Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,503
- 113,616
Vijana wasomi kote nchini na haswa wahitimu wa vyuo vikuu, wamepewa changamoto ya kuutumia usomi wao kubaini fursa mbalimbali zilizopo kwa kujiajiri, badala ya kubweteka kwa kusubiria kuajiriwa rasmi au kuendelea kusotea kusaka ajira rasmi ambazo ni finyu kulinganisha na idadi ya wasomi.
Changamoto hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Trade Development Authority (TanTrade), Bibi Jacquline Mneney Maleko, wakati wa Semina maalum ya Uhamasishaji vijana wasomi Kujiajiri, iliyofanyika ukumbi wa JK Nyerere, TanTrade, Kilwa RD, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Bibi Maleko, Tanzania inazo fursa nyingi za kujiajiri, ambapo watu kutoka nchi za wenzetu wanakuja kuzitumia, huku Watanzania tukibaki kama watazamaji, hivyo ni muhimu kwa vijana wasomi, wahitimu wa vyuo vikuu nchini, kuutumia usomi wao kubaini fursa na kuzichangamkia.
Bibi Maleko amesema, anashangazwa na idadi kubwa ya wahitimu wa vyuo vikuu wanaojitokeza kusaka ajira, na kutolea mfano ameshangaa kuona waombaji zaidi ya 3,000 wamejitokeza kufanya interview ya kazi kugombea nafasi 30 tuu za kazi, hivyo kati ya hao, watakaopata ajira ni watu 30 tuu na wale wengine 2, 970 wataendelea kusubiria ajira nyingine zitangazwe na kujikuta wakiendelea kubweteka kusotea ajira, wakati kuna fursa nyingi za wao kutengeneza ajira.
Bibi Maleko amesema, hakuna sababu kwa vijana wasomi waliohitimu vyuo vikuu, kubweteka kusubiria ajira rasmi wakati Tanzania umezungukwa na fursa nyingi za kujiajiri, hivyo kupata maisha bora kuliko hata kusubiria ajira na kutegemea mshahara ambao nao siku zote ni kiduchu tuu.
Kufuatia hali hii, Bibi Maleko, amesema kupitia TanTrade, kila kukifanyika usahili wa nafasi za ajira, Tan Trade itakuwa inaendesha semina elekezi za fursa za kujiajiri kwa vijana wasomi, kwa kuwatumia wakufunzi wa vitendo, wale wasomi vijana walioamua kujiajiri mara baada ya kuhitimu masomo yao, ili wasomi wapya wayatumie mafanikio ya wenzao kama hamasa ya kujiajiri, na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Wakizungumza kwenye semina hiyo, wasomi vijana waliojijiri kwa mafanikio makubwa, walitoa ushuhuda siri ya mafanikio yao, kwa kueleza jinsi walivyoanza kwa mwanzo mgumu, lakini sasa wanavuna mafanikio makubwa.
Akielezea mafanikio yake, mmoja wa wasomi vijana waliofanikiwa kujiajiri ni mwana dada ambaye ni mmiliki wa saloon ya Maznat, Bi. Maza Sinare, ameeleza yeye ni msomi wa sharia ngazi ya shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya kuhitimu, hakutafuta ajira bali alifungua saloon ya kuwapamba ma bibi harusi, hadi sasa amepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuajiri wafanyakazi zaidi ya 20, ambapo ndoto yake sasa ni kutengeza bidhaa za urembo toka Tanzania zenye nembo ya Maznat.
Mwingine mwenye mafanikio ni Emelda Mwamanga mwenye kampuni ya Realim Entertainment ambayo ni wachapishaji wa jarida la Bang, amesema mwanzo aliajiriwa, kasha akaamua kuachana na ajira na kujiajiri katika fani ya uchapishaji wa jarida na kutoa ushauri kwa vijana, sasa amepata mafanikio hadi kujiona muda wote aliokaa kwenye ajira ilikuwa ni kupoteza muda!. Amewashauri vijana wasomi kuwa siri kubwa mafanikio ni kwanza ni kuwa na na ndoto ya unataka kufanya nini, na pili kujiamini kuwa unaweza, na tatu kukata shauri kuanza utekelezaji wa kutimiza ndoto yako.
Moja ya majukumu ya Tanzania Trade Development Authority (TanTrade) ni kuzibaini fursa mbalimbali za kibiashara na kuwawezesha Watannzania ikiwemo kuwajengea uwezo wa kuzichangamkia fursa hizo kujiletea maendeleo na maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Bibi Maleko ameahidi TanTrade itaendelea kutoa fursa kwa watafuta ajira, kupata fursa za kusikiliza shuhuda za waliofaikiwa kwa kujiajiri ili iwe chachu na hamasa kwa wao kujiajiri ili kutengua bomu la ukosefu wa ajira kwa vijana kabla ya bomu hilo halijalipuka.
Source: Mimi mwenyewe nilikuwa eneo la tukio.
Paskali

Attachments
-
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Trade Development Authority (TanTrade), Bibi Jacquline Mneney Maleko.JPG494.9 KB · Views: 397
-
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Trade Development Authority (TanTrade), Bibi Jacquline Mneney Maleko.JPG543.4 KB · Views: 372
-
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Trade Development Authority (TanTrade), Bibi Jacquline Mneney Maleko.JPG458.2 KB · Views: 362
-
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Trade Development Authority (TanTrade), Bibi Jacquline Mneney Maleko.JPG373.4 KB · Views: 361
-
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Trade Development Authority (TanTrade), Bibi Jacquline Mneney Maleko.JPG367.5 KB · Views: 320
-
Mshiriki kutoka MaxCom wanaoendesha Mtandao wa Maxmalipo, akiwahamasisha vijana wasomi kubuni aj.JPG586.2 KB · Views: 313
-
Msomi Mmiliki wa Saloon ya Mharusi ya Maznat, Bibi Maza Sinare, mwenye shahada ya uzamili ya she.JPG363.7 KB · Views: 343
-
Msomi Mmiliki wa Saloon ya Mharusi ya Maznat, Bibi Maza Sinare, mwenye shahada ya uazamili ya sh.JPG637.2 KB · Views: 206
-
DSC_0770.JPG549.5 KB · Views: 153
-
DSC_0787.JPG376.1 KB · Views: 142
-
DSC_0797.JPG500 KB · Views: 173
-
DSC_0796.JPG500 KB · Views: 179