Vitanzi na miiba michungu kwa CCM 2025

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Vichonganishi vya CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao ambavyo vimepigiwa kelele bila mafanikio na vimetafuna hazina za nchi bila huruma na bila tija ni vifuatavyo:-

1. NIDA.
2. BIMA YA AFYA.
3. TOZO.
4. TANESCO.
5. PEMBEJEO.
6. 10% YA MAPATO YA HALMASHAURI.
7. MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA NA WAMAMA.
8. KIKOKOTOO CHA MAFAO.
9. PENSHENI ZA WASTAAFU.
10. WABUNGE NA MADIWANI MIZIGO.
11. MIKWAMO YA MIRADI YA KIMKAKATI.
12. MIGOGORO MIPYA YA ARDHI.
13. BEI YA MAFUTA.

NB.
Hiyo namba 2 mngesubiri hadi 2026 ili uchaguzi upite salama kwanza kwa sababu sioni dhamira ya kuitekeleza kwa tija labda kama imewahishwa ili kukusanya ela za uchaguzi kupitia hiyo Bima.

Hakuna mpinzani atayeweza kukishinda CCM. Hivyo hizo 13 hapo juu ndiyo wachawi na wapinzani wa kweli wa CCM 2025.

Baada ya vyama vya upinzani sasa kuwa mfu rasmi, wapigakura wenyewe ndiyo wataibua upinzani ndani yao dhidi ya CCM pasina kuwa na chama cha upinzani; wakitumia agenda 13 hizo hapo juu.

CCM msipoteze muda na jasho kuhangaika na kuhofu vyama vya upinzani badala yake hofuni hizo agenda 13.

Kama tamu meza kama gwadu tema.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Umesahau DP wORLD.
 
Umesahau DP wORLD.
Hiyo ni agenda iliyotoa mimba (aborted agenda or miscarriage).

EU Commission inajenga mfumo mkubwa wa logistics unaoweza kuhudumia Afrika nzima wakichagua bandari ya Lobito na kujenga EPZ kubwa Zambia Kaskazini na DR Congo Kusini (zitazounganishwa na hiyo bandari) ambao hawa ndiyo wateja wa kimkakati na wa kihistoria wa TPA. Sasa DP World na TPA watafanya kazi gani?

EU Commission inashirikiana na Team Europe, G7 na kwa kuzingatia Paris Agreement.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
1. NIDA.
2. BIMA YA AFYA.
3. TOZO.
4. TANESCO.
5. PEMBEJEO.
6. 10% YA MAPATO YA HALMASHAURI.
7. MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA NA WAMAMA.
8. KIKOKOTOO CHA MAFAO.
9. PENSHENI ZA WASTAAFU.
10. WABUNGE NA MADIWANI MIZIGO.
11. MIKWAMO YA MIRADI YA KIMKAKATI.
12. MIGOGORO MIPYA YA ARDHI.
13. BEI YA MAFUTA.
afu wanamtuma kijana wa koromije, eti ndiye atoe majibu ya matitizo haya - unajua CCM wana utani mbaya sana.
 
Vichonganishi vya CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao ambavyo vimepigiwa kelele bila mafanikio na vimetafuna hazina za nchi bila huruma na bila tija ni vifuatavyo:-

1. NIDA.
2. BIMA YA AFYA.
3. TOZO.
4. TANESCO.
5. PEMBEJEO.
6. 10% YA MAPATO YA HALMASHAURI.
7. MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA NA WAMAMA.
8. KIKOKOTOO CHA MAFAO.
9. PENSHENI ZA WASTAAFU.
10. WABUNGE NA MADIWANI MIZIGO.
11. MIKWAMO YA MIRADI YA KIMKAKATI.
12. MIGOGORO MIPYA YA ARDHI.
13. BEI YA MAFUTA.

NB.
Hiyo namba 2 mngesubiri hadi 2026 ili uchaguzi upite salama kwanza kwa sababu sioni dhamira ya kuitekeleza kwa tija labda kama imewahishwa ili kukusanya ela za uchaguzi kupitia hiyo Bima.

Hakuna mpinzani atayeweza kukishinda CCM. Hivyo hizo 13 hapo juu ndiyo wachawi na wapinzani wa kweli wa CCM 2025.

Baada ya vyama vya upinzani sasa kuwa mfu rasmi, wapigakura wenyewe ndiyo wataibua upinzani ndani yao dhidi ya CCM pasina kuwa na chama cha upinzani; wakitumia agenda 13 hizo hapo juu.

