Kwa bahati mbaya wengi ya Vijana hawajui historia yangu na hivyo hujikuta katika mkanganyiko mkubwa wakiwa wanajaribu kujadiliana na mimi. Hoja yako ndugu yangu haiko sahihi, mimi si miongoni mwa "HIGH CLASS" au "PRIVELEDGED FEW" mimi ni mtoto wa masikini, niliyekulia kijijini kabisa Usukumani kwetu. Ila nataka ufahamu kuwa mafanikio yangu ya kimaisha, kiuchumi na kisiasa kunatokana na Chama Cha Mapinduzi..,malezi ya Mzee wangu Makamba, Jakaya, Kinana na wengineo yamenifikisha hapa nilipo.
Kuniambia kuwa sijawafikiria Vijana wa Vijijini katika post hii, nasema ni uelewa wa taratibu sana wa kile nilichokiandika, nikitaja Vijana waje kwenye CCM kwani ndiko kwenye fursa namaanisha Vijana wote na namaanisha fursa za aina zote, wala sibagui kuwa ni graduates tu ama vijana wa mjini pekee...jaribu kusoma na kuelewa kabla haujachangia.
Mtoa mada nakuelewa sana ila andiko lako lina upotoshaji mkubwa, sidhani ni ndoto zipi ambazo unataka zitimie kwa vijana waliokwisha KUKATA TAMAA na maisha yao. Sio kweli kuwa kila kijana anataka kuwa kiongozi ndani ya ccm, vijana wana mahitaji mengine zaidi ya uongozi, ndio maana najaribu kukueleza wewe unazungumzia THE PRIVILEGED FEW, tazama vijana WANAOCHUKUA MADARAKA ndani ya ccm ni wale wale WABARIKIWA WACHACHE huku wengine wakiwa wapambe na wabeba mikoba. Kwako ni katika wale wachache wenye hulka ya kujikomba kwa watawala wa sasa na kutimiza malengo yao na nyie kutokea kwenye njia hizo. Sio sawa vijana KUJIBANZA-BANZA kwa wakubwa na watoto wao ili watoke kama wewe. Nashukuru kwa kuwa mwungwana kwa kujibu "comments" kiungwanaNitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao.
Na wewe unajiita mwanasiasa pia? Hii nchi kwisha kabisa.
Nafikiri huyu Mhe. Mjumbe wa Bunge Maalum ana tatizo kwenye kuelezea na kufafanua NDOTO ZA VIJANA WA KITANZANIA. Vijana wa kitanzania wana ndoto nyingi zaidi ya uongozi lakini ZIMESHAZIKWA NA MIFUMO mibaya iliyoasisiwa na ccm. Tukatae tukubali tukiendelea na ccm basi TUKUBALI KUTAWALIWA NA WATOTO KUTOKA FAMILIA CHACHE BARIKIWA NCHI HII na hata kama tutaongozwa na vijana kutoka familia maskini kama ya huyu mtoa mada lakini bado tutakuwa tunatimiza mahitaji na matakwa ya WABARIKIWA WACHACHE ambao wamejibariki kwa rasilimali za UMMA. Lazima mtoa mada afanye utafiti kwanza kabla ya kuja kuwaambia vijana wahamie ccm, wakafanye nini au WAKAKUTE LIPI JIPYA?Makonda hivi ndoto gani tena au sikuelewi? Tangu tupate uhuru CCM ndio inatawala, ni juzi tu vimekuja hivi vyama vingine na kimsingi ni baada ya uhitaji kuwepo uhitaji utokanao na CCM kutotimiza ndoto. Asilimia kubwa ya maeneo yapo chini ya Ccm ajabu ndio yanatisha kwa ufukara, ccm wameua elimu yetu tutegemeayo vijana ambao ndio ndoto zetu zingetimia. Sisi hatuna wazazi viongozi kuturithisha uongozi ndoto zitimieje?? Sisi wengine dadazetu wana sura mbaya hawawezi kupendwa na viongozi japo watupe nafasi za upendeleo kama wakuu wa mikoa na wilaya, hizo ndoto zitatimiaje Makonda?? Acha dharau bwana wewe. Tumekusikia ukidai 300,000 hazikutoshi wakati sisi huku mtaani hiyo hata kwa mwaka ni ngumu na tunakadi zachama au unadhani ndoto zetu ni kuwauzia kadi za Ccm kipindi cha uchaguzi? Au unadhani ndoto zetu ni kuvaa tishet na kofia mnazotupa wakati wa uchaguzi??
Mkuu kabla sijaja CCM, naomba unijibu maswali matatu tu
Ingefaa sana iwapo ungeainisha mafanikio ya hao "vijana" uliowatolea mfano kuwa "ndoto zao zimetimia" ili tufahamu walikuwa na ndoto gani (zaidi ya kupata vyeo / tu).
Kwa mafanikio, ninamaaisha kwa jamii nzima ya waTanzania kuwaletea maisha bora.
Iwapo unachokisema kwenye bandiko lako ni kuwavutia tu vijana waje "kupiga hela" etc., kwangu mimi ninaona ni propaganda "hasi" kwa chama chenu.
Ninashauri ungehamasisha vijana wa Tanzania (ukiwa mwenzao) wafanye kazi popote walipo kwa juhudi na maarifa ili kujiletea maendeleo yao na jamii zao, mwishowe nchi nzima.
Ni bahati mbaya sana kwamba vijana wengi siku hizi mnadhani vyama vitaleta maendeleo yoyote kwa taifa. Ni bahati mbaya zaidi kuwa vijana wenyewe ndiyo mnaojipambanua kuwa na elimu. Sasa wasio na elimu sijui ndiyo wakoje. Loh!
Tafadhali ainisha "ndoto zilizotimia" sambamba na majina ili vijana wenzio wafahamu ulichoandika badala ya hii "who's who", waambie "who done what".
Ni ushauri wangu kwako na vijana wengine. Jaribuni kufikiria zaidi ya vyama.
Well said brother..vijana wameshakuelewa.
Hivi mtoto wa mvuvi anakuwa mvuvi kwa hiyari au analazimika tu?
mjinga mjibu kwa kiasi cha ujinga wake....kwani mtoto wa mwanasiasa anakuwa mwansiasa kwa hiyari au analazimika tu.?