Vipo viashiria vya utakatishaji fedha, upo wizi; kuna kufeli kwa wizara lakini ipo hofu ya kusumbua wapiga kura. Tufanyeje nini tuwe salama kiuchumi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
890
4,140
Hali ya uchumi kidogo siyo nzuri, miradi mikubwa imesimama na baadhi imeenda beyond time kwa sababu hakuna fedha.

Speed ya ujenzi wa miundombinu mfano barabara imeshuka sana; mfano taarifa zinasema barabara ya kimara to kibaha mkandarasi ameondoka site na kuacha mawe barabarani huku maeneo mengi yakiwa yamesitishwa kukamilika kwa kukosekana fedha.

SGR imekwama kwa sababu ya flow ya fedha kutopendana na mahitaji hivyo wafanyakazi wameacha au kuachishwa kazi. Awali wataalam walishauri ikamilike Sehemu moja ianze kazi ila watawala wakaziba masikio na sasa Mradi imegawanywa kwenye vipande vipande ila hakuna consistency baina ya lot moja na nyingine

Miradi ya taasisi moja moja nayo imekwama. Mfano Mradi wa ujenzi wa shule na vyumba vya madarasa siyo tena agenda masikioni mwa wananchi kwa sababu waliopo wizarani walidhani makosa ni ya wakurugenzi ila finally wamekubali bila fedha wataishia kutumbua viongozi wa halmashauri bila hatia.

Kwenye eneo la mikopo, kuna tatizo kubwa zaidi ya tunavyoliona. Inaelezwa kwamba mfumo wa kutegemea kukopa umepelekea kushuka kwa udhibiti wa makusanyo ya ndani.

Wizara ya fedha imewekeza zaidi kwenye mikopo kuliko kuwekeza nguvu kuongeza mikopo. Sababu zinazotajwa kupelekea kushuka kwa udhibiti wa mapato ya ndani ni hizi zifuatazo.
1. Mfumo wa rushwa unaoongozwa na viongozi wa umma umepelekea Rais kutoambiwa ukweli pale mianya inapobainika.

2. Watumishi wa umma na wanasiasa wamefungua biashara kwa kasi; mfano biashara ya magari kila siku zinafunguliwa yard mpya kila mkoa ila magari mengi kwenye hizi yard yameingizwa kama transit au yameingizwa kinyume cha taratibu. Kwa sababu wamiliki ni watoto wa wanasiasa na ndugu zao hakuna mikakati ya kudhibiti hii hali

3. Tunakopesheka. Hii kauli imetufanya tuzidi kuwaza kukopa kuliko kuwekeza zaidi kulipa mikopo.

4. Hofu kwamba tukiwekeza kukusanya kodi tutawakwaza wapiga kura na kujenga chuki. Hakuna mwanasiasa anayethubutu kuweka nguvu kukusanya kodi mtaani kwa sababu wameaminishwa wananchi watawachukia zaidi.

Nini kinapangwa kufanyika, kwanza nikubadili mawaziri na viongozi wa baadhi ya taasisi kulete njia mpya ya kufikiri.

Kuona kama mchakato wa kutumia nguvu kudai kodi unaathiri siasa na wapiga kura kupelekea wakusanya kodi kuelekezwa kutotumia nguvu

Tatu, kuendelea kuwasihi wahisani wazidi kutuamini na kutukopesha kwa masharti nafuu au magumu ila tu tufike 2025 salama

Mwisho, nikuwekeza rasilimali zetu kwa mikataba ya muda mrefu kwa mabeberu

Madhara yanayoweza kupatikana nikutengeneza taifa lililofilisika kiuchumi kwa msingi wa tunakopesheka au tusiwakwaze wapiga kura . Lakini pia kiusalama upo uwezekano mkubwa nchi yetu ikapata vikwazo pale itakapothibitika tunahifadhi watakatishaji fedha na wafadhili wa uhalifu Dunia.

Tunakumbuka namna visiwa vya Jersey vilivyotumiwa na wanasiasa wetu.....tufahamu pia kwamba wenye biashara za ukanjanja kama uuzaji wa magari wanaweza kuwa wafadhili wa uhalifu huko Duniani.

Wizara zinazopaswa kuwajibika kuokoa jahazi ni
1. Ofisi ya Rais Tqmisemi na wizara nyingine

2. Wizara ya mambo ya ndani hadhi udhibiti wa wahalifu na wqtakatisha fedha

3. Wizara ya uchukuzi

4. Wizara ya miundombinu- wizara imeshindwa hata kutoa mawe barabara za mwendokasi kweli

5. Wizara ya fedha

6. Wizara ya Mipango
 
Ukiona huku chini kuko shagalabagala tambua huko juu ndo chanzo, ushawahi sikia namna ubadhirifu unavyokemewa na kiongozi mkuu wa nchi?

Ule msemo wa mwl. Nyerere tukimuangalia usoni tujiridhishe huyu anakerwa na rushwa kweli? Simuoni akikerwa

Sasa mtu anarembua et mnakula hadi mnavembewa!

Mkristo huwa anakusanya muislam hutapanya! Chunguza hilo

Huu utawala kwa wafanyabiashara ni mserereko!

Ccm uwezo wa kufikiri umefika mwisho!
 
