Vitu unavyotakiwa kufahamu ili uwe front end developer mzuri

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,208
1,755
Salamu wana jamvi/jukwaa ni vyema kujifunza na kuielewa technology hii kifupi niseme ndani ya uzi huu hatutajifunza language yoyote inayoendana na kazi hii ila ukiwa na swali waweza uliza na wadau watachangia.
Nianze kwa njia ya kujijibu katika maswali karibu!.

1. Je, utakapo master/kuwa na uelewa Mzuri katika lugha hizi html/html5,css/css3,pure javascript/jquery library inatosha kuwa front end developer MZURI ?

TUANZE HIVI:
html na css ni msingi wa kwanza ambao unatakiwa kuuelewa kwa undani kabla ujaruka kwenda javascript hivyo kukuraisishia kazi ya kudevelop front end pages zikiwa na mvuto na mwonekano mzuri.
Baada ya hapo unatakiwa ujifunze javascript kwa utaratibu, mwanzoni javascript uonekana haieleweki, kwasababu wengi uikimbilia wakiwa na msingi mbovu kwenye html na css hivyo mwishoni uichukia na kuachana nayo wakiwa wamekata tamaa kabisa.
Na hizi lugha tatu uwezi zikimbia hata mojawapo, lazima uzijue zote la sivyo unaweza fanya vitu vingine na sio hii profession asikudangamye mtu wala asikukatishe tamaa mtu unapojifunza lugha hizi muhimu kwa ajili ya front end website development.

JE LUGHA HIZI ZINAFANYA NINI SASA ?
Html
- ni kwaajili ya uandishi wa maudhui ya kurasa/pages za website wakati Css inapamba hayo uliyoandika kwenye kurasa.
mfano:
Ukiangalia kwenye website ya jamiiforum utaona logo/membo ya jf iko kushoto hapo ni css imetumika kuiweka upande huo wakati logo/nembo yenyewe imo nani ya html

Javascript - utumika kutoa uhai kwenye page husika mfano ukiwa unatumia simu ku peruzi jamiiforum ukitouch menu unaona ni kama inatokea kulia kuja kushoto halafu contents nyingine zinafifia bila hii lugha ukitouch hapo hakuna kinachotokea hivyo mtumiaji hawezi kuona menu.

jquery - hii ni library ya javascript inayookusaidia kudevelop front end kwa haraka bila utumia raw javascript lakini ili uitumie lazima uwe unafahamu javascript. N yenyewe ufanya kama javascript lakini ina mapungufu yake hivyo kuna library nyingine pia mfano ,react,Angular,ember na vue libraries.
napendekeza jquery kwa kuanzia ni rahisi sana.

JIBU:HAPANA!
KWANINI HAPANA?


Kuna technology nyingi unatakiwa kufahamu kama ifuatavyo;
Hizi ni technology muhimu
1.front end framework
Uchaguzi wa framework ya/za kujifunza uangalia popularity/wingi wa watumiaji uwezi kuacha framework ambayo inatumika kwa sana ukaamua kujifunza isiyotumika kwa sana.
mfano bootstrap ndo framework pendwa na wanatoa update mara kwa mara ili kuondoa mapungufu yanayo gunduliwa na watumiaji.
mbali na bootstrap kuna foundatiuon by zurb hii ndo inayofuata kwa popularity
so jifunze bootstrap kwanza.

2.Css preprocessors
Hizi sio framework ni scripting language zinazotumika kuitanua css ukizitumia ujibadilisha na kuwa css ya kawaida css preprocessors nzuri ni SASS na LESS.
mfano: ukiwa unaandika css ya kawaida unaweza jiukuta unarudia rudia baadhi ya property but ukiwa unatumia sass iunakusaidia ku declare variable kabla ya kutumia so utakua unaita tu kama niu color hutorudia kuiandika uta ita variable.
sass-vs-less-logos.webp



3.Responsive web design
huu ni uwezo wa kufanya web pages zote za website yako kuwa na uwezo wa kuzionyesha contents zote bila bottom scroll bar na pia contents zi fit au zikae kwenye window/screen ya kifa chako zikionekana vizuri hapa utatakiwa kujua css media queries au css frameworks na kitu kinaitwa flex box/grid utaweza fanya responsive design .

mfano:jamiiforum ikiwa kwenye desktop computer uonekana hivi

jamiiforums mwonekano katika desktop computer.png



jamiiforum ikiwa kwenye tablets uonekana hivi














jamiiforums mwonekano katika tablets.png


jamiiforum ikiwa kwenye smartphone uonekana hivi

jamiiforums mwonekano katika smartphone.png


unaona kwamba hakuna content ambayo mtu ataikosa akitumia smartphone au tablet au desctop computer.



4.cross browser development
hii ni technique inayo kusaidia kuifanya website ionekane sawa katika browser tofauti tofauti .kuna vitu haviwi supported mpaka umeapply hii technique page yako/layout inaweza kuwa na mwonekano mbaya kwenye internet explorer. au opera browser alafu ikaonekana vizuri kwenye chrome na microsoft edge kwa sababu hukutumia hii technique but now days browser zinasupport property nyingi kwenye css ,html but uwezi kusema hauitaji kuifahamu na kui apply hii technique basi utatapata tabu sana tu angalia hii article hapa

1. Developing cross-browser and cross-platform pages
2. CSS Reference Browser Support
3. HTML5 Browser Support


5.penda kutumia opem source project kama sehemu ya kujifunzia simaanishi utafute templates bali jumuika na watu wanaofanya project omba task mojawapo si kwaajili ya kulipwa fanya itakusaidia kujenga experience na kufahamika pia,

6.Fanya project muhimu tupia github au hata codepen andika pens nyingi pia unaweza ziedit watu wakionyesha makosa About CodePen kuusu sababu za kuitumia code pen hapa 9 Reasons You Should Be Using CodePen — SitePoint kusaidia wengine sio lazima ulipwe ila malipo huja baadae kumbuka ukienda kufanya interview na hauna sample work unatoka unalia tu utajivunia nini kama front end web developer ?
kama ulikuwa ufahamu juu ya github kwa kina soma hii article What Exactly Is GitHub Anyway?


TUTORIALS NZURI HIZI HAPA NA VITABU

VIDEO TUTORIAL
KAMA UWEZI NUNUA TUMIA TORRENTS DOWNLOAD HIZI VIDEO COURSE

html essential training
http://tparser.org/magnet.php?t=165309225

css essential; training
http://tparser.org/magnet.php?t=165590705

javascript essential training
http://tparser.org/magnet.php?t=165405227

jquery essential training
http://tparser.org/magnet.php?t=165308021

sass essential training
http://tparser.org/magnet.php?t=165092356

youtube playlist




















ukimaliza hizi ntafute tena
 

Attachments

  • HTML and CSS - Design and Build Websites - Jon Duckett - November 2011.pdf
    18.8 MB · Views: 33
  • JavaScript - The Definitive Guide - David Flanagan - 6th Edition - May 2011.pdf
    13.5 MB · Views: 112
  • JavaScript_Succinctly.pdf
    1.6 MB · Views: 79
  • jQuery in Action 3ed [2015].pdf
    10.3 MB · Views: 728
Last edited:
nakupendekezea vitabu na tutorials nzuri kwa ajili ya kujifunza hizi technology lazima uwive /uive kwa msaada wa ziada uliza hapa hapa

nime update
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom