Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,020
- 4,698
Kila ukipita Singida unaona hali ni ileile miaka nenda rudi same applies to Manyara. Na hapa tunapita mjini hata maji ya kunywa shida, ukienda huko wilayani kisha vijijini hali ni mbaya zaidi.
Mkoa wa Kagera ni moja ya mikoa maskini nchini kwa sasa. Pamoja na hali ya hewa nzuri na kuzalisha watu wengi wasomi lakini hakuna maendeleo. Sababu kubwa ni wenyeji kupakataa kwao lakini cha pili ni Serikali kutopeleka miradi ya kimkakati.
Wakati uwanja wa ndege wa Chato unajengwa niliamini watu wa Kagera wangetumia vyema rasilimali hii kufanya biashara na Kongo, Uganda, Rwanda na Burundi lakini matokeo yake viongozi wa kanda ile walichokifanya sasa hivi nikwenda Dodoma kudhibiti hata maono ya JPM ya kupata mkoa mpya yasifikiwe. Unajiuliza mkoa mpya unawanyima kuishi masaki? Mkoa mpya wa Chato ungeweza kuwanyima wananchi chakula au ungeleta chakula zaidi?
Haya ni baadhi ya mambo ambayo ninapotafakari umaskini wa mikao hii natamani sana kujua kama ipo mikakati ya kuwakomboa wananchi wanaoteseka.
Mfano maji ya ziwa Victoria kwanini yasifike wilaya zote za Singida na Manyara kisha yakasambaa vijijini hata kwa kukopa trilions? Wananchi wakipata maji watazalisha na muda mfupi trilioni tuliyokopa itarejeshwa.
Kwanini tusifungue masoko makubwa ya mafuta na viwanda Singida? Mafuta yakzalishwa na kufungwa tayari kwa kuuza? Kwanini tusifungue mashamba ya kilimo makubwa ya umwagiliaji? Viongozi wote wazaliwa wa Singida na Manyara wanaishi Dar es Salaam lini watafikiria kurudisha nyumbani?