Vijana oeni wanawake wanaowapenda, pesa zako sio chochote ndani ya mapenzi na ndoa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Asikudanganye mtu yeyote yule, pesa haina nguvu yeyote kwenye mapenzi. Pesa hainunui mapenzi, haijawahi kununua mapenzi. Pesa inaweza kununua ngono lakini kamwe haitoweza kununua upendo wa kweli.

Elewa kuwa pesa inagawanyika lakini mapenzi hayagawanyiki. Elewa kuwa pesa ni namba tuu, kamwe haitoshi, yaani huwezi kutosheka pesa lakini mapenzi yanatosha na kujitosheleza. Bado hujanielewa.

Wakati unafikiri ukipata V8 na jumba la ghorofa na akaunti yenye bilioni 5 ndio kuwa na pesa na mchumba wako atakupendea kisa waesa. Elewa kuwa kuna wenzako wana zaidi ya hiyo V8 yako, wana apartment za ghorofa karibu nchi nzima au Afrika nzima, ni mabilionea. Huwezi jiamini kwenye mapenzi kwa kutumia pesa. Huko ni kujidanganya.

ukiwa na pesa utajihakikishia ngono, chakula, makazi, mavazi na vitu vyote vinavyonunulika. Pesa haitakupa amani ndani ya nyumba ikiwa ndani ya nyumba hakutakuwa na upendo na mapenzi aidha kwa mkeo au kwa watoto wako.

Usitumie nguvu kubwa kuingia ndoani kwa mtu asiyekupenda ati kisa unapesa, au anataka pesa. Kama mwanamke amekupenda kisa unamshahara wa ualimu elewa kuwa kuna wenye mshahara wa Daktari. Kama amekupenda kisa udaktari wako elewa kuwa akija boss wa Madaktari atamchukua mkeo.

Hiyo ni biashara na mapenzi sio biashara. Mapenzi ni hisia za ndani ambazo mtu anakupenda bila sababu yoyote Ile.

Huwezi replace upendo wa mtu lakini unaweza ku-replace pesa za mtu. Ukiachana na mwanamke aliyekupendea pesa hawezi kuumia kwani ataku-replace kwa mwanaume mwenye esa zaidi yako au mnayelingana.

Pesa haiachi jeraha moyoni lakini mapenzi yanaacha jeraha moyoni la maisha. Hakuna kazi ngumu kama ku-move on baada ya kuachwa na mtu aliyekupenda na uliyempenda. Ni kazi ngumu sana.

Mtu aliyekupenda atafurahi na kuishi kwa raha hata kama mnakula ugali dagaa, lakini mtu aliyekupendea pesa hawezi kubali umlishe ugali dagaa.

Mwanamke aliyekupenda hata ufilisike au upatwe na majanga kama kuumwa magonjwa mazito ya kulazwa miaka na miaka kamwe hawezi kukukimbia, lakini kamwe haiwezekani mwanamke aliyekupendea pesa akavumilia siku ukifilisika na kuumwa sana.

Ndio yale mnawaita wanawake ni wabaya lakini kimsingi wala sio wabaya, wabaya ni sisi ambao tunajua kabisa mwanamke huyu hanipendi lakini tulilazimisha kumuoa kisa tuna pesa.

Mwanamke akikupenda hawezi kuchepuka, na kama atachepuka atachepuka nyakati ukiwa unaumwa magonjwa ya kupooza, kisukari au presha inayokufanya usiwe na nguvu za kiume na uume usisimame. Tena atachepuka kwa kificho sana wala usitambue.

Lakini mwanamke akikupendea pesa lazima atachepuka uwe unaumwa au hauumwi. Ni lazima atachepuka kwa sababu ananjaa katika hisia yake ya moyoni, humtoshelezi kinafsi. Kumbuka mapenzi ni hisia na kama hana hisia na wewe automatically umembaka, hawezi kuenjoy sex mkiwa wote. Ingawaje anaweza ku-pretend kuwa anaenjoy.

Mwanamke anayekupendea pesa hana shukrani, hana subira kwa chochote atakachokitaka kutoka kwako. Akikuomba pesa labda ni laki tano, atataka umtumie laki saba. Hapo atafurahi lakini furaha ya muda.

