Vituo vya afya 807 nchini kujengewa wodi za wagonjwa

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Katika mwaka wa fedha 2024/25 serikali omesema itaanza ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa katika vituo vya afya 807 nchini kikiwamo Kituo cha Afya cha Kihangara wilayani Nyasa.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Nyasa, Stella Man-yanya (CCM) bungeni Dodoma jana, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mi-taa (Tamisemi), Deogratius Nde-jembi alisema serikali imedhamiria kutekeleza hilo katika vituo vya afya vilivyokwisha kupokea fedha za ukarabati na ujenzi.

Manyanya katika swali lake la msingi alitaka kujua ni lini serikali itajenga wodi katika Kituo cha Afya Kihangara.
Ndejembi alisema katika Mwaka wa Fedha 2024 /25 Ofisi ya Rais (Tamisemi) inakusudia kuanza ujenzi wa wodi hizo katika vituo vya afya 807 kikiwamo kituo cha Kihangara.

Ndejembi alisema ili kuboresha huduma za afya nchini, serikali imeanza na uboreshaji wa miundombinu ya vituo vya afya, kipaumbele kikiwa ni utoaji wa huduma za dharura na upasuaji ambapo fedha iliyotolewa iliele-kezwa kujenga jengo la wazazi, la upasuaji, la maabara, la kufulia na nyumba ya mtumishi
 
Back
Top Bottom