Vip engineering yashinda kesi

mangaukawa

Senior Member
Dec 5, 2014
153
63
Kampuni ya VIP Engineering and Marketing inayoshutumiwa kimakosa kwamba imefanya vitendo vya uvunjifu wa sheria kuhusiana na Akaunti ya Escrow imeibwaga Benki ya Standard Chartered katika shauri lililofunguliwa New York, Marekani. Angalia attachments hapo chini.
 

Attachments

  • Summary Order.pdf
    114.5 KB · Views: 439
  • 2013.09.10 Decision and Order (1).pdf
    205.6 KB · Views: 289
  • 2013.09.24 Second Marrero Order.pdf.pdf
    871 KB · Views: 213
  • 2013.10.04 Third Marrero Order.pdf.pdf
    1.9 MB · Views: 203
Kama swala hili limeanzia tanzania obviously watashinda kwasababu, hawa wapiga dili huwa wanatoa rushwa kuanzia kwa mfagiaji hadi huko juu kabisa kwahiyo kwa mahakamani hutowaweza kwakuwa documents zote zinakuwa zimetengenezwa kwa jinsi wanavyotaka wao , mfano unadhani kwanini baadhi ya wafanyakazi wa tanesco walipewa hela?? Au wa TRA ??
Hawa ni wezi wazoefu serikali ingeanza kudeal na watumishi wao wa umma kwanza rushwa imeota mizizi , kama hadi judge kaingiziwa hela unategemea utakimbilia wapi??
 
Hivi mlitegemea washindwe?? Wakati mpaka majaji wamepewa mgao...eti mchango wa harusi,...haya ni matusi kwa nchi..nani anayeweza mpa rafikiye mchango wa mil 400 kwa ajili ya harus??

Mpaka sasa prof wa anga kashikwa na kigugumizi kutoa tamko..chea bil 5 aliyopewa mke wa kigogo magomeni....
 
Mimi naona kama kesi ilikuwa dismissed! sikuona mshindi kwenye kesi hiyo.
 
Hivi watz tumesahau kuwa takrima kwa ccm ni ruksa na haikufafanua kiwango. Hivyo majaji, maaskofu na wafanyakazi wengine wa umma walipata takrima na hawana kesi ya kujibu juu ya escrow
 
Hivi mlitegemea washindwe?? Wakati mpaka majaji wamepewa mgao...eti mchango wa harusi,...haya ni matusi kwa nchi..nani anayeweza mpa rafikiye mchango wa mil 400 kwa ajili ya harus??

Mpaka sasa prof wa anga kashikwa na kigugumizi kutoa tamko..chea bil 5 aliyopewa mke wa kigogo magomeni....

kesi ni NY sio bongo.
 
Jamani mtu alielewa hii kitu na implication yake atujuze.
  •  Standard Chartered wanadai kuwa wanahisa IPTL.
  •  VIP ilikuwa ina hisa 30% kweye IPTL kama mzalendo, ikaamua kuziuza zote kwa PAP (Kalasinga).
  • Standard Chartered wakasema sio halali kuuza hisa kwa Kalasinga bila mimi ambaye ndio nina-control hisa kutoshirikishwa.
  •  Mahakama ya Tanzania inatambua mauzo hayo na umiliki wa Kalasinga (PAP).
  •  Standard Chartered wakafungua kesi Uingereza, VIP wakafungua kesi Marekani (Kama trick ya kisheria kuonyeshauhalali wa jurisdiction ya Tanzania).
  •  Wakashinda, kuwa jurisdiction ya Tanzania inatosha kwa sababu hata Standard Chartered walikubali kesi zao zisikilizweTanzania halafu baadae wakabadili mawazo.
  •  Standard Chartered wakakata rufaa maamuzi ya mahakama za Marekani.
  • Wameshindwa rufaa (StandardChartered).

IMPLICATIONS

  •  VIP walifungua kesi ya madai kwaStandard Chartered Bank (Hong Kong) wakitaka walipwe ¾ of a billion kwakutuhumiwa vibaya na kupoteza muda kwenye mahaka ya Tanzania, StandardChartered wakakataa wakidai mahakama ya Tanzania haina competence. Kwa maamuzihaya, kesi imeonekana kimataifa kuwa ipo kwenye mikono halali na competent.



  •  Ripoti nya PAC, imetaja kuwepo kuwamauzo ya VIP siyo halali, kwa sababu IPTL inamilikiwa na Standard CharteredBank kama mdeni kutokana na maamuzi ya mahakama ya Uingereza na Cayman Islandsna siyo mahakama ya Tanzania, ambayo Standard Charterd inaikwepa. Uamuzi huukiaina unaifanya PAC na Standard Chartered kuonekana kama walidharau maamuzi yamahakama ya Tanzania, na sasa mahakama ya US imeitambua mahakama ya Tanzaniakuwa competent enough.
I STAND TOBE CORRECTED.
 
Inawezekana kwamba Standard Chartered walikuwa wamelenga kuonesha kwamba mahakama za Tanzania hazitendi haki kutokana na kile walichodai kwamba kuna rushwa kila kona. Kama Mahakama hiyo ya New York ingekubaliana na Standard Chartered basi maana yake ni kwamba hakuna uamuzi wowote wa mahakama za tanzania dhidi ya benki hiyo ungekubalika. Kwa kushindwa katika rufaa (kwa maana ya kesi hiyo ktupiliwa mbali) inamaanisha kwamba uamuzi wa mahakama ya New York uliotolewa mapema kusema kwamba Tanzania ni mahali ambako kesi hizo za Standard Chartered zinaweza kusikilizwa na kuamuliwa unabakia pale pale.
 
Back
Top Bottom