Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

made

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
890
581
Idadi hiyo imeokotwa ktk mifuko ya viroba. Ni hali ya kusikitisha kwa kweli miongoni mwao wapo watoto.

========

POLISI mkoani Dar es Salaam wamekamata mafurushi ya mifuko yakiwa na viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto ya Bunju wilayani Kinondoni, FikraPevu imefahamishwa.

Tukio hilo lililoibua hisia kali kwa wananchi limesababisha polisi kufyatua mabomu ya machozi kudhibiti wananchi waliofurika na kutaka kuvamia kituo cha polisi kumkamata dereva wa gari lililokutwa na viungo hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Cammillius Wambura ameithibitishia FikraPevu kukamatwa kwa viungo hivyo lakini hakuingia undani kutokana na kuwapo eneo la tukio Bunge, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, katika barabara iendayo Bagamoyo.

Taarifa zilizoifikia FikraPevu usiku wa Jumatatu Julai 21, 2014 na kuthibitishwa Kamanda Wambura, zimeeleza kwamba viungo hivyo vimeokotwa katika machimbo hayo Jumatatu jioni vikiwa katika gari aina ya Toyota Hilux Pickup ikidaiwa kuwa ilifika hapo kwa mara ya pili kumwaga viungo hivyo.

"Ni kweli tumepata taarifa hizo muda mfupi uliopita na sisi tumefika katika eneo la tukio kwa taarifa zaidi tutawapa baadae tuko katika eneo la tukio hatuwezi tuzungumza," anasema Wambura.

Taarifa zinasema miili hiyo imeonekana ikiwa imetelekezwa katika eneo hilo pamoja na kufungwa kwenye mifuko hiyo, ikiwa imekaushwa huku baadhi ya viungo vikionekana kua vya watu wazima. Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia FikraPevu kuwa baada ya Jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio wameondoka na miili hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Gari lakamatwa likiwa na shehena ya viungo vya binadamu

Katika tukio hilo polisi walitumia mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto hewani, kutawanya wananchi waliovamia Kituo cha polisi cha Bunju 'A' wakitaka kumchukua na kumuua dareva aliyekamatwa na gari isiyofahamika namba mara moja ikiwa imesheheni viungo vya binadamu.

Taarifa zilizoifikia FikraPevu majira ya saa nne usiku zinadai kuwa, polisi katika Kituo cha polisi Bunju A na Wazo jijini Dar es Salaam, wamepiga mabomu ya machozi na risasi za moto hewani kwa lengo la kutawanya wananchi hao.

Mashuhuda wamesema kwamba wananchi walijawa na hasira baada ya kupata taarifa kwamba baadhi ya viungo vilikua havijakauka baadhi vikielezwa kuvuja damu.

Dereva huyo anadaiwa kummwaga viungo hivyo mara ya kwanza, katika Shule iliyotajwa kwa jina la Consolata inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, na kuwa baada ya wananchi kushuhudia tukio hilo waliripoti polisi ambao waliofika na kulikamata gari hilo.

FikraPevu inaendelea kufuatilia tukio, kadri tutakapopata taarifa zaidi tutawajulisha.

=========

Nukuu ya mwanafunzi wa IMTU.

"for a while our university administration imekua na matatizo..iliwahi kutokea miaka ya nyuma scenario kama hiyo ambapo mwanafunzi alieonekana na mkono mtaani of which hairuhusiwi hata kutoka na groves inje ya hicho chumba..sasa semester one ilimaliza kutumia hizo dead body on march zikatakiwa zitupwe..kwakua kifaa kilikua kibovu waliomba MuHAS wawasaidie ambapo inasemekana walisema nao kifaa(according to the guy anayehusika) chao kina shida wakaomba hindu mandal wakatakiwa kutoa 7m..ikacheleweshwa kutolewa..

Leo umoja wa vyuo vya madaktari Afrika mashariki ulikuja for inspection kwakua hazikutakiwa kuonekana wakaamua kufanya hivyo of which is illegal..

On friday nilikua mwenyewe ofisini and i heard one of teachers anaongelea kuzitoa hizo dead bodies"
 
maiti zaidi ya 100.....what a f@????? hii hatari, hebu tupe habari zaidi mkuu
 
itakuwa bunju ya GAZA,,, watu 100 sio mchezo lazima ingekuwa issue ya kitaifa
 
Bado sijaamini hebu dadavua kiundani zaidi ni katika mazingira gani, hali kiujumla ni vp hapo tupe update mkuu
 
Bado sijaamini hebu dadavua kiundani zaidi ni katika mazingira gani, hali kiujumla ni vp hapo tupe update mkuu

unajua mleta mada kaileta issue hii kimzamzaa wkt kama ni kweli ni kitu si cha masihara.atupe habari kamili au yeye naye kaambiwa
 
Hata mm nasikia kutoka kwa watu bhana!!!sina uhakika..

kwahiyo nyinyi ndio mliodikia mwai kibaki kafa mkaleta uzushi wenu humu? ujinga mtupu.

nyinyi ndio mliosababisha Tanzania iwe ranked in top 10 poor iq's population.
 
du, yani habari muhimu kama hii unaileta kigazeti pendwa, bila more details, watu 100 si idadi ndogo ndugu, ebu ilete ikiwa imekamilika, huku kupost kwa haraka hakutusaidii sisi kuielewa habari yako.
 
TBC wametangaza sasa hivi kuwa ni viungo vya binadamu ambavyo vilikuwa kwenye mifuko vimekutwa katika eneo la kutupia takataka lakini idadi haijasemwa kwakua imefika kama habari iliyofika punde (breaking news) kwahiyo bado hawajotoa taarifa kiundani.
 
Back
Top Bottom