Vipaumbele vya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Nimefuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara ya Madini uliofanywa leo 27 April 2023 na Waziri Dotto Biteko Bungeni na nimevutiwa na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na sekta hiyo hasa katika uendelezaji wa sekta unaofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na sera na uongozi thabiti ukuaji wa Sekta ya Madini na mchango wake kwenye Pato la Taifa umeendelea kuimarika. Mchango wa sekta katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017 hadi asilimia 7.2 mwaka 2021. Aidha, katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2022, Sekta ya Madini ilikua kwa asilimia 9.8. Aidha, katika kipindi hicho, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa uliongezeka hadi kufikia asilimia 9.7 ikilinganishwa na asilimia 7.9 kwa kipindi kama hicho mwaka 2021.

Katika ya mengi niliyoyasoma hivi ni vipaumbele vya wizara kwa mwaka ujao wa fedha:
1. Kuimarisha Ukusanyaji wa Maduhuli na Kuongeza Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa
2. Kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati (critical and strategic minerals)
3. Kuwaendeleza na Kusogeza Huduma za Ugani kwa Wachimbaji Wadogo
4. Kuhamasisha Shughuli za Uongezaji Thamani Madini
5. Kuhamasisha Uwekezaji na Biashara katika Sekta ya Madini, Uanzishwaji wa Minada na Maonesho ya Madini ya Vito
6. Kuzijengea Uwezo Taasisi Zilizo Chini ya Wizara ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi

Vipi wadau mnaonaje mwelekeo wa Sekta hii muhimu nchini, kwa mwenye kupenda kusoma bajeti nimeambatanisha chini hapo.









 

Attachments

  • HOTUBA WIZARA YA MADINI 2023-24.pdf
    16.2 MB · Views: 1
Back
Top Bottom