Vilio ni vile vile

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Kwako atakwambia yupo bize hana muda, ila ukweli ni kwamba yupo sehemu na mtu mwingine akipoteza muda.

Wakati wewe unapambana kuboresha penzi lako, yupo mtu anarekebisha mazingira yatayomvutia mpenzi wako.

Wewe unatembea na ahadi zake ili umkumbuke popote uendapo, lakini yeye anatembea na chaji yake ili apate nafasi ya kulala popote afikapo.

Wewe unapiga magoti kumuombea kwa Mungu ili amlinde, yeye huko alipo anabishana na nafsi yake asitumie kinga ili asijilinde.

Wewe unasema ni yeye tu anaekufaa, lakini yeye ana wapenzi wengi na haoni wa kumfaa. Wewe unampa kipaumbele na kumsikiliza kuliko watu wengine, lakini yeye anapewa vipaumbele na kutunzwa pia na watu wengine.

Ni kweli unamwambia unampenda kila siku, lakini bahati mbaya ni kwamba hilo neno analisikia kutoka kwa kila mtu na kinachouma zaidi jibu lile alilokujibu wewe la "nakupenda zaidi" ndio hilo hilo aliwajibu wengine.

Kwahiyo hapo muongo ni nani? mimi, wewe au yeye?? ukute muongo ni mwalimu wetu wa baiolojia aliyetufundisha kuwa moyo wa mwanadamu una vyumba vinne. Sasa mbona huyo unaempenda amewapa nafasi watu wengi kwenye moyo wake? Au yeye moyo wake ni Apartment?

Alisikika mmoja akisema "anaweza kukwambia watu waliomtongoza akawakataa, lakini hawezi kukwambia aliowakubalia"

Siku hizi usaliti imekuwa ni mithili ya shubili au pakanga chungu ila unapewa na maneno matamu ya kupozea. Siku hizi usaliti imekuwa ni fashion, kiasi kwamba mtu akiwa na mpenzi mmoja anaonekana ni mshamba.

Aaanh! nimeelewa, kumbe nyie bado mmelala. Kumbe naongea na watu ambao wapo usingizini. Kama hamjalala mbona hamkushtuka mlipopewa takwimu za sensa kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume lakini ajabu ni kwamba kila mwanamke ana mwanaume.

Amkeni nyie, amkeni nyie watu wa karne hii. Karne ambayo inabadili dhambi majina ili watu wakizitenga wasihisi hatia tena. Hii karne uaminifu ni gharama, na ndio maana usaliti unasambazwa bure.

Haya endeleeni kudanganyana mi yangu macho. Kelele za wanaolia na kulalamika kuhusu mapenzi zitazidi kuongezeka kila siku sababu wapenzi wengi hawajui umuhimu wa uaminifu hivyo wanajidhuru na madhara ya usaliti.

Kwenye kalamu ni yule yule kijana wenu Amani Dimile, juzi jana na leo

#amanidimile #mwana_ukae #misemo_ya_hekima #quotes #tungomaridadi #mapenzi
 
Back
Top Bottom