Viongozi wangu hiki kiwanda cha mbolea na kemikali za petroli kiliishia wapi? Tanzania Mbolea and Petrochemical Company

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,251
Hiki kiwanda cha mbolea na petrochemical kinaonekana kipo Tanzania ukiangalia kwenye page ya wikipidia.

---
Wajerumani kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea Mtwara
Kampuni ya HELM A.G ya nchini Ujerumani imeanza maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea, kitakachojengwa katika kijiji cha Msanga Mkuu wilaya na mkoa wa Mtwara na kugarimu dola za kimarekani bilioni mbili kitakapokamilika.


Mwakilishi wa kampuni ya HELM anayeshughulika na miradi ya uzalishaji bidhaa zinazotokana na taka petrol katika bara la Afrika Mohamed Maatouk, alitoa taarifa hiyo kwenye kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Mtwara na viongozi wengine wa serikali,kilichofanyika katika ukumbi wa boma mjini humo hivi karibuni.


Alisema kiwanda hicho ambacho kitajengwa kwa awamu nne,ujenzi wa awamu ya kwanza unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu na kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.


Kwa mujibu wa bw. Maatouk ujenzi wa awamu ya kwanza ya kiwanda hicho ukikamilika kitatengeneza nafasi 600 za ajira za moja kwa moja,tofauti na miradi mingine mradi huo utamilikiwa kwa ubia kati ya kampuni yake na halmashauri za wilaya katika mkoa huo.


Kulingana na mwakilishi huyo wa kampuni ya HELM amani na utulivu wa kiasiasa wa nchi ya Tanzania na kuwepo mazingira mazuri ya uwekezaji katika mkoa wa Mtwara ikiwemo mali ghafi,ni kivutio kilichosukuma kampuni yake kufikiri na kufanya uamuzi kuwekeza hapa nchini.


“Dhamira yetu ni kuhakikisha kuwa katika kipindi cha miaka kumi hadi kumi na mitano kiwanda kitakachojengwa kitaendeshwa kwa asilimia mia moja na wataalam na nguvu kazi ya Tanzania” alisisitiza Maatouk.


Akizungumza katika kikao hicho aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa Mamlaka Ya unendelezaji Maeneo huru ya Uzalishaji bidhaa za kuuza nje ya nchi EPZ ,knl mstaafu Joseph Simbakalia, alisema mkoa wa Mtwara unayo nafasi kubwa ya kuvutia wawekezaji wengi kutokana na ukweli kwamba mkoa huo ni pekee hapa nchini,mwekezaji akihitaji eneo la kuwekeza linapatikana na hakuna fidia kwani mamlaka ya bandari nchini ina eneo kubwa ambalo ilitoa fidia kwa wamiliki wa zamani wa eneo hilo.


“Mkoa wa Mtwara ni mkoa pekee akija mwekezaji na kusema mimi nahitaji ekari mia moja za kiwanda,nazungumzia EPZA sasa;baada ya kupewa eneo hilo,nitamwambia twende,hakuna fidia maana bandari walikwishatoa fidia.Eneo liko wazi,kwingine kote wanakwenda wanaanza kuzungumza,tuelewanae na wananchi miezi sita mwaka;wengine hawana subira,anasema bwana mimi nawapeni miezi miwili kama hamuwezi basi ntakenda Kenya,ntakwenda wapi wengine hawana subira”Alisisitiza Simbakalia.


Mkurugenzi wa EPZA alikwenda mbali na kubainisha kwamba huhitaji kuwa mtabiri kujua kwamba kama hali ya amani itaendelea jinsi ilivyo sasa hapa Tanzania,na hali ya Mtwara,katika nchi za Afrika mashariki na kati mji mkubwa wa viwanda katika ukanda huu utakuwa ni mji wa Mtwara.


Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tamisemi mheshimiwa Hawa Ghasia na mkuu wa mkoa huo mh.Halima Debdegu waliwataka wananchi wa mkoa huo kuwa watulivu na kuhakikisha amani inakuwa endelevu ili kuendelea kuvutia fursa zaidi za wawekezaji kutoka nje ya nchi.Kwa nyakati tofauti walisisitiza kuwa hatua hiyo ya kuwepo kwa amani na utulivu itasaidia sana kuongeza nafasi za ajiria na kupunguza umaskini katika jamii.


Aidha mkuu wa mkoa wa Mtwara aliwataka wananchi hasa vijana kuwa watulivu na kuhakikisha wanajielimisha katika maswala mbalimbali kupitia elimu rasmi na elimu ya maisha, ili waweze kuendana na mabadiliko yatakayoletwa na uwekezaji huo na ule unaokuta.