Ukimtumia hiyohiyo laki tano atasema huyu naye nimemwambia antumie kiasi hiki halafu anatuma kilekile, hata hajiongezi lakini mwanamke akikupenda akikuomba laki tano hata ukimpa laki mbili atashukuru mno na kukuambia usijali. Huo ni Upendo.

Tafuta Mwanamke anayekupenda kama unampango wa kuishi maisha mazuri yenye furaha. Mwanamke anayekupenda atahitaji upendo wako tuu, kama ni pesa mtatafuta wote. Huyo anakupenda.

Mwanamke anayekupenda haihitaji mambo mengi ni kama sisi tunavyowapenda wao. Atahitajika umpende pekeake tuu, umheshimu na kumjali kama mkeo/mpenzi wake, lakini mwanamke ambaye anakupendea pesa anamashrti mengi na ambayo kila siku yanabadilika badilika.

Leo anataka simu ya Samsung kesho atakuambia ameona kwa rafiki yake Iphone, na yote ukimfanyia anafurahi kwa muda tuu kisha masharti mengine yanatokea.

Ukitafuta Mwanamke anayekupenda hautakuwa mtumwa wa maisha na mtumwa wa wanawake. Bali utaishi kwa raha huku mkisaidiana na mkeo/mpenzi wako kutatua changamoto za maisha.

Ukioa mwanamke mpenda pesa utakuwa na kazi kuu mbili, mosi; kutatua changamoto za mkeo ambazo hazitatuliki, pili, kutatua changamoto za maisha na kimsingi kama mkeo anakuoa changamoto zisizotatulika automatically huwezi tatua changamoto za maisha.

Muhimu: Hata ukimpata anayekupenda usiache kufanya wajibu na majukumu yako ya kuzalisha mali na kuhudumia familia kwa uwezo uliobarikiwa.

Taikon acha nipumzike sasa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Tafuta pesa ufanikishe Malengo yako, uishi vizuri wewe na familia uliyo toka.
👉Kutafuta pesa ili kumridhisha mtu, ni kosa kubwa Sana.

Screenshot_20230815-102545_1.jpg
 
Katika umri wangu huu,wa miaka kadhaa nimethibitisha pasina shaka Mwanamke hapendi,bali Mwanaume ndio anapenda.
99% ya Wanawake wanaolewa na Wanaume walio tayari kuanza maisha ya ndoa.Mwanamke ataanza kuvutiwa na wewe namna utavyoanza Ku mu care.

Hayo mambo ya Wanawake kupenda mnayaleta nyie Wanaume wa kizazi hiki,ambapo haina justification yoyote.Issue kuu ni maadili-ndugu zetu waarabu wanawake wanachaguliwa Wanaume kama ilivyokuwa zamani huku Afrika but ndoa zao huzisikii zina makando kando mengi maana wanawake wamelelwa katika maadili na wanajua wajibu wao.
 
Umesema kweli kabisa,pesa sio kila kitu kwenye mapenzi/ndoa,ingawa ukiwa nayo inanogesha kama vile kutia sukari kwenye chai,ila vijana wengi hawatakuelewa hapa,wanatamani pesa ili wawe na wanawake wengi wenye tamaa na wasio na mapenzi ya kweli kwaaajili ya kufanya nao ngono,na mwisho wa siku anavyoona wanamkimbilia anajua wanampenda kumbe wanaipenda ile pesa yake...
 
Kijana wa kiume tafuta pesa uishi vizuri upate mwanamke ambae hamjatofautiana sana level ya kiuchumi ili uache kujistukia kila mwanamke anafata vihela vyako....
Binti wa kike tafuta hela upendeze angalau mwanaume akikufata asisikie harufu ya njaa na kama ni mwanaume kamili atakuhudumia tu kwa uwezo wake bila kuhisi amechukua nafasi ya baba yako. Hizi tabia za kuomba hela za kodi ya nyumba mara vocha mara sijui hela ya kula ndo mnaonekana wadangaji while ni basic needs unapaswa ujihudimie mwenyewe

changamoto za mapenzi hata masikini wanazo tutafute hela regardless wa kike au kiume.
 
Back
Top Bottom