwamba nilikuwa nikitumia salio hilo.
Huu ni wizi tena wa wazi wazi kama ujambazi.
 

Attachments

  • 1479041103218.png
    1479041103218.png
    35.9 KB · Views: 61
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Vodacom, mimi ni mkazi wa kijiji cha Ikana, wilaya ya Momba, mkoa wa Songwe. Tatizo linalotukabili sisi wakazi wa kijiji hiki ni kwamba tumekosa mawasiliano hususan ya kupiga simu kuelekea kwa mtu mwingine ambapo simu zimekuwa haziendi (fail) endapo tukiwa tunawapigia watu wengine ili tuwasiliane na endapo mtu wa mbali akitupigia simu pekee, huwa inafanikiwa kuingia na kufanikiwa kuwasiliana.
Tatizo hili limeanza tangia tarehe 3/11/2016 na tumekuwa tukipata changamoto kubwa kutokana na wanakijiji wengi tumekuwa tukiutegemea na kuutumia mtandao huu kwa kiasi kikubwa kuliko mitandao mingine na sasa tunashindwa hata kuwasiliana kwa masuala yetu ya kijamii.
 
Vodacom na nyie tumewachoka huku boda murongo hebu tuleteeni 3g bhana mbona wengine Mtandao ya 3g wameweka
 
Back
Top Bottom