Vituko vya wale ngedere wetu

Khaaah
Mie nilizani umetumia lugha ya picha kumbe umeenda moja kwa moja.
 
Mbona hukuweka selfie zako na hao ngedere kwa ushahidi?
 
sokwe,,,nyani,,ngedere,,kima,,mbega,,hao wote ni jamii moja na tabia zao hushahabiana na binadamu
 
Wanabodi nawasalimu sana!

Ngedere ni wanyama Jamii wenye haiba ambayo kwa kiasi Fulani inataka kufanana na binadamu. Kwa Tanzania Ngedere ni moja ya wanyama wanaopatikana maeneo mengi na hivyo kujulikana na wengi. Kwa DSM, Ngedere wapo maeneo mengi tu lakini ndani Chuo Kikuu DSM (UDSM) wanapatikana kwa wingi sana. Kwa UDSM, Ngedere hawa wamekuwepo miaka na miaka, Mazingira ya UDSM ni rafiki kwa Ngedere hawa! Na kwa pale UDSM, kuna kumbuizi anuai za Ngedere wale. Baadhi yake ni hizi!

Ngedere wanaopatikana UDSM, wameweka record ya kuwa Mabishoo kuliko Ngedere wote wanaopatikana Tanzania na hasa mikoani. Ndio Ngedere wanaoongoza kuwa na swaga na uwezo mkubwa wa kuonyesha mapozi, ni kawaida kabisa kukuta Ngedere hawa wakionyesha mahaba ikiwemo kukumbatiana tena mchana wa jua kali katika viunga vya UDSM mf Nyuma ya Jengo la UCC au pale maeneo jirani na Yombo cafeteria! Hawa ndio Ngedere wasioogopa kelele za magari wala watu! Pia wanao uwezo wa kukuongozana na sister duu mkali kwa umbali flani ikitokea tu dada huyo anacho kilichowavutia!

Ngedere hawa wa UDSM, wanakulaChips, wanakula slices za mikate, wanakula slices za mikate zenye jam, wanakula slices za mikate zenye blueband. Kifupi Ngedere hawa hawana maringo linapokuja swala la kula. Washazoea kula vile anavokula Mwanadamu wa Jamii ya UDSM, wanakula pilau, wanakula choclate! Pia Ngedere hawa wanaweza kuongeza chumvi ama pilipili kwenye kitu anachokula incase wamehisi haijatohsa! Nimewahi kumshuhudia Ngedere akitafuna Banzoka maeneo ya karibu na cafeteria ya pale COET!

Ngedere wa UDSM, wanajua mwisho wa semester. Kwa kifupi Ngedere wa UDSM wanaijui academic calendar ya UDSM, wanajua misimu ambayo wanafunzi wa UDSM wako vizuri, wako na boom, na wanajua ni wakati gani wanafunzi wanakulia majalala, wamefulia. Mwishoni mwa semester Ngedere hupunguza safari zao kuelekea campus huku wakijua kwa wanafunzi hawana kitu wengi wao, pili hupunguza mishe zao ili kuwapa fursa wanafunzi na utulivu wa masomo na mitihani!

Ngedere wa UDSM wanapiga selfie. Ngedere wa UDSM hawana simu. Lakini utashangaa imekuwaje Ngedere hawa wanapenda kupiga selfie! Ngedere wa UDSM wanajua na wanapenda selfie, wanajua dalili za wanafunzi kutaka kupiga selfie, wakiona dalili hizo, Ngedere hawa hujisogeza karibu na wanafunzi wanaotaka kupiga selfie, na kama wanafunzi hawa hawatajali, basi ngedere hawa hutokezea katika selfie hizo. Binafsi nimepiga nao sana selfi kuanzia pale mdigrii mpaka kule Mathematics kwenye vile vigarden jirani na UCC!

Ngedere wa UDSM wana utamaduni wao mzuri sana wa kuwahi kureport chuoni kabla wale wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza hawajareport, lengo huwa ni kuwapokea na kuwasaidia kujua kwamba sasa wamefika UDSM "Mlimani"

Pale UDSM eneo la Utawala, ukiwa unatokea kituo bondeni upande wa kushoto wa Barabara kuna mti mkuwa ambao Ngedere huwa wanautumia kujivinjari kwa kubembea na wakati mwingine huruka mpaka mti wa ng’ambo ya Barabara, ilitokea siku moja katika misafara yao Ngedere mtoto akagongwa na gari na kujeruhiwa vibaya! Yule ngedere mwana hakufa lakini kilichofuata pale, waliokuwepo UDSM siku ile ni mashahidi!

Ngedere wale haijulikani walitumia aina gani ya Mawasiliano lakini waliitana wengi kupitiliza, na kwamba wana umoja kuliko ule wa wavuta sigara! Kwa kutumia maarifa yao walioyapata kwa kuwepo UDSM kwa muda mrefu, Ngedere walifunga Barabara, hamna kwenda wala kurudi kwa kutumia University rd! Ngedere madume makubwa makubwa baadhi yakiwa na O kidevuni na wengine wameachia uchebe, yalikuwa yakiparamia vioo vya magari yaliyolazimisha kupita pasi, police wa auxiliary walifanya kazi ya ziada kuwapa watu tahadhari juu ya uwepo wa Ngedere wenye hasira!

Kwa kawaida, Ngedere ana uwezo wa kuishi kwa Umri wa miaka 12-45. Ndio kusema inawezekana kabisa kuwa na Ngedere Mwenye Degree, Masters ama PhD kama itatokea ulisoma degree UDSM, Masters mpk PhD na Ngedere akiwepo, mapaka ulipograduate alikuwepo, basi hiyo degree yako si yako pekeako!

Ushauri wa bure, kama utakutwa na sintofahamu yoyote maeneo ya ugenini ama porini, hujui ule nini katika sintofahamu hiyo, tazama kama kuna Ngedere karibu! Kula alacho Ngedere! Hutajutia!

Binafsi sijutii, kula alacho Ngedere!
Mliosoma UDSM mnacho cha kurudisha kwa Ngedere hawa!
Wanaijua lugha ya Malkia!??
 
Yaani wewe umeacha kusoma unafanya utafiti wa tumbiri...haya!declare interest kama upo zoology department...ila hao wenye O umetupiga chepeo!
 
Back
Top Bottom