Vijana Watanzania tafuteni majibu ya maswali magumu

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Wakuu

Kuna wakati ili tuendele tunahitaji ujasiri wa kusimama, lakini si kwa kutoa majibu mepesi, bali majibu ya maswali magumu yakiwa majawabu huru. Tutoe majibu huru yasiyokuwa na harufu ya kupandikizwa.

Ni kwa bahati mbaya nchi yetu kitambo hatukujenga misingi ya ujasiriamali. Kwa mapinduzi makubwa yaliyotokea katika sekta ya mawasiliano, kwamba asilimia kubwa ya vijana wana vishikwambi mkononi, matarajio yangu halali vijana hawastahili kutumia mitandao ya kijamii kulalamika, bali waitumie kama fursa ya kujikwamua kiuchumi.

Kufikia hili, tunahitaji vijana kujitambua. Kila kukicha kijana atafute fursa. Ni vyema tuangalie tunapokwenda kabla ya kutoa majibu mepesi. Lazima tufikirishe akili kwanza! Kabla vijana hawajatafuta kusifiwa, waangalie misingi waliojijengea kwa nia ya kuwa na familia imara zitakazo kuwa na urithi wa kudumu. Vijana wabadili lugha na mijadala yao vijiweni. Mazungumzo yawe ni mipango ya maisha ya kwa sasa na siku zijazo.

Natoa hoja hii, kwa kuangalia mbali na kutanguliza maslahi mapana ya vijana wote wa Tanzania waliojiajiri kupitia sekta mbalimbali. Nawaheshimu na kuwapenda sana vijana, lakini kuna mahali tunakosea mno!

Hivi karibuni ndugu zetu Kenya wamefanya uchaguzi. Kipindi chote cha kampeni, vijana hawakuwa wakiuliza mawali ya serikali itafutanyia nini, bali waliuliza serikali itajengaje fursa za wao kukua kiuchumi.

Ni bahati mbaya hapa kwetu kila siku kwenye mitandao ya kijamii na vijiweni, kila awaye ana gunia la lawama kwenda kwa Serikali. Sioni tofauti kati ya vijana wa Mwaka 1980 na sisi 2022. Ukifuatilia kushindwa huku kwa vijana kutafuta majibu ya masuala mazito yanayowakabili, jibu letu ni kuwa hatupo tayari kuwa rasmi, kujali kesho yetu.

Nasikitika, kwamba vijana wetu wako tayari kulipia gharama za kupofusha akili zao, sijui wanaita “connections”, tena kwa gharama kubwa badala ya kusaka masoko ya mchicha, mayai, utengenezaji wa tofali, ujenzi, uuzaji wa mazao mtandao au kutafuta uwakala na kazi nyingine nyingi zilizozagaa mtandaoni.
Inawezekana, narudia, inawezekana kuwa vijana wetu hawana utaalam wa kutumia mtandao na hili linaweza kutumiwa kama sababu ya kutopata kazi za kufanya kupitia mtandaoni, lakini najiuliza nani aliwapa utaalam wa kutafuta “connections?” Walifundishwa na nani? Iweje wana utaalam huo, lakini hawana utaalam wa kutafuta kazi mtandaoni? Tuitumie vizuri mitandao itulinde.

Hii ni hatari mno, lakini imenifikirisha kuwa vijana wengi Watanzania hawaijui kesho yao na ujana hauwezi ukadumu na kukaa milele. Kuna msemo kuwa kazi inavyofanywa na nywele, ndicho chakula cha mvi siku za usoni. Vijana tusipoandaa mazingira yetu sasa, hakika tutakuwa na wakati mgumu milele.

Vijana inapaswa wajitambue. Tumesikia vijana madaktari 9 waliounganisha nguvu huko Kipunguni Dar es Salaam wakaanzisha zahanati. Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, ameahidi kuwasaidia kutimiza ndogo yao. Yule anayewaza nje ya mstari wa kawaida ndiye anatoboa.

Narudia, kuna siku vijana wanakesha mtandaoni kutafuta connection ya dada yetu maarufu kwenye mitandao anayewajaza upepo bila mashiko. Hapa nikamkumbuka rafiki yangu Ruge Mutahaba, nikajisemea moyoni mwanangu pumzika salama na Semina za Fursa.

Kwanini tutafute majibu mepesi kwa ajili ya vijana wetu? Lipo tatizo mahali. Kwanza vijana tumekosa ushirikiano sisi kwa sisi hatupo pamoja. Vijana kukaa na kujisifu haisaidii.

Tumeshuhudia wengi wanapoteza muda katika kujaza akili upepo, ila maisha yanapobana wanaelekeza lawama Rais Samia Suluhu Hassan. Ni kweli Serikali ina wajibu wa kuwaonyesha vijana fursa, ila kamwe Serikali haitafanya kazi kwa niaba ya mikono yako.

Tukiendelea hivi, itafika mahala ambapo naogopa kuwa kuna siku wanafunzi watafeli mitihani, pamoja na Serikali kujenga shule, kuajiri walimu, kufuta ada na mengine mengi, vijana tusipojishughulisha tutamtupia lawama Rais Samia kwa kosa la wanafunzi kutoketi tukasoma wakaelewa waliyofundishwa darasani. Wengine watalalamika kuwa Rais hasomi masomo kwa niaba yao na wao wakashinda mitihani!

Sisi Vijana hatuna budi ya kutambua tunao wajibu katika taifa. Vijana tunatakiwa kuleta mapinduzi ya fikra kwa kubadili mitazamo, fikra na dhana zinazoturudisha nyuma katika kujikomboa kiuchumi, ikiwemo utegemezi kwa Serikali, husda, kukatishana tamaa na kutoungana mkono.

Vijana tunatakiwa kukabiliana na changamoto za kiuchumi zilizo mbele yetu, ikiwemo ushindani mkubwa wa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, dunia ya utandawazi na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda yajayo mbele yetu.

Sisi Vijana hatuna budi kushikamana, kusaidiana na kuinuana kwa lengo la kuhakikisha tunaibua fursa mbalimbali za kiuchumi hapa nyumbani Tanzania.

Serikali ina wajibu kwetu sisi vijana kwa kuweka mazingira wezeshi ya kisera, kisheria na kitaasisi yanayochochea ustawi wetu, hifadhi ya jamii na kutuwezesha kufikia kilele cha ndoto zetu au ukomo wa uwezo, vipaji na vipawa vyetu katika nyanja zote. Hii iwe ni katika uongozi, biashara, uvumbuzi, ubunifu, sanaa na michezo, tunayo fursa hiyo.

Kama nilivyosema, Serikali inatujengea vijana uwezo kwa kutupatia stadi muhimu za kiuongozi, biashara na kitaasisi tuweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya dunia, kumudu ushindani katika Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutuandaa kikamilifu kutoachwa nyuma na kukabiliana na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda yajayo mbele yetu.

Serikali ya Awamu ya Sita imeongeze bidii kuhakikisha upatikanaji wa taarifa kuhusu fursa za elimu, uendelezaji vipaji, biashara na uchumi za nje zitokanazo na mkakati wa Diplomasia ya Uchumi ambapo inahakikisha zinatufikia. Kwa hapa Rais Samia hana mpinzani, bali kazi kwetu sisi vijana.

Serikali imeongezi kasi ya kuchochea upatikanaji wa mitaji kwa vijana, hususan biashara ndogo na kati kwa kuboreshe sera kwenye taasisi za fedha za umma na sekta binafsi kutukopesha sisi vijana kwa masharti nafuu. Tunasikia kinachoendelea katika sekta ya kilimo yalikojazwa mabilioni ya fedha zikisubiri sisi vijana tuchukue fursa hizi.

Kuna mipango ya kutunganisha na mifuko mbalimbali ya uwezeshaji iliyopo chini ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi la Taifa (NEEC), ambayo tunaikaribisha. Hapa nina wazo zito. Mama yangu mpendwa Rais Samia, ikikupendeza naomba uanzishe Benki ya Maendeleo ya Vijana.

Mheshimiwa Rais tunakuomba kufanya mapitio katika sera ya Ununuzi na Sheria ya Manunuzi ya Umma Mwaka 2011 na Kanuni zake za Mwaka 2013 na kuelekeza walau asilimia 30 ya manunuzi ya bidhaa na huduma zifanywe na Vijana. Hapa utakuwa umetuongezea kasi wakati vijana tunazidi kusaka fursa. Mungu ibariki Tanzania.

Asante sana.
Majibu mepesi kwenye majawabu huru.

Billal Saadat.
0742 117302.
 
Mkuu PendoLyimo, nimekupenda bure kwa bandiko hili la Bilali Sadati,
Asante, ubarikiwe sana!.
P
 
Unamaanisha nini unaposema sera ibadilishwe na kuwa 30% ya manunuzi ya bidhaa yafanywe na vijana?
Ninachojua kazi ya kununua hasa kitaasisi ina idara maalumu ya manunuzi ambayo kazi zake zimeainishwa kwenye sheria ya manunuzi...Sasa hapo vijana wanunue??Aaah sijakuelewa,taasisi zina wafanyakazi wakiwemo vijana kwenye idara husika na hawanunui kwa ajili ya matumbo yao bali sheria ilivyo ni kuhakikisha ile “Value for money” inapatikana kwa either kuselect lowest evaluated bidder mathalani lakini ku maintain quality na other factors...
 
Back
Top Bottom