Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,919
- 46,662
Kama mkataba wa serikali na DP World utaweka wazi kipengele kwamba mkataba utavunjika endapo DP World watashindwa kuingiza zaidi Trillion 20 kwa mwaka, kuleta ajira 70,000 za Watanzania bandarini na kususha kontena kwa chini ya saa 48. Haya yote yakiwa ndani ya miaka mitano ya kwanza ya uwekezaji wao.
Mkataba wa kwanza uwape DP world bandari tu za Pwani ya bahari.
Bandari za Zanzibar ziingizwe kwenye makubaliano ya uwekezaji wa DP World.
Kodi na tozo za mizigo bandarini zitashuka kwa 30% na kupelekea bei za bidhaa pia kushuka.
Uwekwe ukomo wa miaka 30 na endapo utendaji wa DP World utafikia zaidi ya 80% ya makubaliano ya mkataba wa uwekezaji basi wataongezewa miaka mingine 30.
Ni uhakika serikali ikiweka haya katika mkataba asilimia tisini ya raia wanaopenda uwekezaji wataridhika na kuunga mkono, nafikiri raia wengi wataridhikika na kukubaliana nao kabisa bila kujali vipengele vyake vingine vingi.