Vita ni vita tu, Haichagui aina ya Silaha au Mbinu, Lengo ni kumuondoa adui awe Raia au Mwanasiasa

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Ndani ya ccm na hata huko upinzani kumetawaliwa na vita tu, Watu wengi ambao sio wanachama wa vyama hivi vya siasa huona vita wakati wa kura za maoni na uchaguzi tu. Kiuhalisia vita inatokota wakati wote usipokuwa makini unaangushiwa jumba bovu

Hakuna mwana CCM au wa upinzani anayeridhika jina lake kukatwa au kuenguliwa na watu wanaojiita kamati kuu ya ccm au kamati kuu ya Chadema, Act wakati alishinda kura za maoni

Nashangaa kuona wakati wa vita wanajitokeza watu kushauri aina za mbinu za kumdhoofisha adui

Kuna watu wanasema aachiwe huru bila masharti yeyote na kuna Wengine wanasema amekosa kitu gani abaki huko huko ndani mpaka pale wazungu watakapotoa ripoti kama ile inayosema Tanzania ni nchi maskini, choka mbaya, hoe hae na imeelemewa na madeni na Umaskini uliotopea kama Ethiopia na Eritrea

Tangu lini watu wakapangiana silaha za kutumia katikati ya vita ambavyo havijulikana lengo lake na mwisho wake

Ndani ya ccm watu kutumia fimbo kuchapana wakati wa uchaguzi ni jambo la kawaida, Na hata Wengine huchapana kwa njia za giza kwa kutumia masangoma na mambo ya giza ni muendelezo wa kila siku

Vita ni vita tu hakuna kuchagua silaha na kupangiana mbinu, Kuna wakati pesa imetumika kama fimbo za kuchapia na kumdhoofisha adui kwa kuhonga wajumbe na kukodi watu wa Kuandika na kuchafuana, Hizi kamati hujulikana kama Kamati za fitina na majungu na zina Mwenyekiti, Katibu na mtunza hazina

Ni ngumu sana kuingilia vita usiyoijua Chanzo chake, Chimbuko, uhalisia na muanzilishi wa vita husika,

Marekani ni Taifa kubwa sana lenye silaha na nguvu za kila aina kutafuta adui duniani, Lakini kuna wakati ameamua kuondoka Afghanistan na Iraq sio kwa kupenda au kulazimisha bali baada ya mbinu kushindwa , hasara ya kupoteza wanajeshi, Na kuongezeka kwa wanajeshi wazawa wasaliti wa nchi husika aliowafunza mmerekani mwenyewe

Tambua vita hudumu kwa wakati mrefu kama adui hajulikani vizuri au kama adui anatumia Raia kama ngao ya kumkinga au anaanzisha mashambulizi katikati ya Makazi ya Raia wema na wasiokuwa na hatia

Kuna mifano mingi ya vita imekwisha tokea ndani ya vyama vya siasa na Wengine walisalimu amri na kuna Wengine mpaka Leo wamegoma kuomba msamaha au kusalimu amri

Vita ya Humprey Polepole na hao wahuni

Vita ya Bernard Membe na Bashiru and the Company

Vita ya Zito Kabwe and the company VS Chadema

Vita ya Tundu lissu na Marehamu JPM

Vita ya kambi ya lowasa na kambi ya Membe na JK

Vita ya Job Ndugai na Yule kada aliyepigwa Rungu

Vita ya Makamba Yusufu, Kinana you VS Bashiru and the company

Vita ya Nape Nnauye, Makamba January, Membe VS JPM

Vita ya Sofia Simba, Emanuel Nchimbi Vs Kambi ya JPM

Wakati wa vita hakuna kupangiana silaha za kumteketeza adui, Vita haina urafiki,Katikati ya vita hakuna mawasiliano wala majadiliano. Majadiliano hufanyika kabla ya vita au baada ya vita mmoja anapoamua kusalimu amri

Aachiwe huru au asiachiwe huru inategemea lengo la vita kama muanzilishi anafahamu nguvu ya adui au haifahamu, Na hata kama anafahamu nguvu ya adui itategemea uwezo wake wa kuhifadhi silaha na kuzitumia vizuri, Huwezi endesha vita kwa Fedha za mikopo na misaada muda wowote mikopo na misaada ikikata utasababisha maafa makubwa kwa Raia na wapiganaji wanaokuunga mkono
 
Wakati mwingine vita huwa ngumu kama aliyeianzisha alikosea mbinu na akataka kurekebisha mbinu katikati ya mapambano. Wapiganaji wake wanapoanza minong'ono ya kutoridhika na mbinu za kamanda wao huamua kupambana kulingana na hali ya uwanja wa mapambano ilivyo.
Lakini pia gharama ya kuwahudumia askari walioko vitani lazima iongezeke sambamba na muda unavyoenda hasa vita inapokuwa ngumu.
 
Wakati mwingine vita huwa ngumu kama aliyeianzisha alikosea mbinu na akataka kurekebisha mbinu katikati ya mapambano. Wapiganaji wake wanapoanza minong'ono ya kutoridhika na mbinu za kamanda wao huamua kupambana kulingana na hali ya uwanja wa mapambano ilivyo.
Lakini pia gharama ya kuwahudumia askari walioko vitani lazima iongezeke sambamba na muda unavyoenda hasa vita inapokuwa ngumu.
Tatizo majeraha yanayoachwa baada ya vita kwa ndugu, Jamaa na marafiki

Unayaziba vipi majeraha
 
mbowe angekuwa nje tanzania isingeitwa masikini kulinganishwa na nchi zenye vita ebu tusubili lingine kutoka kwa wazungu
 
Bahati mbaya vita nyingi kati ya hizo huwa ni kwa maslahi binafsi ya wanasiasa na sio kumkomboa mtanzania.

Vita ya Lissu na JPM pekee ndio vita iliyokuwa na maslahi mapana kwa wengi.
 
Bahati mbaya vita nyingi kati ya hizo huwa ni kwa maslahi binafsi ya wanasiasa na sio kumkomboa mtanzania.

Vita ya Lissu na JPM pekee ndio vita iliyokuwa na maslahi mapana kwa wengi.
Na vita ya Ndugai
 
Back
Top Bottom