Viongozi wa kata wa cuf jimbo la lushoto kuhamia chadema wiki ijayo!

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Heshima kwako Mkuu!

Katika muendelezo wa kuendelea kukubalika kwa CDM wanachama na baadhi ya viongozi wa CUF kata ya kwemashai na Ngulwi jimbo la Lushoto wametangaza kujiunga na CDM wiki ijayo kutokana na kile walichodai ni chama cha CUF kukosa mwelekeo na tumaini la Watanzania kwa vyama vya upinzani nchini kubakia kwa CHADEMA.

Aidha baadhi ya wanachama wa CUF wamefurahishwa kwa jinsi CDM ilivyo na mikakati imara ya kienezi inayolenga kukimarisha chama.

Nitatoa taarifa rasmi wiki ijayo baada ya taratibu zitakapokamilika.
 
Ungeileta hii baada ya tukio. Hukusoma kuwa Lema aliwataja vigogo wanaotaka kuhamia cdm wakakanusha?
 
Ungeileta hii baada ya tukio. Hukusoma kuwa Lema aliwataja vigogo wanaotaka kuhamia cdm wakakanusha?

Hii ni habari ya uhakika, usiwe na wasiwasi mkuu mimi ndo kamanda wa uenezi Lushoto, utaratibu utakamilika soon nitarudi na habari kamili......
 
Mbelwa!
Umeruka kulivuka daraja kabla hujalifikia mkuu. Next time learn to hold your breath before you chew a gum.

Kaka! Kwa kifupi nimetoa taarifa hii kwa tahadhari kubwa, hivyo ondoa wasiwasi, natambua kinachoendelea kwa sasa!
 
Usiwe na haraka Mbelwa! Hili tsunami litamkumba kila mwenye ngozi ngumu. Umeleta taarifa ukiwa bado hujakamilisha utaratibu, kamilisha utaratibu kwanza. Nimeona hapo juu umesema "Utaratibu
utakamilika soon nitarudi
na habari kamili".

Kamilisha utaratibu ndio ulete hiyo habari kamili. Chadema ni chama makini, onyesha umakini unao sadifu uimara wa chama kinachoenda kushika dola.
Home sweet home, keep rocking home boys.

Dont rush! You rush you crush. Better slowly but sure.
 
Kaka! Kwa kifupi nimetoa taarifa hii kwa tahadhari kubwa, hivyo ondoa wasiwasi, natambua kinachoendelea kwa sasa!

Tatizo letu wakishakabidhiwa kadi utakuja kufungua uzi mwingine au utauendeleza huu huu? Maana JF tumechoka na habari moja ila sredi kibao
 
Itakuwa vyema kama atakuja ku-search na kuuendeleza huu uzi pindipo huo utaratibu utakapo kuwa umekamilika. Ninaexperience ya kutosha na watu wa Lushoto nimezaliwa, kusoma na kukulia hapo. Nakushauri Mbelwa mpaka utaratibu ukamilike ndio urudi tena, nakumbuka walisha jiapiza kuwa hata shekifu arudi na ahadi alizo ahidi mwaka 1995 hawamchagui, what happened after ambassador mshangama na kagonji kule Mlalo?!
 
Usiwe na haraka Mbelwa! Hili tsunami litamkumba kila mwenye ngozi ngumu. Umeleta taarifa ukiwa bado hujakamilisha utaratibu, kamilisha utaratibu kwanza. Nimeona hapo juu umesema "Utaratibu
utakamilika soon nitarudi
na habari kamili".

Kamilisha utaratibu ndio ulete hiyo habari kamili. Chadema ni chama makini, onyesha umakini unao sadifu uimara wa chama kinachoenda kushika dola.
Home sweet home, keep rocking home boys.

Dont rush! You rush you crush. Better slowly but sure.

OK!What comes around goes around....i accept challenges coz tunajenga pamoja..
 
Japo mda wa habari iyo bado, lakini ni habari yenye kufurahisha sana, ngulwi pia kwemashai napafahamu, maeneo ayo kiukweli ilikuwa ni ngome ya cuf (ccm 'b') ivyo litakuwa pigo kwa ccm magamba pia, tutaraji pia lushoto mjini watu kwa wingi watajivua gamba na kuvaa gwanda
 
Kaka! Kwa kifupi nimetoa taarifa hii kwa tahadhari kubwa, hivyo ondoa wasiwasi, natambua kinachoendelea kwa sasa!
Kama ukishauriwa unakuwa mgumu kukubali basi hufai kuwa kiongozi, siku zote kiongozi bora hupokea mashauri na kuyafanyia kazi.. Bila kumumunya ndugu yangu umekurupuka, hata kama una uhakika 101% ulipaswa kuwa na subira na hiyo (subira) ndiyo sifa kuu ya uanasiasa.
 
Back
Top Bottom