gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 759
- 1,250
Sauti ya watu ni sauti ya Mungu, "Vox populi vox Dei." Nimefurahishwa na tamko la Maaskofu wa kanisa Katoliki juu ya mtanziko huu ulio tupata juu ya kusainiwa kwa makubaliano ya uendeshaji wa bandari kupitia kampuni ya DP-World yaliyotuletea wasiwasi mkubwa juu ya mustakabali wa Taifa letu.
Maaskofu 37 wa Tanzania nzima wamepinga mkataba huo kupitia tamko hilo, jambo la kushangaza zaidi ni kwamba viongozi tulio wapa mamlaka bado wameshupaza shingo na kubaki kimya bila kuongea jambo lolote kana kwamba hawakusikia tamko hilo!
Kwakuwa baadhi ya viongozi hao ni waumini wa kanisa Katoliki akiwemo spika wa bunge Tulia Akson na mkamu wa raisi Dk Philip Mpango, ningependa kulishauri baraza la maaskofu kuwafungia sakramenti viongozi hawa (kuwatenga na kanisa) kwani kwa mujibu wa andiko hilo bila shaka wametenda dhambi kubwa sana iliyowapelekea Watanzania wengi kuingia kwenye mtanziko huu.
Ikiwa watatubu na kurudi kwa kukataa mkataba huu basi wasamehewe na warudishwe kwenye ushirika, ama la wakiendelea kusimamia msimamo wao huo wa kuendelea na mkataba huu basi mamlaka ya kikanisa iwahukumu kutokana na matendo yao, wawe 'Excommunicated!' Naamini kwamba kwa kufanya hivyo italeta funzo na heshima kubwa kwa jamii. Mababa zetu wasiishie kutoa tamko tu waende extra miles kwa kuwachukulia hatua waumini wote walio tufikisha hapa kwa kuwa excommunicate.
Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao ikiwemo kuwazuia kukaa viti vya mbele, na pia wale wasio Wakatoliki wazuiwe kuhudhuria matamasha ya kikanisa wasije wakatumia majukwaa ya kikanisa kuendelea kusambaza propaganda zao kama alivyofanya mstaafu Kikwete huko mkoa wa Mara kwenye tamasha la Wasabato.
Haya ni maoni yangu binafsi.