Pastor Achachanda
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 3,022
- 1,305
Ni dhahiri kwamba kutokana na kukerwa na huduma mbovu za Vodacom wateja wengi wameuhama mtandao huu na kuhamia mitandao mingine.
Mfano nina wateja wa vodacom 110 kwenye simu yangu. Kati yao, 92 wamenijulisha kuwa wamehamia airtel kwani wamekerwa na huduma zao. Wanatoa hoja hizi:
A. Ukituma sms inachelewa kumfikia mhusika wakati simu iko hewani.
B. Makato makubwa ya kutisha ya M-Pesa.
C. Dakika 1 isiyo na faida kwa mteja (wanasema haitoshi).
D. Usumbufu wa kukatika mara kwa mara kwa mtandao na haupo makini kila sehemu kuanzia mjini.
E. Ukisafiri kuelekea nje ya mji huna mawasiliano na unakotoka wala unakokwenda.
F. Kukimbia kwa haraka dakika za cheka bombastiki. Mmoja akatoa mfano kuwa utaongea dakika 2 ukija kuangalia salio utakuta zimekwenda dk 3-4
G. Mnara wao unamaliza haraka sana chaji (kisayansi kudumu kwa chaji huendana sana na provider.
Kwa mtazamo wangu, kama idadi hiyo wamehamia mitandao mingine hasa airtel, hakuna sababu ya kujiita mtandao "unaoongoza" Tanzania. Hapo unaoongoza iwe "unaohamwa"