CCM msipoteze muda na jasho kuhangaika na kuhofu vyama vya upinzani badala yake hofuni hizo agenda 13.

Kama tamu meza kama gwadu tema.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Kwa yote hayo hapo Juu sijaona hata Moja ambalo Lina mkwamo, pengine umekariri huelewi hata shida kubwa za Wananchi ni zipi.

Mfano unataka tozo,zipi hizo maana tozo zilishafutwa au wewe unaijua tozo ipi hiyo ambayo watu Wanalalamika?

Bima ya Afya ndio kwanza Inaanza,itakuwa effective 2027

Bei ya mafuta imefanyaje? Tanzania ndio tuna bei nafuu kuliko wote.

Tanesco wamefanyaje wakati bwawa litakuwa tayari na grid itakuwa imefika Kigoma na Katavi,umeme Vijiji vyote na Sasa ni Kusambaza Vitongojini

Hakuna mstaafu anaechukua hata miezi 3 bila mafao Kwa Sasa sana sana labda kama unasema waobgezewe malipo ya Kila mwezi

Vijana hawajawahi kuwa na mikopo Yao ,walikuwemo kwenye 10% ya Halmashauri ambayo Serikali inatengeneza utaratibu mzuri maana ule wa awamu watu wamepiga zaidi ya Bil.92 za Bure

NIDA imefanyaje wakati Kwa sasa vitambulisho vimeanza kugawiwa na Hadi Desemba 2024 Kila mtu atakuwa na Kitambulisho.

Pembejeo zimefanyaje Mzee wakati Mwaka wa 3 huu Rais anatoa ruzuku ya Mbolea?

Hiyo kikokotoo inaweza futws ila sijasikia jibu la Serikali.

Changamoto ya Wananchi Kwa Sasa ni Barabara ndio ziliibuliwa bungeni hata Rais alisema akiwa Manyara kwamba watu sasahivi wanataka Barabara tena za lami.

Yaani we Jamaa umeandika vitu rahisi sana ambavyo tayari vina majibu.
 
Hiyo ni agenda iliyotoa mimba (aborted agenda or miscarriage).

EU Commission inajenga mfumo mkubwa wa logistics unaoweza kuhudumia Afrika nzima wakichagua bandari ya Lobito na kujenga EPZ kubwa Zambia Kaskazini na DR Congo Kusini (zitazounganishwa na hiyo bandari) ambao hawa ndiyo wateja wa kimkakati na wa kihistoria wa TPA. Sasa DP World na TPA watafanya kazi gani?

EU Commission inashirikiana na Team Europe, G7 na kwa kuzingatia Paris Agreement.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Sisi tunaenda Mashariki ndiko Kuna biashara

Kwani unadhani China ni Mjinga?
 
Majority ya watanzania na wale hasa wanaopanga mstari kupiga kura wanaguswa na hayo yote kweli? Pengine pembejeo tu,mengine wanaona yana ahueni. Walau vituo vya afya,barabara na mashule yameboreshwa.
 
Hiyo ni agenda iliyotoa mimba (aborted agenda or miscarriage).

EU Commission inajenga mfumo mkubwa wa logistics unaoweza kuhudumia Afrika nzima wakichagua bandari ya Lobito na kujenga EPZ kubwa Zambia Kaskazini na DR Congo Kusini (zitazounganishwa na hiyo bandari) ambao hawa ndiyo wateja wa kimkakati na wa kihistoria wa TPA. Sasa DP World na TPA watafanya kazi gani?

EU Commission inashirikiana na Team Europe, G7 na kwa kuzingatia Paris Agreement.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app

1. Bandari ya Lobito ya Angola iko ktk bahari ya Atlantic na sio mshindani wa bandari ya Dsm.

2. Dp W wameahidi kuwekeza usd 250 mil na kuchukua 40% ya mapato. Uwekezaji huo ni kidogo sana kuhalalisha mgao huo. Watz tungeweza kuwekeza wenyewe na kujipatia 100% ya mapato.
 
Majority ya watanzania na wale hasa wanaopanga mstari kupiga kura wanaguswa na hayo yote kweli? Pengine pembejeo tu,mengine wanaona yana ahueni. Walau vituo vya afya,barabara na mashule yameboreshwa.
Hiyo Bima ya Afya kwa wote ni kitanzi kuliko Pembejeo. Jinsi ilivyotengenezwa itakuja kuwa kama mikopo ya elimu ya juu ambapo; maskini ndiyo wataambiwa walipe alafu fungu walilotengewa kulipiwa maskini litatumika kulipia matajiri na wenye uwezo wa kujilipia. Huu unabii utaukumbuka utapotimia, vuta subira.

