Vodacom sasa watapatapa kutafuta wateja

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,022
1,305
Ni dhahiri kwamba kutokana na kukerwa na huduma mbovu za Vodacom wateja wengi wameuhama mtandao huu na kuhamia mitandao mingine.

Mfano nina wateja wa vodacom 110 kwenye simu yangu. Kati yao, 92 wamenijulisha kuwa wamehamia airtel kwani wamekerwa na huduma zao. Wanatoa hoja hizi:

A. Ukituma sms inachelewa kumfikia mhusika wakati simu iko hewani.

B. Makato makubwa ya kutisha ya M-Pesa.

C. Dakika 1 isiyo na faida kwa mteja (wanasema haitoshi).

D. Usumbufu wa kukatika mara kwa mara kwa mtandao na haupo makini kila sehemu kuanzia mjini.

E. Ukisafiri kuelekea nje ya mji huna mawasiliano na unakotoka wala unakokwenda.

F. Kukimbia kwa haraka dakika za cheka bombastiki. Mmoja akatoa mfano kuwa utaongea dakika 2 ukija kuangalia salio utakuta zimekwenda dk 3-4

G. Mnara wao unamaliza haraka sana chaji (kisayansi kudumu kwa chaji huendana sana na provider.
Kwa mtazamo wangu, kama idadi hiyo wamehamia mitandao mingine hasa airtel, hakuna sababu ya kujiita mtandao "unaoongoza" Tanzania. Hapo unaoongoza iwe "unaohamwa"
 
mengine sijui ila iyo A ya sms kuchelewa ni kweli,mpenzi wangu yuko voda mi kwingine,kila siku tunalaumiana mbona sms zake akituma zinanifikia baada ya masaa au hata kesho yake mi nikituma zinawahi kama kawaida!.
 
mengine sijui ila iyo A ya sms kuchelewa ni kweli,mpenzi wangu yuko voda mi kwingine,kila siku tunalaumiana mbona sms zake akituma zinanifikia baada ya masaa au hata kesho yake mi nikituma zinawahi kama kawaida!.
Tatizo lako ni kama la kwangu tu..nmeshazoea msg za usiku kuzipata asubuhi hawa voda sijui wana nni..!
 
A.ni kweli sms zinatumwa sa1jioni zifika kesho asubuhi ingawa sio kila mara kwa hiyo kama mtu unaishu yako ya muhimu usijidanganye eti utume ujumbe ni bora upige tu hata kama upo sehemu yenye makele.
 
hata mimi niko mbioni kwa mfano ukiwa una sh1000 kwenye simu ukajirusha cheka ya mia 400 pindi dk zako zinapoisha awakupi taharifa kama wanavyofanya kwenda mitandao mingine. matokeo yake wakata naile mia600 iliyobaki
huu ni wizi.
 
Tatizo lako ni kama la kwangu tu..nmeshazoea msg za usiku kuzipata asubuhi hawa voda sijui wana nni..!

Kwa kweli wanaudhi. Jana tu saa 11 jioni nilinunua LUKU kupitia m-pesa. Sms kunijulisha nimefanikiwa imekuja saa 3 usiku! Imagine. Muda wote tunasubiri tuko gizani. Jirani yangu aliishiwa luku saa 2 usiku. Ndani ya dakika 5 akawa amenunua umeme kupitia Tigopesa. Nimekoma. Sitathubutu tena kununua luku kupitia m-pesa.
 
Nakubaliana kabisa na wewe mkuu Pastor kwani mimi kuna siku niliamua kujiunga na bando la 5000 ili nipige mitandao yote kwa wiki nzima kuepusha kujiunga kila siku, lakini matokeo yake nilijuta kuujua mtandao wa vodacom.

Unajua kwa nini! walinipa dakika 100 mitandao yote. Kiukweli nilitumia ndani ya siku tatu tu wakanambia zimeisha. Hiyo sio ajabu kwani yategemea na upigaji wa simu, ila ni kwamba, upigaji wangu ni mdogo sana kiasi kwamba kwa siku ni mara chache kuzidisha dakika 15. Dakika hizohizo nikijiunga tigo kwa mitandao yote nafikisha wiki nzima au ikipungua labda siku moja tu.

Kwa hiyo voda ni wezi acha watu wakimbie. Mimi toka siku ile sijaweka tena vocha. Natumia mitandao mingine
 
mengine sijui ila iyo A ya sms kuchelewa ni kweli,mpenzi wangu yuko voda mi kwingine,kila siku tunalaumiana mbona sms zake akituma zinanifikia baada ya masaa au hata kesho yake mi nikituma zinawahi kama kawaida!.
Bila shaka mpenzi wako yuko Tigo, hilo ni tatizo la Tigo.
 
Punguza mahaba! Penye ukweli lazima tuseme, mimi nimemtumia sms mtu jana saa 18:8,amekuja kuipata saa 23:45.usiku! Unapotoa kasoro ya kitu fulani unachokitumia haimaanishi hukipendi bali unataka kirekebishwe! Voda plse take action! Otherwise.....!@Malignat Tumor!
 
likingine kero kuu ni kukuwekea huduma ya nyimbo bila ya idhini yako,mke wangu anatumia voda mi nilihamia airtel na tigo toka mwaka jana,sisi ni wakristo nikimpigia mke wangu nyimbo inayoita ni kuruan


Kha ha ha ha ha ha ha haaaaaa! Pole sana Mkuu Marire karibu Zantel ongea pole pole!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom