Mtu wa Asali
Senior Member
- May 9, 2022
- 152
- 291
Kuna kitu huwa najiuliza wakati wote kuwa sisi Tanzania kipindi cha 2015-2021 pale Mungu alipo amua ugomvi tuliaminishwa kuwa kuna vita ya kiuchumi!
Huu ulikuwa ni uongo na uzandiki wa wazi kabisa. Tanzania hatukuwa na vikwazo vyovyote vya kiuchumi bali tulikuwa na vikwazo vya kisheria kutokana na kuvunja mikataba kiholela na wawekezaji.
Magufuli alituaminisha kuna vita ya kiuchumi si kweli tulikuwa na mkwamo wa kidiplomasia, nchi iliendeshwa kama familia palipokuwa na migogoro haikusuluhishwa kwa maslahi ya nchi bali iliamuliwa kibabe. Sakata la kuchoma vifaranga, sakata la kuwauwa wavuvi wa nchi jirani.
Ukitazama haya mambo yote Magufuli hakuwa anajali hata kidogo ni mtu katili ambaye alithubutu kula hata rambirambi za wahanga wa tetemeko pale Kagera.
Nchi hii ilikosa mfariji kabisa, Nchi iliendeshwa kwa akili ya Rais anavyotaka Task force ziliwafilisi watoto wa kitanzania waliowekeza kwenye Bureau waliingia kwenye umaskini mkubwa.
Magufuli hakujua diplomasia hakujua Mahusiano mazuri yanavyojenga na kukuza uchumi. Hakujua Sadam Hussein kuwa ni Rais wa Iraq.
Namnukuu “Rais wa Libya sadam husein hapana wa Libya gadafi, Sadam husein wa Kuwait.” Tangu siku hii nilifahamu kidiplomasia tunaingia kwenye tope.
Licha ya kuboronga kidiplomasia hata ndani alishindwa kujenga Mahusiano na wawekezaji wazawa aliwachukia walikuwa maadui mfanyabiashara Vicent Lasway mmiliki wa Kibo Palace hadi leo yupo taabani kiuchumi, alikwapua kila kitu jamaa ameisha.
Mfanyabiashara Mohamed Dewji alikamatwa na kutekwa kwenye hotel ya kifahari na Watekaji walikaa naye zaidi ya siku sita.
Msanii Roma mkatoliki alitekwa siku ya tatu akapatikana ununio na majeraha kibao. Serikali yake ilikuwa katili kwa Vijana wa kitanzania.
Mwandishi Kabendera hadi mama yake mzazi alifariki Dunia kwa kesi ya mchongo chini ya serikali ya Magufuli kosa lake kuandika Habari kwenye magazeti ya mabepari juu ya serikali suala lile lilimchukiza Rais. Kabendera akatupwa Jela.
Tajiri Yusuph Manji alinyang’anywa kampuni ya Tigo aliyoinunua kihalali kwenye soko la hisa kijana mdogo, Paul Makonda alimsweka ndani wiki hadi Manji kukimbia nchi.
Watoto wa kitanzania waliotafuta kwa jasho walichukiwa ndani ya ardhi ya kwao wakalazimishwa kuishi kama mashetani wakateswa kwa kudra walizojaliwa na Mungu kuwa matajiri kwa kiongozi aliyejinasibu ni Mcha Mungu.
Baba Askofu Severine Niwemugizi alipo unyanyua mdomo katika baraza la maaskofu alitishiwa siyo Raia.
Askofu kakobe alipounyanyua mdomo wake juu dhidi ya serikali, TRA walibisha hodi Kanisani. Baba Askofu aliufyata hadi kukimbia uhamishoni South Africa.
Aliwaumiza wale waliojaliwa kudra za Mwenyezi Mungu aliwanyonga kwa siri wale waliomsema pembeni.
Mfanyabiashara mmoja kule Kanda ya Kaskazini mmiliki wa Kerai Construction hadi leo anajiuliza Rais yule alikuwa Mtanzania au tulimwazima toka nchi Jirani sababu matendo aliyoyafanya yalikuwa kinyume na sisi watanzania wenyewe tulivyo. Kosa lake ni kumfadhili mgombea wa Urais Mwaka 2015.
Alikwiba, akadhulumu akatapanya mali kwa mahawara akapenda sifa kuliko kiumbe mwanamke akataka atukuzwe akagawa vyeo kama njugu kwa vibinti vidogo umri wa watoto wake ilibakia kuitwa Mtakatifu Jiwe.
Aliuza nyumba za serikali baadaye alizinyang’anya rejea sakata la mwanaume wa mkoa wa Tarime yule anaitwa Zakaria alitupwa Jela. Kuna mzee alinyang’anywa nyumba aliyonunua kihalali pale Ilala alilazimishwa kusarenda nyumba ile au atupwe Jela chini ya mtutu wa bunduki.
Hivi ndivyo vita vya Kiuchumi hewa vya Mhe. Mungu kwa sauti ya Profesa Majalala.
Legacy ya Magufuli ndiyo hii daima tutamkumbuka kwa vituko vyake.