Umeongea ukweli mtu uchukue maua yako kula kitu hivyo hovyo rais anatapanyq pesa balaa
 
Hali ya uchumi kidogo siyo nzuri, miradi mikubwa imesimama na baadhi imeenda beyond time kwa sababu hakuna fedha.

Speed ya ujenzi wa miundombinu mfano barabara imeshuka sana; mfano taarifa zinasema barabara ya kimara to kibaha mkandarasi ameondoka site na kuacha mawe barabarani huku maeneo mengi yakiwa yamesitishwa kukamilika kwa kukosekana fedha.

SGR imekwama kwa sababu ya flow ya fedha kutopendana na mahitaji hivyo wafanyakazi wameacha au kuachishwa kazi. Awali wataalam walishauri ikamilike Sehemu moja ianze kazi ila watawala wakaziba masikio na sasa Mradi imegawanywa kwenye vipande vipande ila hakuna consistency baina ya lot moja na nyingine

Miradi ya taasisi moja moja nayo imekwama. Mfano Mradi wa ujenzi wa shule na vyumba vya madarasa siyo tena agenda masikioni mwa wananchi kwa sababu waliopo wizarani walidhani makosa ni ya wakurugenzi ila finally wamekubali bila fedha wataishia kutumbua viongozi wa halmashauri bila hatia.

Kwenye eneo la mikopo, kuna tatizo kubwa zaidi ya tunavyoliona. Inaelezwa kwamba mfumo wa kutegemea kukopa umepelekea kushuka kwa udhibiti wa makusanyo ya ndani.

Wizara ya fedha imewekeza zaidi kwenye mikopo kuliko kuwekeza nguvu kuongeza mikopo. Sababu zinazotajwa kupelekea kushuka kwa udhibiti wa mapato ya ndani ni hizi zifuatazo.
1. Mfumo wa rushwa unaoongozwa na viongozi wa umma umepelekea Rais kutoambiwa ukweli pale mianya inapobainika.

2. Watumishi wa umma na wanasiasa wamefungua biashara kwa kasi; mfano biashara ya magari kila siku zinafunguliwa yard mpya kila mkoa ila magari mengi kwenye hizi yard yameingizwa kama transit au yameingizwa kinyume cha taratibu. Kwa sababu wamiliki ni watoto wa wanasiasa na ndugu zao hakuna mikakati ya kudhibiti hii hali

3. Tunakopesheka. Hii kauli imetufanya tuzidi kuwaza kukopa kuliko kuwekeza zaidi kulipa mikopo.

4. Hofu kwamba tukiwekeza kukusanya kodi tutawakwaza wapiga kura na kujenga chuki. Hakuna mwanasiasa anayethubutu kuweka nguvu kukusanya kodi mtaani kwa sababu wameaminishwa wananchi watawachukia zaidi.

Nini kinapangwa kufanyika, kwanza nikubadili mawaziri na viongozi wa baadhi ya taasisi kulete njia mpya ya kufikiri.

Kuona kama mchakato wa kutumia nguvu kudai kodi unaathiri siasa na wapiga kura kupelekea wakusanya kodi kuelekezwa kutotumia nguvu

Tatu, kuendelea kuwasihi wahisani wazidi kutuamini na kutukopesha kwa masharti nafuu au magumu ila tu tufike 2025 salama

Mwisho, nikuwekeza rasilimali zetu kwa mikataba ya muda mrefu kwa mabeberu

Madhara yanayoweza kupatikana nikutengeneza taifa lililofilisika kiuchumi kwa msingi wa tunakopesheka au tusiwakwaze wapiga kura . Lakini pia kiusalama upo uwezekano mkubwa nchi yetu ikapata vikwazo pale itakapothibitika tunahifadhi watakatishaji fedha na wafadhili wa uhalifu Dunia.

Tunakumbuka namna visiwa vya Jersey vilivyotumiwa na wanasiasa wetu.....tufahamu pia kwamba wenye biashara za ukanjanja kama uuzaji wa magari wanaweza kuwa wafadhili wa uhalifu huko Duniani.

Wizara zinazopaswa kuwajibika kuokoa jahazi ni
1. Ofisi ya Rais Tqmisemi na wizara nyingine

2. Wizara ya mambo ya ndani hadhi udhibiti wa wahalifu na wqtakatisha fedha

3. Wizara ya uchukuzi

4. Wizara ya miundombinu- wizara imeshindwa hata kutoa mawe barabara za mwendokasi kweli

5. Wizara ya fedha

6. Wizara ya
"Watanzania mtanikumbuka" kwasasa hakuna Rais, Watanzania watambue hivyo. Kama watadanganywa 2025 watakwisha zaidi. Wale mko na akili wasaidieni wasio kuwa sawasawa kichwani. Kwasasa hakuna Rais Bali ni utapeli tu ndiyo unafanyika. Hebu fikiria mwendo Kasi mbagala not more than 30 km haijaisha mpaka sasa,sgr dar moro ni uongo mpaka basi,meli iliyokuwa inajengwa mwanza ni uongo mpaka basi,ukarabati wa Viwanja vya mpira mikoani ni uongo mpaka basi,bwawa la umeme ni uongo mpaka basi,..huyu anaweza Nini sasa? Bado wewe mwenye akili timamu utamchagua Tena?
 
Back
Top Bottom