Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,561
- 21,535
Habari wakuu,
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Tokea vita hiyo ya Hamas na Israel imeibua mijadala na maneno makali kati ya watu. Ajabu wanaoibua mijadala hii ni Waislamu na Wakristo kila mmoja anatetea dini yake.
Hapa kuna wanaotoa maneno ya busara hasa wale watumishi wa Mungu. Kwa pande zote mbili, yaani Waislamu na Wakristo. Ila kuna wale wafia dini ambao wao waonyesha hasira za kibinadamu.
Wamefikia hatua ya kurushiana maneno makali kwenye mijadala mitandaoni kama hapa JF ndio nashinda sana. Hii inaonyesha kuwa watu Bado wana Imani haba na Mungu.
Hasa wakristo ndio wameonesha kuwa Imani yao ipo chini. Nasema zaidi na wakristo maana wao wanajua historia ya Israel. Wanajua ni Taifa teule linalopiganiwa na Mungu na Mungu aliwachagua wao, na wanajua Mungu wao hajawahi kushindwa ila wanatukanana..
Badala ya kuomba vita viishe watu wake wakae kwa amani wao wanaanzisha vita ya maneno na chuki za kidini.
Nashangazwa sana na hii hali ya kufia Dini.