Bima hii maskini akiishabaguliwa, kama ilivyokuwa kodi ya kichwa ya maendeleo, watu (maskini) watakimbilia porini kujificha wasikamatwe kwa sababu sheria yake imeifanya kuwa lazima kwa kila mtu.

Iile bundle la Toto Afya lilikuwa 50,000/ sasa limefutwa na kuwa 350,000/, ebu fikiria baba yako kule Kijijini ana wake 5 kila mke mmoja ana watoto wadogo 3 jumla 15 mara 350,000/ = 5,250,000/ ÷ kwa 200,000/ bei ya ng'ombe mdogo basi babako kwa mwaka atatakiwa kuuza ng'ombe 26 kulipia Bima ya watoto tu (bado tegemezi wake wakubwa) ambayo hii ni kununua umaskini kwa sababu kila mwaka atakuwa anauza ng'ombe 26 kulipia Bima ya Afya ya watoto tu, huku wewe pia ulisomea mkopo wa serikali bado unapambana kulipa (makato makubwa) na unatakiwa ukatwe na Bima ya Afya pia.

Baba yako anakutazama umsaidie na wewe unamtazama akusaidie, mnatazamana.

Kwanini usiamini Bima ya Afya ni kitanzi kwa CCM kuliko hata pembejeo?

Kwanini usiamini kwamba ili CCM iwe salama 2025 (isilazimike kucheza rafu kwenye masanduku ya kura) ingesubiri uchaguzi upite salama kwanza ndiyo serikali yake ije na Bima ya Afya? Vinginevyo CCM itapata ushindi wa machozi maana serikali yake itakuwa imeleta zimwi (Bima ya Afya) kukusanyia ela za chaguzi.

Kubuni jambo na kuparamia kulitekeleza ni rahisi sana maana inahitaji tu makofi ya Wabunge, lakini kulitekeleza kwa uzoefu wa historia ya Tz ni majuto tupu, ni msiba mkuu, ni kufukuza utajiri mdogo wa wananchi na kukaribisha umaskini mkubwa kwao (unabadilisha umaskini kwa utajiri kama watani zangu Wakwere wanaouza nanasi kununua mua).

Asante sana kwa ufafanuzi huu kuhusu Bima ya Afya. Naomba nitulie nisome na nifanye tathmini ya kisiasa ya hili,nitarudi na maoni yangu.
 
Kwa yote hayo hapo Juu sijaona hata Moja ambalo Lina mkwamo, pengine umekariri huelewi hata shida kubwa za Wananchi ni zipi.

Mfano unataka tozo,zipi hizo maana tozo zilishafutwa au wewe unaijua tozo ipi hiyo ambayo watu Wanalalamika?

Bima ya Afya ndio kwanza Inaanza,itakuwa effective 2027

Bei ya mafuta imefanyaje? Tanzania ndio tuna bei nafuu kuliko wote.

Tanesco wamefanyaje wakati bwawa litakuwa tayari na grid itakuwa imefika Kigoma na Katavi,umeme Vijiji vyote na Sasa ni Kusambaza Vitongojini

Hakuna mstaafu anaechukua hata miezi 3 bila mafao Kwa Sasa sana sana labda kama unasema waobgezewe malipo ya Kila mwezi

Vijana hawajawahi kuwa na mikopo Yao ,walikuwemo kwenye 10% ya Halmashauri ambayo Serikali inatengeneza utaratibu mzuri maana ule wa awamu watu wamepiga zaidi ya Bil.92 za Bure

NIDA imefanyaje wakati Kwa sasa vitambulisho vimeanza kugawiwa na Hadi Desemba 2024 Kila mtu atakuwa na Kitambulisho.

Pembejeo zimefanyaje Mzee wakati Mwaka wa 3 huu Rais anatoa ruzuku ya Mbolea?

Hiyo kikokotoo inaweza futws ila sijasikia jibu la Serikali.

Changamoto ya Wananchi Kwa Sasa ni Barabara ndio ziliibuliwa bungeni hata Rais alisema akiwa Manyara kwamba watu sasahivi wanataka Barabara tena za lami.

Yaani we Jamaa umeandika vitu rahisi sana ambavyo tayari vina majibu.
The dread of criticism is the death of genius (William Gilmore Simms).

Back
Top Bottom