vijana na wazee kuhusu ulaya

Mabagala

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,477
325
vijana wa zamani walikuwa wakilazimishwa kwenda ulaya au amerika,tena walikuwa hawapendi,wako tayari kufa lakni wasiende ulaya. Vijana wa sasa wako tayari kufa waende ulaya,hawalizimishwi,hawakamatwi ila wenyewe wanaenda tena kwa kujilipia. Sweet slavish!
 
nilidhani viazi ulaya

haya mengine ngoja nijifunze kudance kwanza ili nikienda huko nisiabishwe na clementine. Ocol na lawino kazi sana
 
Unadhani ni kwa nini vijana wa zamani walikuwa hawapendi kwenda ulaya na kwa nini vijana wa sasa hivi wanapenda kwenda ulaya?
 
kongosho jifunze na kunywa whisky,sigara, na ukubwa
 
Mi nataka kwenda Uropa,maana si kila mtu anaenda huko!

Kila mtu ulayaa....ulayaaa....ulaya... Kunani ulayaaa...!
 
vijana wa zamani walikuwa wakilazimishwa kwenda ulaya au amerika,tena walikuwa hawapendi,wako tayari kufa lakni wasiende ulaya. Vijana wa sasa wako tayari kufa waende ulaya,hawalizimishwi,hawakamatwi ila wenyewe wanaenda tena kwa kujilipia. Sweet slavish!
Vijana wa kizamani walikuwa wanalazimishwa kwenda Ulaya ili wawe ni watumwa lakini vijana wa kisiku hizi wanajipeleka wenyewe ulaya kwa sababu ya hali ngumu ya Maisha hapo kwetu Tanzania.

Unadhani ni kwa nini vijana wa zamani walikuwa hawapendi kwenda ulaya na kwa nini vijana wa sasa hivi wanapenda kwenda ulaya?
Mkuu Young_Master umemuuliza swali zuri sana lakini ameshindwa kulijibu mimi nimemjibu.
 
Mi ntaenda hata kwa miguu kama kunafikika!!
Lakini Ulaya ya siku hizi hakuna kitu zaidi ya Mabarabara Mazuri, Miji ni misafi na Majumba ya Magorofa yanayofika karibu ya mbinguni. Njaa huku kazi hakuna kazi zenyewe ni kubeba mabox bora huko nyumbani kama una kazi yako huko nzuri Mkuu Lizzy bora usije huku maisha magumu pia huku.
 
Sikujijua kama mie ni kijana wa zamani! I'm so disappointed with myself!
By the way, hivi ujana unaishia miaka mingapi?
 
Lakini Ulaya ya siku hizi hakuna kitu zaidi ya Mabarabara Mazuri, Miji ni misafi na Majumba ya Magorofa yanayofika karibu ya mbinguni. Njaa huku kazi hakuna kazi zenyewe ni kubeba mabox bora huko nyumbani kama una kazi yako huko nzuri Mkuu Lizzy bora usije huku maisha magumu pia huku.

MziziMkavu kwani kubeba box kuna ubaya gani?!

Angalau huko nikilipa kodi ntajua inaenda wapi..
Mwisho wa mwezi/wiki nna uhakika wa kupokea
mshahara wangu bila matatizo yoyote...n.k
Sio nakula vumbi huku na mshahara anaambiwa serikali haina pesa yakunilipa!!
 
Back
Top Bottom