Vijana mliokuwa mnasubiri u DC vaaeni GWANDA sasa

msambaru

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
245
109
Vijana wengi ndani ya ccm walikuwa wanasikilizia zawadi ya u DC wameula wachuya na kama hawatajali wakate shauri na waahidi kumuacha shetani na mambo yake yote na kwamba watakuwa waaminifu kwa CDM ili nchi ikombolewe.
 
Siasa za vyeo zitatumaliza, zinatafuna nchi kupitia ccm hadi sasa, napingana na invitation hiyo; Wakae huko huko ambako kuwa mchapakazi ni dhambi kuwa mwadilifu ni kosa,kusema ukweli ni kituko etc?
 
Wasikate tamaa bado kuna ukatibu tarafa. kata, afisa mtendaji tarafa, kata na nyingine zinzofanana na hizo.Kudadadadeki
 
Na mimi mwenyewe niliomba sana niwe DC pale Arusha lakini dah imekula kwangu!
 
kabisaaaaa!!,kuna wanaojiita wana mashirikisho ya vyuo vya elimu ya juu..............wanatumiwa km ngazi ya watu kufanikiwa sidhani km kuna hata mmoja aliyepata uDC ,kazi yao kutoa matamko yasiyo na tija,vijana amkeni kabla jua halijawa kali mtaumwa macho.
 
Huko unauhakika watapata uDC? Siasa za vyeo ni hatari ni bora ukaifuata dira ya chama kuliko ukafuata cheo.......tumeona mwaka 2005 idadi ya wategemea vyeo ilikuwa kuliko idadi ya vyeo.... tukashuhudia baraza kubwa sana la mawaziri..... na yale mabilioni ambayo hatujui hata yalipokwenda.....kuongezwa kwa wilaya na mikoa iliangalau wapambe wapate nafasi bila kujali mzigo wa gharama kwa mlipa kodi ambaye ni mtanzania maskini.... mwisho wa yote ni kuanza kushindana katika nafasi chache zilizopo...kutumia za fitina na kuchafuana ili mpate sababu ya kumwagana...... tupeane vyeo kwa kuangalia uwezo na uadilifu wa mtu na si kwa jinsi alivyopiga debe au urafiki wetu...
 
Vijana wengi ndani ya ccm walikuwa wanasikilizia zawadi ya u DC wameula wachuya na kama hawatajali wakate shauri na waahidi kumuacha shetani na mambo yake yote na kwamba watakuwa waaminifu kwa CDM ili nchi ikombolewe.

Wenzio wapo siriazi wewe
unasema wameula wa chuya,
bana?!
 
Back
Top Bottom