KERO Vispika vya matangazo vimekuwa kero kubwa kwenye masoko, mamlaka ipige marufuku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kaka mimi kwa mtizamo wangu nadhani pia ni nchi zote kama sio dunia nzima, ustaarabu unaendana na kipato huwezi kuishi uswahilini ukataka ustaarabu ukaeleweka

Kama una kipato cha ustaarabu usirudie tena kwenda huko karume kwenye makekele, nenda maduka makubwa makubwa

Huko Karume waichie hao ambao sio wastaarabu
 
Kaka mimi kwa mtizamo wangu nadhani pia ni nchi zote kama sio dunia nzima, ustaarabu unaendana na kipato huwezi kuishi uswahilini ukataka ustaarabu ukaeleweka

Kama una kipato cha ustaarabu usirudie tena kwenda huko karume kwenye makekele, nenda maduka makubwa makubwa

Huko Karume waichie hao ambao sio wastaarabu
Tunaweza kuweka mifumo ya kujiendesha kistaarabu sehemu nyingi.

Tunaweza ku plan mambo yawe ya kistaarabu hata sehemu za watu wa hali ya chini.

Kwa kweli, huko ndiko tulikotokea.

Dar es salaam ulikuwa ni mji wa kistaarabu. Kuna vijana tukiwahadithia kuwa mji ulikuwa na umeme, maji, mabasi ya usafiri wa umma mpaka ya Icarus Kumbakumba, huduma za kuzoa takataka angalau mara moja za Halmashauri ya Jiji, mpaka miaka ya mwanzo ya 1980s, watu wanaona kama hadithi za kubuni.

Ni vigumu sana kuwa na ustaarabu kama kuna mfumuko mkubwa wa idadi ya watu, watu hawana kazi, wenye kazi kazi nyingi ni za "disguised unemployment" kama hizo za umachinga.

Ni vigumu sana kuwa nanustaarabu katika jamii yenye watu wenye njaa, njaa inaondoa ustaarabu. Hapo Karume hata kama mtu kalelewa kwa misingi ya heshima na kutoshikashika watu huko kijijini kwao, akija mjini na kuona ushindaninwa kibiashara ndiyo unamtaka afanye hivyo ili kufanikiwa, atafanya hivyo tu.

Njaa haina ustaarabu.

Ukitaka ustaarabu, tengeneza uchumi vizuri uondoe njaa kwanza.

Sisi tulijitahidi kuendeleza ustaarabu hata kwenye njaa ya miaka ya 1980- 1985, tukapanga foleni kwenye maduka ya kaya kununua chakula, tukisaidiwa sana na idadi ya watu kuwa ndogo. Ni vigumu sana kukosa ustaarabu kama ukiangalia kushoto unamuona mtu mnayesoma naye, ukiangalia kulia unamuona mtu mnayesali naye.

Sasa hivi, kuna njaa halafu kuna massive rural urban migration, vijana wanatoka vijijini mwao, wanakuja mijini hawamjui yeyote, wana njaa katika mji mkubwa ambao hawamjui mtu, hapo ustaarabu ni kitu cha mwisho kabisa katika mawazo yao.
 
Wana tabia pia ya kushika wateja kuwalazimisha waende wanapotaka wao
As if wewe hujui unakoenda ๐Ÿ˜†

Hii tabia sijui wameacha? Sijafika karume miaka minne hii
Bado ipo. Yaani mtu anakudaka toka huku barabarani kabisa. Wengine tunapenda tuwe na uhuru wa kuingia tunapotaka. Tukitaka msaada tutauliza.
 
Ndugu Hilo swali najiuliza pia... Je wanalala vizuri? Haina athari kwa afya?
Katika miaka 20 ijayo, Dar itakua kwa idadi ya watu kutoka milioni 7 ya sasa mpaka takriban milioni 14.

Hilo ni ongezeko la 100%, doubling.

Ongezeko la miundombinu kama sehemu za kulala ni dogo sana, kama halipo kabisa.

Mpaka sasa, watu wanalala vibaya sana, na hali itazidi kuwa mbaya maradufu.

Inabidi serikali na watu wajipange sana kukabiliana na matatizo kama magonjwa ya kuambukiza, vinginevyo kutakuwa na majanga sana.
 
Juzi niliamua kuingia soko la mitumba Karume kwa mara ya kwanza. Kweli ni sehemu nzuri ya kupata nguo nzuri za mitumba. Ila kuna kero moja isiyovumilika kwa watu tunaopenda ustaarabu.

Kila mfanyabiashara ana spika kwahiyo kelele za pale zimekuwa ni kero kubwa sijui wenyewe wanaonaje ila kwangu palinishinda. Yaani hizi spika ni kero sana.

NEMC WAZIPIGE MARUFUKU NI UCHAFUZI WA MAZINGIRA

noise polution. Ila usitegemee wapige marufuku maana wanaogopa mwaka huu na ujao ni uchaguzi. Labda BAADA. Tegemea mambo ya hovyo hovyo kuzuka na kuongezeka kipindi hiki na hakuna atakayekemea.
 
Hiyo ni kweli pamoja na hilo kuna haya maspika yanakaa sana kwenye vituo vya daladala sehem mbalimbali hawa WAUZA VIWANJA haw jamaa wanakera sana na yale maspika ni kerooo
 
Ndio boss
Karume napapenda lakini hiyo tabia ya kushikana na 'kulazimisha' niende wanakotaka wao siipendi
Wadada ni wahanga wakubwa wa hii kadhia, ukikubali kushikwa mkono jiandae kupapaswa, kuna vijana hawana ustaarabu kabisa.

Wanaume wanaangalia wa kuwashika, sisi wengine ni ngumi mkononi.
 
Kariakoo mitaa wanapouza vifaa vya ujenzi na umeme angalau hakuna purukushani sana
Ila kuna mitaa wanayouza nguo za wanawake kwenye meza etc aisee hatari sana wauzaji wanaimba wanapiga makofi sijui ndio mtindo gani huo wa kufanya biashara
 
Wadada ni wahanga wakubwa wa hii kadhia, ukikubali kushikwa mkono jiandae kupapaswa, kuna vijana hawana ustaarabu kabisa.

Wanaume wanaangalia wa kuwashika, sisi wengine ni ngumi mkononi.

Aah! Hiyo kupapaswa wamezidi sasa
Mimi nilikuwa naona wanashika mkono huku wakifosi kukupeleka sehemu wanakodai kuna nguo nzuri
 
Back
Top Bottom