Viongozi 32 wa ngazi ya juu wa CDM warudisha kadi zao za uanachama!

ZINGATIA KWENYE RED, hii wilaya ya Nyanza imekuwa ngeni kwangu labda kwavile nimekuwa sipo huko muda mrefu but nimegoogle sikuipata kabisa. Nilipotoka mimi niliacha Mwanza ilikuwa na wilaya kama ifuatavyo. ILEMELA, NYAMAGANA, SENGEREMA, GEITA, MAGU, KWIMBA, MISUNGWI NA UKEREWE. Hii wilaya ya Nyanza iko upande gani mkuu?
Tumsamehe mleta hoja ni katika harakati za kuwahi ku-post nafikiri atarekebisha, ila ujumbe ndio huo, sijui hao viongozi wa ngazi za juu ni akina nani labda ngazi za juu za shina kwenye vijiwe. What I know, Ngeleja asicheze na wasukuma labda akae huku huku asirudi Dar, amuulize Dialo pamoja na kuwa na TV, redio yake tulikula vyuku vyake sana na kumwachia manyoya.
 
Ngeleja anagawa nini huko? Watanzania tutanunuliwa mpaka lini, Ngeleja ana kitu gani kipya cha kumwambia mtu akahama chama, tamaa zitatumaliza wabongo

...Kama hii ni kweli basi ni lazima itakuwa ni ngawira tu na dau si ajabu ni kubwa sana, labda huu ni mkakati wa chama cha mafisadi/magamba kuelekea 2015 katika kila kona ya nchi ambayo CHADEMA imekuwa na umaarufu mkubwa basi kuwanunua viongozi wa chama hicho kwa mamilioni chungu nzima. Mkakati huu lazima yule fisadi Rostam atakuwa ana mkono wake maana kama tujuavyo ana mabilioni chungu nzima
 
Uzushi mwingine hata kama ni viwanachama dhaifu, kichwa cha habari kikuubwa eti viongozi wa juu wa cdm? mie nilitegemea unatuwekea na wasifu wa hao viongozi waliohama......!
Watakuwa wale wazee wajumbe wa nyumba kumi kumi hao njaa zinawasumbua hao. mtu mwenye akili timamu hawezi kamwe akawa mwanachama wa ccm.
 
Ni pigo kubwa kwa Wenje!

hao ni sisomizi tu,yaani wanachama 32 mnaona ni pigo? Jumapili iliyopita tulienda kujenga chama cdm kijiji kimoja kinaitwa ngamanga jimbo la njombe kaskazini tulikomba wanachama wa ccm 108 na hatujatangaza ,wanaoingia cdm toka ccm kila siku ni wengi sana ila tu hawatangazwi kama magamba wafanyavyo.
 
Sengerema viogozi 7 Nyanza 32 jumla 39 !! chama kina watu gani hawa wasio na msimamo ?

hata Sengerema nasikia walio hama chama walizomewa na wananchi walipo kuwa wakijitambulisha jukwani .. kimsingi naona Mwanza kazi ipo kwa pande zote mbili ( chama tawala na Upinzani)
 
ZINGATIA KWENYE RED, hii wilaya ya Nyanza imekuwa ngeni kwangu labda kwavile nimekuwa sipo huko muda mrefu but nimegoogle sikuipata kabisa. Nilipotoka mimi niliacha Mwanza ilikuwa na wilaya kama ifuatavyo. ILEMELA, NYAMAGANA, SENGEREMA, GEITA, MAGU, KWIMBA, MISUNGWI NA UKEREWE. Hii wilaya ya Nyanza iko upande gani mkuu?
Mkuu hata hiyo ya GEITA pia haipo Mwanza tena!

Lakini kuhama kwa hao wana CDM si jambo la kushangaza, kwani hatukumbuki kwamba kuna thread humu watu walilalamika kuhusu utendaji wa wabunge wa CDM huko mwanza? Hapa hakuna mchawi CDM iwasimamie wabunge wake waahakimishe wanatekeleza ahadi zao. Regia alikuja humu akatuambia alichokifanya tangia awe mbunge. Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna mbunge mwingine wa CDM aliyejitokeza kutuambia kama Regia na sisi tukampa ushauri! Huenda hakuna walilolifanya ama wamefanya kidogo sana ukilinganisha na matarajio ya wananchi wakati wanawachagua!
 
Wakuu JF sio sehemu ya porojo kama mtu huna data au facts zozote usimwage pumba humu JF...

Hizi ni pumba kwa kuwa zimemwagwa na Pro-chadema watu wanashindwa kuhoji..

Chadema Mwanza, wameshinda Wilaya tatu Ukerewe, Ilemela, Nyamagana.

Sasa hii Wilaya ya Nyanza Mbunge wake ni nani?
 
Huyu Ngeleja katumwa na JK kutumia hela za makampuni ya uchimbaji dhahabu kuirejesha kanda ya Ziwa mikononi mwa CCM. Hii inaonyesha kitu kimoja tu, kwa kuwa wanashindwa kuwaondoa wananchi wa sehemu hiyo kutoka umasinikini uliokithiri pamoja na utajiri mkubwa walio nao chini ya ardhi yao, basi sasa CCM inatumia utajiri huo kuwanunua viongozi wachache wa CDM.

kamwe CCM haitafanikiwa! Umma wa sehemu hiyo ni mkubwa mno na wameshaichoka CCM.

Kama kweli Ngeleja ana ubavu wa kuurudisha mkoa wa Mwanza katika himaya ya CCM, athubutu siku moja kuitisha mkutano pale Kirumba, na Dr Slaa afanye mkutano wake ule uwanja mwingine nimesahau jina, tuone wapi watakwenda watu wengi.

Very simple! Hawezi fisadi huyo, atapopolewa mawe! Anatapatapa tu na kununua vizee vichache vimasikini.

Fisadi Ngeleja anamdanganya JK kutumia pesa kwa kazi hiyo, kumbe hapo hapo anajitajirisha yeye mwenyewe! Juzi kamwaga milioni 500 kule jimboni kwake na Hoisea hata hashituki!

Ndo maana Jenerali Ulimwangu alimchamba sana Hosea katika Raia mwema wiki iliyopita, na sidhani Hosea ana ubavu wa kumjibu kwa hoja alizotoa Jenerali.

Who wants to have a bunch of sellouts on their side anyway. . !! Kama wananunulika kirahisi namna hiyo basi waendee tu maana wangeleta matatizo baadae wakati wanahitajika zaidi.
 
Sengerema viogozi 7 Nyanza 32 jumla 39 !! chama kina watu gani hawa wasio na msimamo ?

hata Sengerema nasikia walio hama chama walizomewa na wananchi walipo kuwa wakijitambulisha jukwani .. kimsingi naona Mwanza kazi ipo kwa pande zote mbili ( chama tawala na Upinzani)
mkuu mimi naona kazi ipo kwa CDM kwa kuwa hiyo si dalili njema kwenye ngome yao huko Mwanza
 
Wakuu JF sio sehemu ya porojo kama mtu huna data au facts zozote usimwage pumba humu JF...

Hizi ni pumba kwa kuwa zimemwagwa na Pro-chadema watu wanashindwa kuhoji..

Chadema Mwanza, wameshinda Wilaya tatu Ukerewe, Ilemela, Nyamagana.

Sasa hii Wilaya ya Nyanza Mbunge wake ni nani?
Hakuna wilaya ya Nyanza!..
 
Inaoneka kila kiongozi ndani ya Chadema ananunulika tatizo bei tu, huu ndio ukweli mtaongea sana lakini mwisho wa siku nikununuliwa tu.
 
Huyu Ngeleja katumwa na JK kutumia hela za makampuni ya uchimbaji dhahabu kuirejesha kanda ya Ziwa mikononi mwa CCM. Hii inaonyesha kitu kimoja tu, kwa kuwa wanashindwa kuwaondoa wananchi wa sehemu hiyo kutoka umasinikini uliokithiri pamoja na utajiri mkubwa walio nao chini ya ardhi yao, basi sasa CCM inatumia utajiri huo kuwanunua viongozi wachache wa CDM.

kamwe CCM haitafanikiwa! Umma wa sehemu hiyo ni mkubwa mno na wameshaichoka CCM.

Kama kweli Ngeleja ana ubavu wa kuurudisha mkoa wa Mwanza katika himaya ya CCM, athubutu siku moja kuitisha mkutano pale Kirumba, na Dr Slaa afanye mkutano wake ule uwanja mwingine nimesahau jina, tuone wapi watakwenda watu wengi.

Very simple! Hawezi fisadi huyo, atapopolewa mawe! Anatapatapa tu na kununua vizee vichache vimasikini.

Fisadi Ngeleja anamdanganya JK kutumia pesa kwa kazi hiyo, kumbe hapo hapo anajitajirisha yeye mwenyewe! Juzi kamwaga milioni 500 kule jimboni kwake na Hoisea hata hashituki!

Ndo maana Jenerali Ulimwangu alimchamba sana Hosea katika Raia mwema wiki iliyopita, na sidhani Hosea ana ubavu wa kumjibu kwa hoja alizotoa Jenerali.

Penye red: Duh! Bonge la challenge na kama Ngeleja anataka kujipima nguvu yake afanye hivyo! Mawe!!! Siku Dr Slaa akisema 'haya tufanye mikutano hapo Mza,' fisadi Ngeleja ataufyata kama m***.

Anacheza tu na hela za wananchi!
 
Huyu Ngeleja katumwa na JK kutumia hela za makampuni ya uchimbaji dhahabu kuirejesha kanda ya Ziwa mikononi mwa CCM. Hii inaonyesha kitu kimoja tu, kwa kuwa wanashindwa kuwaondoa wananchi wa sehemu hiyo kutoka umasinikini uliokithiri pamoja na utajiri mkubwa walio nao chini ya ardhi yao, basi sasa CCM inatumia utajiri huo kuwanunua viongozi wachache wa CDM.

kamwe CCM haitafanikiwa! Umma wa sehemu hiyo ni mkubwa mno na wameshaichoka CCM.

Kama kweli Ngeleja ana ubavu wa kuurudisha mkoa wa Mwanza katika himaya ya CCM, athubutu siku moja kuitisha mkutano pale Kirumba, na Dr Slaa afanye mkutano wake ule uwanja mwingine nimesahau jina, tuone wapi watakwenda watu wengi.

Very simple! Hawezi fisadi huyo, atapopolewa mawe! Anatapatapa tu na kununua vizee vichache vimasikini.

Fisadi Ngeleja anamdanganya JK kutumia pesa kwa kazi hiyo, kumbe hapo hapo anajitajirisha yeye mwenyewe! Juzi kamwaga milioni 500 kule jimboni kwake na Hoisea hata hashituki!

Ndo maana Jenerali Ulimwangu alimchamba sana Hosea katika Raia mwema wiki iliyopita, na sidhani Hosea ana ubavu wa kumjibu kwa hoja alizotoa Jenerali.

Una maana y viwanj vy Furahisha?
 
Hebu niambieni, ile kamati ya Bunge kuhusu Jairo ilisemaje kuhusu fisadi huyu? Ana roho ya paka kuendelea na wadhifa wake badala ya kujiuzulu!!!

Kweli CCM itamfia mikononi mwa Kikwete, pamoja na sasa kuamrisha watu wake kutumia pesa kununua wafuasi!
 
Back
Top Bottom