Viongozi wa CHADEMA kitaifa waongezewa mashtaka mapya Arusha

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
VIONGOZI wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamezidi kubanwa na mahakama baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwafungulia mashitaka mapya yanayohusu maandamano ya Arusha.

Hata hivyo, DPP pia amewaachia huru washitakiwa wengine 11 baada ya kubaini kuwa hawahusiki na kesi iliyowafikisha mahakamani hapo.

Viongozi waliofunguliwa mashitaka mapya manane ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo.

Wanasiasa hao wanaungana na wanachama na wafuasi wengine 16 akiwamo mchumba wa Slaa, Josephine Mushumbusi kujibu mashitaka hayo.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Serikali, walioachiwa huru ni Edwin Kakolaki ni Kenneth Bundala, Pochesi Kimario, Eusebia Akaro, Bakari Issa, Goodluck Kimaro, Elisante Noel, Calvin Daudi, Michael Kimario, Mevorongori Lukumay, Prosper Kimaro na Pancras Kimario.

Akizungumza nje ya mahakama, Lema alisema, haitakuwa ajabu kufungwa akitolea mfano wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kwamba alifungwa, lakini bado akawa shujaa wa nchi yake.

Kakolaki alitaja mashitaka hayo mapya dhidi ya viongozi hao na wenzao, kuwa ni kula njama ya kutenda makosa ya kufanya mkusanyiko, kukaidi amri ya Jeshi la Polisi, kufanya mkusanyiko isivyo halali na kufanya vurugu baada ya kutolewa amri ya Polisi.

Mashitaka mengine ambayo yanamhusu Slaa peke yake ni kutoa maneno ya uchochezi Januari 5 katika viwanja vya NMC, Arusha, akiwa Katibu Mkuu wa Chadema.

Mashitaka mengine yanamhusu Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, ambayo ni ya kutoa maneno ya uchochezi na kejeli dhidi ya Rais Jakaya Kikwete. Mengine ambayo yanawahusu Ndesamburo, Slaa na Samson Mwigamba ni ya kuchochea na kutaka kutorosha watu waliokuwa chini ya ulinzi Januari 5 kwenye viwanja vya NMC, Arusha.

Pia washitakiwa hao 19 kwa pamoja wanadaiwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha taharuki kwa jamii. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Judith Kamala, washitakiwa kwa pamoja walikana mashitaka.

Kakolaki alidai mahakamani hapo kwamba, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe ya usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo. Hakimu Kamala aliamua kesi hiyo ianze kusikilizwa Aprili 29.

Hata hivyo, wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya mahakama waliendelea kutoa maneno ya kejeli baada ya kusikia mashtaka mapya dhidi ya viongozi hao. Baadhi yao walisema mahakama inapaswa kutenda haki wakidai kuwa, mashitaka yamepindishwa na kutenganisha baadhi ya washitakiwa.

Lema alipotoka mahakamani baada ya kesi kuahirishwa, aliwatuliza wafuasi wa chama hicho kwa kuwaambia kuwa hata Mandela alifungwa kwa kupigania haki hivyo wasubiri uamuzi wa mahakama. Aliwasihi wafuasi wa Chadema kutawanyika na kwenda kwenye shughuli zao na warudi mahakamani hapo Aprili 29.

Viongozi hao wa Chadema walifanya maandamano Januari 5 licha ya Polisi kukataza kwa misingi ya kiusalama, lakini pia wafuasi wao wakataka kuvamia kituo kikuu cha Polisi kuwatoa viongozi waliokuwa wanashikiliwa. Katika ghasia hizo, watu watatu walipoterza maisha kwa kupigwa risasi na polisi akiwamo raia mmoja wa Kenya.

Source: Habari Leo
 
Sidhani kama jitihada hizi zinaweza kudhoofisha nguvu na kasi ya Chadema, badala yake wanazidi kuipa umaarufu.
 
Watahangaika tu, lakini mwisho wa siku, mabere marando yupo hawa waendesha mashitaka ambao walishindwa hata kumfunga zombe ambaye ushahidi mmoja unaonesha kwamba aliuwa lakini ukashindwa kumtia hatiani itakuwa hii kesi ya kipuuzi, labda wangeongeza na shitaka kuwa waliuwa kwa kushirikiana na polisi.

Wasicheze na peoplezzzz, power wawe makini bado siku 19 tu zimebaki kama uchaguzi wa meya wa arusha haujafanyika mhhhhhh, sijui
 
Nadhani Mahakama ya kiCCMCCM itaharakisha kifo cha serikali chovu na ya dhulma hii mapema kinyume na ilivyotarajiwa. Itatusaidia wananchi ambao ndiyo "Nguvu ya Umma" CCM wanayodai hawaifahamu kufanya uamuzi wa kuihukumu serikali ya dhulma hii mapema zaidi.

Hakuna mantiki ya kuwanyanyasa viongozi wa CHADEMA kwa kesi za kupikwa bila ya kuwafikisha Mahakamani walioua na kujeruhi ndugu, jamaa na wananchi wasio na hatia kwa makusudi. Tutahakikisha nchi inawaka moto hadi haki ipatikane kwa maana waliouwawa na kujeruhiwa na Polisi wana haki ya kutetewa pia. Safari hii hatutakubali kutulizwa iwe na Mbowe, Slaa, Lema, Zitto au kiongozi yeyote wa CHADEMA hadi tulipe kisasi.

Kwa taarifa yao CCM yoote wanayowafanyia wapinzani sasa yatalipizwa sawia. Tatizo ni upole wa hawa viongozi wa CHADEMA maana kama wangekuwa wametoa msimamo tungeshawatangulia Misri na Tunisia mapema tangu walipotuchakachua.
 
Ole wenu CCM maana kifo chetu ktakuwa kibaya kuliko jnsi ilvokuwa ikitegemewa, nyie endeleen kuchefua akili na utashi wa waTanzania wapole, sku tukiingia na mashoka na mapanga mtaan ndo mtaitambua hasira yetu!

Sijawaskia mkizungumzia kuhusu vifo vya ndg zetu mloua badala yake mmekazia mimacho yenu kwa wasiohuska, nyoooooo! Ivi walokufa ni mende? Mnadhani kua hatujaona uovu wenu mlotufanyia? Mmevunja na kuharibu mali na magari yetu kwa kutuvunjia vioo!

Mi nadhani dawa yenu itolewe mapema hata km bado haijaiva vzr.
 
mwenye kutambuwa kwamba kunakifo akaamuwakufanya maandarizi kujichongeya jeneza kanunuwa kaburi kunahajagani kumuraumu? CCM na sirikari yake yotehaya namaandalizi yakifo tenakifo chakujinyonga ataungewashauli juuyahilo haiwezekani faham ilishapotea na tama ubinafus
 
CCM haiko siriasi tena.Na ndio mwisho wa chama hiki cha CCCM.Ok yetu macho na mikono.Karibu dk Slaa ikulu ya MAGOGONI.
 
Watahangaika tu, lakini mwisho wa siku, mabere marando yupo hawa waendesha mashitaka ambao walishindwa hata kumfunga zombe ambaye ushahidi mmoja unaonesha kwamba aliuwa lakini ukashindwa kumtia hatiani itakuwa hii kesi ya kipuuzi, labda wangeongeza na shitaka kuwa waliuwa kwa kushirikiana na polisi.

Wasicheze na peoplezzzz, power wawe makini bado siku 19 tu zimebaki kama uchaguzi wa meya wa arusha haujafanyika mhhhhhh, sijui
Napo mimi ndipo ninapopasubilia
 
Nadhani Mahakama ya kiCCMCCM itaharakisha kifo cha serikali chovu na ya dhulma hii mapema kinyume na ilivyotarajiwa. Itatusaidia wananchi ambao ndiyo "Nguvu ya Umma" CCM wanayodai hawaifahamu kufanya uamuzi wa kuihukumu serikali ya dhulma hii mapema zaidi.

Hakuna mantiki ya kuwanyanyasa viongozi wa CHADEMA kwa kesi za kupikwa bila ya kuwafikisha Mahakamani walioua na kujeruhi ndugu, jamaa na wananchi wasio na hatia kwa makusudi. Tutahakikisha nchi inawaka moto hadi haki ipatikane kwa maana waliouwawa na kujeruhiwa na Polisi wana haki ya kutetewa pia. Safari hii hatutakubali kutulizwa iwe na Mbowe, Slaa, Lema, Zitto au kiongozi yeyote wa CHADEMA hadi tulipe kisasi.

Kwa taarifa yao CCM yoote wanayowafanyia wapinzani sasa yatalipizwa sawia. Tatizo ni upole wa hawa viongozi wa CHADEMA maana kama wangekuwa wametoa msimamo tungeshawatangulia Misri na Tunisia mapema tangu walipotuchakachua.
Pamoja mkuu, umesema yaliyo moyo mwangu, safari hii tutaenda tumekamilika wakitugusa tu basi uhuru kamili utaanzia Arusha...
 
ushauri wa bure kwa rais kikwete na ccm yake TANZANIA ni mali ya WATANZANIA si mali yako wala ccm maamuzi mtakayoyafanya yawe na maslahi na taifa sio ubinafsi wenu utuletee matatizo.mbinu zenu chafu mnazotakakutumia kudhoofisha upinzani hazitafanikiwa kamwe vijana tunasema nchi imekushinda ondoka kabla hatujakuondoa
 
hata hivyo nilijua mapema kuwa ARUSHA itakuwa kituo cha mapinduzi tanzania kwani c tunakumbuka azimio la arusha? dr.slaa endelea kuandaa baraza lako la mawaziri
 
Hii ya "Mchumba wa Slaa" imekaaje hii? Jitu zee kuwa na mchumba? Na mkewe Jee? Na mume wa huyo mchumba jee? Na kanisa katoliki? Mnhhh.

"Khatar Kubwa".
 
Sina hakika kama hizi mbinu zitazaa amani Arusha na nchini kote. Siku ambayo wataamua kuwatupa jela hao viongozi wakuu wa CHADEMA, basi sidhani kama JK ataweza kumaliza kipindi chake cha mwisho kwa amani.
Siko hapa kuchochea chochote, lakini naamini mnakumbuka kipindi cha uchaguzi mwaka jana watu walivyokuwa na hasira baada ya kugundua janja ya serikali na tume ya uchaguzi. Watanzania wanajua kuwa haya yote yanafanyika ili kuwaziba midomo hawa viongozi, kitu ambacho siamini kitafanikiwa. People need their country back from THUGS, yes I just said, THUGS.
 
Back
Top Bottom