Kiwanda hicho cha mbolea kitakuwa ni uwekezaji wa pili mkubwa tangu gesi kugunduliwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi,kikitanguliwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha saruji cha mwekezaji kutoka nchini Nigeria Aliko Dangote ambacho kinatarajiwa kuanza uzalishaji wake miezi michache ijayo, ujenzi unaoendelea utakapokamilika.

---



Tanzania Mbolea and Petrochemical Company​

Tanzania Mbolea and Petrochemical Company (TMPC), a Tanzanian company that was specifically formed to design, build and operate a fertilizer-manufacturing factory in the Mtwara Region of Tanzania, using natural gas as raw material.[2]

When completed, the plant will be the largest fertilizer-manufacturing factory in Africa, with capacity of 3.8 million metric tonnes of product annually.[3]

Location
The factory is located on 400 hectares (988 acres) of land in Mtwara, in the Mtwara Region, in extreme southeastern Tanzania, "close to large offshore gas plants".[3] This is approximately 565 kilometres (351 mi), by road, southeast of Dar es Salaam, the commercial centre and largest city of Tanzania.[4] This is about 1,005 kilometres (624 mi), by road, southeast of Dodoma, the capital of the country.[5]

Overview
Tanzania Mbolea and Petrochemical Company, is a special purpose vehicle company (SPVC), established in 2016, to specifically design, build and operate the "Mtwara Fertilizer Factory".[6] The consortium in TMPC includes 1. The Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) 2. Ferrostaal Industrial Projects of Germany 3. Haldor Topsoe AS of Denmark and 4. Fauji Fertiliser Company Limited of Pakistan. This SPV will own 20 percent of the factory. Other potential investors in the factory include National Social Security Fund of Tanzania and Minjingu Mines.[1]

The factory is valued at $3 billion, as of August 2017.[3] The factory is expected to employ a total of 5,000 people, during construction and manufacturing operations.[3] Construction began in 2016,[2] with commissioning expected in 2020.[3] In 2021, the company began building a petrochemical complex in Lindi, Tanzania.[7]

Ownership
Tanzania Mbolea and Petrochemical Company Stock Ownership
RankName of OwnerPercentage Ownership
1Tanzania Petroleum Development Corporation25.0
2Ferrostaal Industrial Projects of Germany25.0
3Haldor Topsoe AS of Denmark25.0
4Fauji Fertiliser Company Limited of Pakistan25.0
Total100.00

References​

  1. Jump up to:ab Mtulya, Athuman (3 February 2015). "TSh1.7 trillion fertiliser plant mooted". The Citizen. Dar es Salaam. Retrieved 29 August 2017.
  2. ^ Jump up to:abc Senelwa, Kennedy (17 October 2016). "Work starts on new $1.5b Mtwara fertiliser plant". The EastAfrican. Nairobi. Retrieved 29 August 2017.
  3. Jump up to:abcdef Tairo, Apolinari (29 August 2017). "Tanzania spells out pricing guidelines for fertilisers". The East African. Nairobi. Retrieved 29 August 2017.
  4. GFC (29 August 2017). "Distance between Dar es Salaam, Tanzania and Mtwara, Mtwara Region, Tanzania". Globefeed.com (GFC). Retrieved 29 August 2017.
  5. GFC (29 August 2017). "Distance between Dodoma, Dodoma Region, Tanzania and Mtwara, Mtwara Region, Tanzania". Globefeed.com (GFC). Retrieved 29 August 2017.
  6. Bungane, Babalwa (2016-10-12). "'Natural gas saves Tanzania $7.4bn'". ESI-Africa.com. Retrieved 2023-03-04.
  7. Carmen (2021-10-22). "Tanzania Mbolea and Petrochemicals Company Kilwa Complex, Tanzania". Offshore Technology. Retrieved 2023-03-04.
External links
 
Muhusika wa Wikipedia hivi majuzi aliueleza ulimwengu kuwa kwa Karibu zaidi ya muongo (miaka kumi) mmoja, Vyombo vya ujasusi vya nchi za Magharibi na Marekani vimekuwa vikiingilia mtandao huu wa Wikipedia.

Sasa taarifa hiyo ya kiwanda haijulikan imeathiriwaje na ujasusi wa nchi tajwa hapo juu.
 
Ninawaza tu, kwa vidole vikipapasa 'keyboard': Sijui Samia angekuwa ni rais wa aina gani kama urais wake wote angeuweka rehani juu ya mradi kama huu, badala ya ule wa bandari?

Lakini sote tunajua jibu lake hapo ni lipi.
 
Huu uzi ili uchangie lazima uwe well informed,tunapenda nyuzi rahisi rahisi ambazo kila kitu tumetafuniwa ili ibaki kulaumu au kusupport.
Tatizo watanzania wanapenda ushabiki wa mpira tu. Yupo radhi kudiscuss mshahara ya wa Messi kuliko kudiscuss mambo ya msingi.
 
Back
Top Bottom