“Vita kuu Tanzania, ni Vita kali kati ya watetezi wa haki na watetezi wa dhuluma”

Aug 31, 2011
35
27
NI UTABIRI WANGU.
“Vita kuu Tanzania, ni Vita kali kati ya watetezi wa haki na watetezi wa dhuluma”

Mateso tunayoyapata, vipigo na kutekwa kwa watetezi wa haki, mabomu, risasi tunazopigwa, uonezi, unyanyaswaji, shutuma tulizokwisha pata, magerezani tulimo pitishwa, dhuluma tulizofanyiwa, sote tuliofukuzwa vyuo vikuu nchini, ni catalyst ya kuongeza hasira ya mabadiliko, ni nyenzo tosha za mapinduzi ya taifa lolote lile duniani.

Mwisho utawala wa mabavu ni ishara ya kuanguka kwa utawala wa dhuluma na kuchipuka utawala wa haki.

Nasema haya kwa sababu, dalili za mvua ni mawingu, na mabadiliko ni dalili ya mapinduzi ya kifikra, ni ishara ya kuwa wimbi zito la mabadiliko na mapinduzi limewasili Tanzania. Ifahamike kuwa kadri siku zinavyoendelea kuna vita kuu nchini Tanzania inayozidi kuchukua sura mpya, vita hii ni baina ya makundi mawili makuu “watetezi wa haki na watetezi wa dhuluma” NDANI YA TANZANIA YETU.

Ni dhahiri kuwa anapoteswa, anapopigwa, anapouwawa mtetezi wa wanyonge, ni kuteswa, kupigwa, na kuuwawa kwa wananchi waliowengi, si dalili njema sana kwa sababu wanyonge silaha yao ni moja. Umoja na mapambano. Wakiungana wanyonge ni zaidi ya mabomu na nguvu za vyombo vya dola.

Niongelee tu sauala ambalo limenifanya niandike taarifa hii. Historia inaonyesha kuwa kulikuwa na kuna matumizi makubwa sana ya nguvu za vyombo vya dola ndani ya vyuo vikuu nchini, sasa ajabu mara kadhaa tumeona dalili hizi zimeanza bungeni. Baadhi ya Wanaoliongoza bunge wamekuwa vipofu wa haki. Wamekuwa na sheria na kanuni za bunge zinazo kata upande mmoja, ni hatari sana ndugu zangu.

Umefika wakati wa watanzania tunaojitambua kufikiri beyond our political ideologies, tufikiri zaidi utanzania kwanza na itikadi za vyama vyetu baadaee.

Bunge haliwatendei haki watanzania kwa sababu tu ya mvutano wa kiitikadi, na kiti kukosa busara za kuongoza huku chenyewe kikiona kipo sahihi. Wamevaa miwani ya mbao na wamekuwa sikio la kufa.

Bila kujali itikadi za vyama vyetu. Tufahamu tu kwamba tuendako siko sahihi

RAI YANGU.

Wasomi wa vyuo vikuu, ni muda muafaka wa kutengeneza BUNGE LA WASOMI” YANAYOSHINDIKANA BUNGENI KWA SABABU YA MVUTANO WA KIITIKADI, bunge la wasomi liamue kwa niaba ya watanzania.

Nasema haya kwa sababu wasomi kwa sasa tumelala, tumetishwa na tumekubali kutishika, silence is a betrayal wasomi. REVOLUTION SQUARE ndani ya vyuo vyetu si mahala pa itikadi, jikusanyeni, jadilini mijadala inayohusu taifa hili amueni kwa niaba ya wavujajasho wa taifa hili.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, niwaambieni kitu, wanaowanyima uhuru wa kukutana hawana mamlaka hata kama wao ni maprofesa, wanaenda kinyume cha katiba ya nchii hii na naombeni mkasome DAR ES SALAAM DECLERATION OF ACADEMIC FREEDOM la mwaka 1990. just GOOGLE. Utatambua hakuna mtawala mwenye taaluma yoyote anaweza kuwazua kukutana na kujadili mambo yenu.

Rudini kwenye misingi ya UTaifa zaidi kuliko itikadi za vyama vyetu kwanza, ogopeni KUOGOPAhofu woga na shaka, aminini na napoleon mtawala jemedari wa vita aliyetawala Ufaransa amabeYE alikiri kuwa UKWELI UNANGUVU NA NI ZAIDI YA UPANGA. Wasomi ni wakati wa kulipigania Taifa. Kumekucha katika mapambano.

NI NDOTO YANGU KWAMBA MABADILIKO NCHI HII YATALETWANA WASOMI, TUSITEGEMEE WANASIASA KULIKOMBOA TAIFA, TUAMINI SISI WASOMI TUKISIMAMA NA UTANZANIA KWANZA ITIKADI BAADAE, TUTALIKOMBOA TAIFA
TOGETHER WE CAN
TRUTH IS POWER
GOD IS OUR LEADER
AND CHANGE IS OUR MISSION.
W.TOGETHER@YAHOO.COM
 
Mungu akubariki mkuu kwa kuyaona na kuyajua hayo,sisi tupo nyuma yenu kwa maombi na dua.
 
Ccm ni watetezi wa dhuluma chadema ni watetezi wa haki

Uko sahihi kijana wangu,Lakini sasa mbona mnabagua ktk utetezi wenu.kuja jamii moja ikidhulumiwa nahao hao gamba hamuandamani kutetea hakizao mpo kimyaaaa,au ndo mnasapoti.Madakti,waalimu,mfumuko wabei,nyamongo etc mliandamana.lakini dhulma ya NECTA, Kufukuzwa wanafunzi Ndanda yote kimyaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.Mmmmh.
 
comrade "Tunduru boy". binafsi sijaongelea gamba. nimeongelea vita baina ya watetezi wa haki na watetezi wa dhuluma bila kujali gamba la chama chochote. haki haichagui gamba. lakini pia nimeongelea matumizi ya nguvu za vyombo vya dola hata bungeni baada ya historia kuonyesha kuwa nguvu ya vyombo vya dola ilikuwa imekithiri sana vyuo vikuu nchini.

msingi wangu mkuu, sisi kama watanzania haswa vijana. umefika wakati wa kuishi beyond our political part ideologies. tusiwe washabiki ndaki ndaki wa itikadi za vyama vyetu hata kama vyama vyetu havilitendei haki taifa letu. bunge letu limeshatafunwa na ushabiki ndakindaki wa kiitikadi.masuala mazuri yenye maslahi na wavujajasho wa taifa letu hayapiti bungeni sababu ya mvutano wa kiitikadi. baadhi ya wabunge wa vyama vyetu hawajawa liberal. endapo hoja imetolewa na mbunge wa chama fulani, wabunge wa vyama vingine wanashindwa kumuunga mkono kwa sababu tu eti ya kuona watampa umaarufu. huu ni upumbavu ambao hautakiwi kuvumiliwa. mtu analeta hoja inayogusa uchumi wa watanzania. wabunge ulimbukeni wanaanza kujihami nani katoa hoja, kwa nini tusiwe chama chetu. wanashindwa kuunga mkono hoja kwa sababu ya upumbavu wa ushabiki ndaki ndaki wa itikadi. binafsi nachoshwa sana na muenendo wa bunge. sijui wew comrade unaonaje...
emekha.
 
nashukuruni sana wadau kwa comment zenu. but ni vyema tuyaishi tunayoyaona yanamsingi katika taifa letu.
kwa sasa Tanzania yetu inakosa dira sahihi kwa sababu wakati wa wavujajasho kuamua hatma ya nchi yao haujafika lakini naamini tupo kwenye danger zone. danger zone kwa sababu wahuni wachache hawajashtuka kuwa wavujajasho kwa sasa tumejitambua, na tupotayari kupambana. wametumia nguvu za vyombo vya dola kwa mda mrefu, sasa wameanza kuzima think tank ya bunge. ni hatari kwa taifa. hili halinaitikadi ya chama chochote ila lina utanzania kwanza.

msingi mkuu wa hoja yangu, sisi kama watanzania haswa vijana. umefika wakati wa kuishi beyond our political part ideologies. tusiwe washabiki ndaki ndaki wa itikadi za vyama vyetu hata kama vyama vyetu havilitendei haki taifa letu. bunge letu limeshatafunwa na ushabiki ndakindaki wa kiitikadi.masuala mazuri yenye maslahi na wavujajasho wa taifa letu hayapiti bungeni sababu ya mvutano wa kiitikadi. baadhi ya wabunge wa vyama vyetu hawajawa liberal. endapo hoja imetolewa na mbunge wa chama fulani, wabunge wa vyama vingine wanashindwa kumuunga mkono kwa sababu tu eti ya kuona watampa umaarufu. huu ni upumbavu ambao hautakiwi kuvumiliwa. mtu analeta hoja inayogusa uchumi wa watanzania. wabunge ulimbukeni wanaanza kujihami nani katoa hoja, kwa nini tusiwe chama chetu. wanashindwa kuunga mkono hoja kwa sababu ya upumbavu wa ushabiki ndaki ndaki wa itikadi. binafsi nachoshwa sana na muenendo wa bunge. sijui wew comrade unaonaje...
emekha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom