Viongozi wetu msisubiri mambo yaharibike

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
272
513
Kipindi Musiba anawatukana viongozi mbalimbali, Maaskofu na Mashehe walikula buyu wakakaa kimya.

Muda wa kugeuza kibao kwa Musiba ulipowadia, hao watu walitoka mafichoni na kupaza sauti ya upatanishi. Nini kiliwasukuma kupatanisha muda huo ambacho hakikiwepo kabla?

Viongozi wastafu wapo kimya, viongozi wa dini wapo kimya kuhusu mkataba mbovu wa kuuza bandari zetu Tanganyika.

Ndugu zangu Wabunge wa bunge letu la JMT, Mawaziri na n.k nyakati zaja ambazo nanyi mtaungana na watanzania baki kuugulia maumivu ya maamuzi haya mabovu.. hakika itawatesa sana

Tanganyika tulilogwa na nani? Hivi suala hili lingekuwa upande wa pili hapo Zanzibar Kuna watu wangelifumbia macho? Si viongozi wa dini, Wawakilishi wao bila kujali vyama vyao, waandishi wa habari n.k wangeungana kuitetea ardhi yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom