Viwanda viwili vyaisoma namba mkoani Pwani na sasa vimefungwa

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Taarifa toka chanzo cha kuaminika zinadai viwanda 2 vyote viko wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, vimefungwa baada ya kukosa soko la bishaa zake.

Kimoja kilikuwa kikitengeneza mafuta ya kujipodolea na kingine kilikuwa kikitengeneza viungo vya msosi (kilikuwa kikiitwa Vegeta).

Hiki Vegeta hakijamaliza hata mwaka tangu kizinduliwe na waziri mkuu.

Taarifa hizi zinakuja huku kukiwa na kilio cha Nape kuhusu uchumi wa gesi mikoa ya Lindi na Mtwara juu ya kuondoka kwa makampuni yaliyokuwa yamejitokeza kuukukuza uchumi huo. Bila kusahau giza liliotanda kuhusu Dangote na kilio cha soko cha yule muwekezaji wa sukari kule Zanzibar. Najiuliza ndoto ya viwanda itatimia??
 
Hatutaki Viwanda vikubwa, ni anasa, Tunataka kuishi kama Mashetani. Viwanda vyetu ni saluni tu na cherehani zinatosha
Hahahaha hadi mjinyonge. Magufuli hamtaa mumuweze nyie wapiga majungu. Nchi iko mstari ulionyooka haijapata kutokea. Mara ooh mhutu. Mtajiju wenye wivu mlizoea kuuza madawa ya kulevya na kuiibia serikali
 
Tanzania ya viwanda ni msemo tu, utekelezaji ni suala lingine kabisa.. Huwezi ukaanzisha sera ya viwanda wakati mipango thabiti haipo.. Kabla ya kufikia kuanzisha viwanda lazima Sector ya kilimo iwe bora kabisa kwa ajili ya raw materials kufeed hivyo viwanda, lakin leo sector ya kilimo hali mbaya kabisa, huwezi kuanzisha viwanda wakat huo nishati hakuna, au ipo na si ya uwakika..

Uwezi kuanzisha sera ya viwanda bila kuwa na sera mathubuti ya kulinda viwanda vya ndani.. Leo hii same products made in Tanzania na ingine ukienda sokoni ya Tanzania ina bei kubwa zaid ya ile ya nje.. Hata Waingereza wakat wanaanza industrialization walilinda soko la ndani kwa kubana bidhaa za nje.. Leo hii kuna bidhaa zinaingia either kwa msamaha wa kodi au kwa kodi kidogo lakin bidhaa zetu kodi ipo juu.. Tanzania ya viwanda inawezekana ila kwa ss ni ndoto isiyo kuwa na utimilifu kabisa.
 
Umeanza vizuri lakini umekuja kuharibu kuingizia mambo tofauti tofauti mara gesi mara NAPE mara Dangote mara Sukari Zanzibar.
 
Hchi changu cha vitandaa krb nakifungaa maana wateja hkn .kila MTU analia hali ngumu
FB_IMG_15237630256024932.jpg
 
Taarifa toka chanzo cha kuaminika zinadai viwanda 2 vyote viko wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, vimefungwa baada ya kukosa soko la bishaa zake.

Kimoja kilikuwa kikitengeneza mafuta ya kujipodolea na kingine kilikuwa kikitengeneza viungo vya msosi (kilikuwa kikiitwa Vegeta).

Hiki Vegeta hakijamaliza hata mwaka tangu kizinduliwe na waziri mkuu.

Taarifa hizi zinakuja huku kukiwa na kilio cha Nape kuhusu uchumi wa gesi mikoa ya Lindi na Mtwara juu ya kuondoka kwa makampuni yaliyokuwa yamejitokeza kuukukuza uchumi huo. Bila kusahau giza liliotanda kuhusu Dangote na kilio cha soko cha yule muwekezaji wa sukari kule Zanzibar. Najiuliza ndoto ya viwanda itatimia??
Sisi tushaanza kununua vyerehani 4 tu hicho ni kiwanda
 
Hahahaha hadi mjinyonge. Magufuli hamtaa mumuweze nyie wapiga majungu. Nchi iko mstari ulionyooka haijapata kutokea. Mara ooh mhutu. Mtajiju wenye wivu mlizoea kuuza madawa ya kulevya na kuiibia serikali
Kwamaana nyingine hivyo viwanda kushindwa kufanya kazi au kufungwa ni fitina ?
 
Back
Top Bottom